Wanajamvi naomba tujadili bila ushabiki swala la mauaji ya kijana wa CCM jimbo la IRAMBA.
Kwanza najiuliza haya
1.Baada ya polisi kupewa taarifa juu ya fujo ambazo zingetokea katika mkutano kwanini hawakuchukua hatua za kuimarisha ulinzi katika mkutano huo?
2.Kwa sababu mkutano ulikuwa na kibali ni dhahiri kwamba polisi walikuwa na jukumu la kutoa ulinzi.Na kama fujo zilitokea wakati polisi wapo ni dhahiri kwamba nina mashaka na uwezo wa jeshi letu la polisi juu ya uwezo wa kutuliza fujo au vurugu
3.Taarifa zinaonyesha kwamba kijana aliefariki dunia hakufia katika eneo la mkutano na haikuwa wakati wa mkutano.Upi ni uhakika juu ya kifo cha kijana huyu? Askari polisi waliokuwa katika eneo la mkutano wanatakiwa nao wawe mashahidi namba moja kueleza kilichotokea.
4.Kama CHADEMA ndio wauaji,mbona maeneo yote waliyopita hakukutokea mauaji? Kwanini IRAMBA na sio MTWARA na LINDI?
5.Kama ni kweli kwamba vijana walirusha mawe kwa sababu eti viongozi wa CHADEMA walimkashifu mbunge wao,mbona LUSINDE nae alitukana viongozi wa CHADEMA kule Arumeru,je wanachadema nao walitakiwa kurusha mawe? polisi walitakiwa kuwakamata vijana wote waliorusha mawe na kuleta vurugu katika mkutano ule kwani ndio waliokuwa walinzi wa amani katika mkutano ule.Kama hawakufanya hivyo kuna walakini kati ya jeshi la [polisi na kutokea kwa vurugu zile tena kwa makusudi.
6.MY TAKE:-NINAOMBA UCHUNGUZI WA KINA UFANYIKE JUU YA MAUAJI HAYA NA KUANGALIA NI KWA KIASI GANI VIONGOZI WA CCM NA CHADEMA WANAHUSIKA NA MAUAJI HAYA NA MAJIBU YAWEKWE HADHARANI.MWISHO NAMUOMBEA MAREHEMU ALAZWE MAHALA PEMA PEPONI.