Tume ya Katiba
JF-Expert Member
- Apr 6, 2012
- 4,896
- 1,862
Inasikitisha sana
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Inasikitisha sana
Hivi huyu jamaa nae anatakiwa akahojiwe na polisi eeeh.mwigulu umeua kijana wa watu sasa roho yako kwatu, damu ya kijana huyu na iwe juu ya uso wako milele na milele
Wanachosahau CCM ni kuwa uungwaji mkono kwenye kundi la vijana kwa sasa ni chini ya 35%. Sasa vurugu wanazochochea sijui watazihimili vipi kwa wazee waliobaki nao.Kama polisi wataendelea kutumika kuhujumu CDM tutashuhudia vifo vingi 2015
Hakuna haja ya kuunda tume kwani waliokuwepo eneo la tukio wanaeleza kuwa kuna picha za video zilikuwa zinachukuliwa. Naona huo utakuwa ushahidi mzuri zaidi kwani hata polisisiemu nao huwa ni vituko tu hawana msaada wowte zaidi ya kutunga uongo tu.Wanajamvi naomba tujadili bila ushabiki swala la mauaji ya kijana wa CCM jimbo la IRAMBA.
Kwanza najiuliza haya
1.Baada ya polisi kupewa taarifa juu ya fujo ambazo zingetokea katika mkutano kwanini hawakuchukua hatua za kuimarisha ulinzi katika mkutano huo?
2.Kwa sababu mkutano ulikuwa na kibali ni dhahiri kwamba polisi walikuwa na jukumu la kutoa ulinzi.Na kama fujo zilitokea wakati polisi wapo ni dhahiri kwamba nina mashaka na uwezo wa jeshi letu la polisi juu ya uwezo wa kutuliza fujo au vurugu
3.Taarifa zinaonyesha kwamba kijana aliefariki dunia hakufia katika eneo la mkutano na haikuwa wakati wa mkutano.Upi ni uhakika juu ya kifo cha kijana huyu? Askari polisi waliokuwa katika eneo la mkutano wanatakiwa nao wawe mashahidi namba moja kueleza kilichotokea.
4.Kama CHADEMA ndio wauaji,mbona maeneo yote waliyopita hakukutokea mauaji? Kwanini IRAMBA na sio MTWARA na LINDI?
5.Kama ni kweli kwamba vijana walirusha mawe kwa sababu eti viongozi wa CHADEMA walimkashifu mbunge wao,mbona LUSINDE nae alitukana viongozi wa CHADEMA kule Arumeru,je wanachadema nao walitakiwa kurusha mawe? polisi walitakiwa kuwakamata vijana wote waliorusha mawe na kuleta vurugu katika mkutano ule kwani ndio waliokuwa walinzi wa amani katika mkutano ule.Kama hawakufanya hivyo kuna walakini kati ya jeshi la [polisi na kutokea kwa vurugu zile tena kwa makusudi.6.MY TAKE:-NINAOMBA UCHUNGUZI WA KINA UFANYIKE JUU YA MAUAJI HAYA NA KUANGALIA NI KWA KIASI GANI VIONGOZI WA CCM NA CHADEMA WANAHUSIKA NA MAUAJI HAYA NA MAJIBU YAWEKWE HADHARANI.MWISHO NAMUOMBEA MAREHEMU ALAZWE MAHALA PEMA PEPONI.