Mazingira yangu ni yapi?

Heshima kwako Mshana Jr.
Kuna hili suala la Mabadiliko ya Tabianchi na Athari zake kwa mazingira yetu. Nanukuu:-
"Hakuna juhudi zozote za kuwekeza kwenye elimu ya utunzaji wa mazingira.. Na ikitokea ni siasa tupu na ujinga mwingi... Sheria na kampeni za kuwa na dust bins kwenye vyombo vya usafiri sijui vimeishia wapi
Mazingira ni maisha
Mazingira ni afya
Mazingira ni mafanikio
Bila afya hakuna maisha na bila maisha hakuna mafanikio
Mazingira yako ndio afya na maisha yako..ndio ustawi na mafanikio yako.. Yatunze yakutunze!"
Mwisho wa kunukuu
e.g. Kama ni kupanda miti - basi ipandwe miti inayoendana na hali iliyopo kwa mfano tupande miti ya Asili inayostahimili ukame na mioto kichaa (ref. ilivyotokea Huko Rombo) ile miti iliyokuwepo i.e. iliyopandwa kwa mazoea haikuhimili moto-Asili uliotokea.
  • kama ni kilimo basi yapandwe mazao yanayostahimili ukame na sio kupanda tu kwa mazoea.
  • Kama ni ufugaji ; tufuge aina na idadi ya mifugo kulingana na uwingi wa malisho yaliyopo na iwe pia ni mifugo yenye tija zaidi.
Kwa kifupi ni kwamba nasi Wanadamu tuliopo kizazi hiki tubadilike na kuachana na kufanya mambo kwa mazoea- "Business as Usual" Matumizi ya rasilimali zetu yazingatie mabadiliko ya Tabianchi tunayoenda nayo ili kuweka uwiano sawa kwetu sisi na kwa vizazi vijavyo.
 
Kongole nyingi kwako ndugu
Mshana Jr kutoka moyoni kabisa nathubutu kusema wewe ni Mmoja wa WAZALENDO wa kweli wa taifa hili,
Achana na wale wachumia tumbo waliojificha Kwenye kivuri Cha siasa uchwara za kiuwendawazimu!

Nadiriki kutoa pongezi za dhati Kwa mchango wako umeandika kiuzalendo Sana mpaka umenifanya nitafakari mambo mengi Sana yanayoendelea hapa Nchi ikiwemo na Serikali kushindwa hata kupangilia miji na vijiji na kusabisha yote Hayo uliyoyaandika hapa maana naamini Kama wangekua makini Kwenye Hilo swala Hayo ya utunzaji mazingira yangekuja automatically!

Niishie hapa aaaaagh!
 
Asante sana Dumas the terrible [emoji1545][emoji1545][emoji1545]
 
Kwa kifupi ni kwamba nasi Wanadamu tuliopo kizazi hiki tubadilike na kuachana na kufanya mambo kwa mazoea- "Business as Usual" Matumizi ya rasilimali zetu yazingatie mabadiliko ya Tabianchi tunayoenda nayo ili kuweka uwiano sawa kwetu sisi na kwa vizazi vijavyo.[emoji1545][emoji1545][emoji1534]
 
Tunazo kampuni rasmi za usafi zilizopewa kutunza, kuhifadhi na kufanya usafi kwenye maeneo mbalimbali mijini.. Hizi kampuni ni kichekesho na ni kichefuchefu mpaka unajiuliza
Je wenye hizi kampuni wana weledi na uzoefu wa kutosha kwenye hii kazi muhimu sana?
Je wana vitendea kazi na nguvu kazi ya kutosha?
Je wanaowapa hizi tenda wanajiridhisha uwezo wa wanaowapa kazi ama ndio 10% inaamua kila kitu?
Maana haiwezekani uchafu uzolewe barabarani na kutupwa juu ya bustani zilizoko pembezoni na katikati ya barabara .. Mwisho wa siku bustani zinageuka matuta makubwa ya uchafu uliogandiana
Still watu hawachukuliwi hatua na ikija tenda nyingine wanapewa![emoji848][emoji2827]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…