Mazishi ya marehemu Yohana Mpinga aliyekufa Ndago - Singida yafanyika

MAMA POROJO

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
4,974
785
Mazishi ya marehemu Yohana mpinga aliyeuawa na vijana wanaodaiwa kuwa wafuasi wa CHADEMA yanafanyika hivi punde katika kitongoji cha Kibaya kijiji cha Songambele kata ya Ndago wilaya ya Iramba.

Mkuu wa mkoa, naibu katibu mkuu CCM tanzania bara john Chiligati na mbunge wa Iramba Mwigulu Nchemba na wanaCCM wengi wamejitokeza.

Watu ni wengi sana.

Waombolezaji wanasema waambie jamaa wa upande wa pili waje kuzika. Hawapo hapa hata mmoja.

marehemu alikuwa katibu wa vijana wa ccm wa kata ya ndago


wabunge takribani 7 hadi 8 hivi wa CCM walikuwepo.

CDM haijatuma mwakilishi kama CCM wanavyofanya kwenye misiba ya CDM, kwa mfano wa Regia Mtema, Wangwe na Bob Makani.

Source: Mimi mwenyewe.
 
Wasiishie kuzika tu wahakikishe na wale waliokuwa wanamtegemea wanasaidia hadi mwisho .
 
Waombolezaji wanasema waambie jamaa wa upande wa pili waje kuzika. Hawapo hapa hata mmoja
 
...Tulishasema siku nyingi Magulu Chemba ni janga la kitaifa ! Sasa mkimaliza mje tena na zile sinema zenu za urongo kama Kova na ndipo mtakapojua huyo Magulu ni cha mtoto na ubitozi wake wa kuvaa skafu na chupi za bendera ya taifa ni wa kizamani !! Video zitawaambua hao polisiccm..
 
Kweli kabisa mwigulu anahusika na hili. Mda mwingine nilifikiria wala sijapata picha pale ambapo Mnyika angeli uawa au kujeruhiwa. Angeshangilia sana Jinga Nchemba.
 
RIP yohana mpinga, najua haikuwa matakwa yako kuanzisha fujo zilizo gharimu maishaa yako, ni mapenzi ya mwigulu kutumia njaa kali ya wananchi kuwanunua walete fujo. damu yako itamlilia milele
 
Mungu aiweke roho yake mahali inapostahili! kama alitumika kuvuruga chadema kwa malipo au ahadi amevuna alichopanda! na ni onyo kwa wengine wenye mipango kama hii! ni huzuni sana kupoteza ndugu na hasa kijana kama huyu ila tujiepushe kuamshana hasira na huyu mpuuzi mwigulu ndiye chanzo cha haya yote damu ya huyu kijana iwe juu ya kichwa cha mwigulu!!
 
Back
Top Bottom