Luqman Van Maliki
Member
- Aug 19, 2021
- 6
- 7
Mazingira mazuri ni jambo muhimu na bora kwa kila maisha ya mwanadamu hivyo ni muhimu kuyalinda na kuyatunza.
Umuhimu wa kuendelea kutunza mazingira ni jambo linalo sisitizwa sana duniani kwa sasa. Hali ya mazingira kadiri ya watu inavyozidi kuongezeka uharibifu wa mazingira huongezeka pia.
Maisha ya mwanadamu yanategemea afya nzuri ,afya ya mtu inaanzia kwenye mazingira yake. Mazingira ndio kila kitu kwa sababu ndio vitu vinavyomzunguka mwanadamu kama vile hewa, mimea na maji hayo yote ni mazingira.
Kila mwananchi anayo dhima ya kutunza mazingira na kuhakikisha kuwa mazingira yanaendelea kuwa salama licha ya kwa sasa dunia na nchi kunaendelea kuharibiwa kwa kutotunza vizuri mazingira.
Kimsingi mazingira ni jambo muhimu linalohitajiwa kutunzwa na kila mtu licha ya kwamba serikali ndio inalo jukumu kubwa la kuendelea kutunza mazingira ya nchi yake.
Umaskini ndio jambo la kwanza linaloweza kusababisha uharibifu wa mazingira hasa maeneo ya vijijini kwasababu wakazi wengi watakuwa wanakata miti hovyo kwa ajili ya kujipatia mbao ili kujipatia mahitaji yao.
Ilivyo ni kwamba ukataji miti hovyo madhara yake yanaeleweka huweza kupelekea uharibifu mkubwa wa mazingira ikiwemo mmomonyoko wa ukosefu wa mvua, hali hii inaweza kupoteza viumbe hai walioko msituni.
Uchafuzi wa mazingira unaweza kusababisha mabadiliko ya tabia ya nchi. Hili jambo zaidi pale ambapo ukataji miti hovyo wa kihole ukitamalaki na ufugaji usio wa kisasa wa kufuga mifugo mingi ambayo inaweza kusababisha uharibifu wa udongo.
Serikali ya jamhuri ya muungano inaendelea kuleta juhudi na kutoa elimu kwa wananchi wake kutunza mazingira kwa lengo la kupata mazingira bora ya kuishi kwa sababu bila mazingira bora na mazuri maisha ya viumbe hai yatakuwa mashakani.
Machapisho kadhaa nchini yalichapishwa ili kutoa elimu kwa watanzania kama toleo maarufu la sera ya taifa kuhusu mazingira la mwaka 2012.
Jarida hilo maalumu lilieleza na kufafanua umuhimu wa kutunza mazingira kwasababu ubora wa mazingira unaweza kuwa chachu ya maendeleo ya sehemu husika. Wawekezaji wengi wanakwenda kuanzisha miradi yao sehemu iliyo na mazingira salama na rafiki.
Sheria mbalimbali zimeendelea kutungwa nchini kwa lengo la kuendelea kutunza mazingira vizuri kwa mfano sheria ya usimamizi wa mazingira ya mwaka 2004 imeeleza kinagaubaga namna nzuri ya utunzaji wa mazingira kwa lengo la kuwalazimisha kutokuchafua mazingira.
Viongzi na wizara mbalimbali zimeendelea kutoa elimu kwa lengo la kutunza mazingira licha yakuwa kazi kubwa inahitajika kuendelea kufanyika ili kulinda na kuyaacha mazingira yakiwa salama ili vizazi vijavyo vikute hali ya mazingira ipo salama kama ilivyorithishwa.
Mazingira ni nyenzo muhimu ya kulinda afya za watu endapo tu wakazi wake au wamiliki wa viwanda wakipunguza utumizi mwingi na mbaya wa gesi viwandani.
Endapo dunia ikiendelea kama ilivyo sasa huku watu wakiendelea kuongezeka basi hali ya mazingira miaka kumi ijayo itakuwa mbaya sana.
Ukataji miti hovyo na uvunaji wa misitu bado linaendelea huku uchomaji wa misitu ukiendelea kufanyika kwa hivi endapo mambo haya yataendelea mazingira yataharibika zaidi tofauti na ilivyo sasa. Watu wanatakiwa kuacha jambo hilo haraka iwezekanavyo.
Maeneo ya mijini utupaji taka hovyo umeendelea kukithiri licha ya kwamba serikali bado inajitahidi kuendelea kupambana na janga hilo lakini bado nguvu kubwa inahitajika zaidi.
Utupaji wa taka hovyo na chupa za plastiki ni moja kati ya mambo ambayo yamekithiri sana maeneo ya mjini huku watu wakiwa hawajali na hawana kama wanafanya uchafuzi wa mazingira.
Serikali inao mzigo mzito sana kwa wanachi wake kwa ajili ya kutioa elimu kwa kushirikiana na wadau wa mazingira kuhakikisha ulimaji wa kizamani unaoharibu udongo unaachwa mara moja kama sera ya mazingira ya mwaka 2019 ilivyobainisha bayana juu ya jambo hilo.
Katika kukabiliana na uchafuzi wa mazingira na kutunza mazingira umoja wa mataifa ulianzisha shirika la mazingira ili kutoa elimu duniani na kila nchi wanachama ijue namna nzuri ya kukabiliana na uchafuzi wa mazingira.
Umoja wa mataifa umeanzisha siku ya mazingira duniani ambayo ni juni 5 ya kila mwaka siku hiyo ilianza mwaka 1972 ambako kidunia ilifanyika mjini mjini Stokholm Sweden.
Mkutano mkuu wa mwaka jana kuhusu mazingira ambao ulifanyika nchini Colombia mwenyeji wake Rais Ivan Marquez akihutubia na kusema kuwa “wakati wa kuchukua hatua ni sasa iwapo tutajali sasa na siku zijazo” hali ya mazingira ya dunia inazidi kuwa mbaya kila nchi inawajibu wa kutunza mazingira yake.
Kitengo cha umoja wa mataifa kinachohusu mazingira kiliwahi kunukuliwa kuwa wanashauri angalau kutunza sehemu ya ardhi kwa asilimia 30 hadi ifikapo mwaka 2030.
Kwa sasa nchi nyingi ongezeko la watu limekuwa kubwa zaidi hivyo maeneo mengi yaliyokuwa wazi yanatumika kwa ajili ya makazi ya watu na mifugo yao kwahiyo serikali lazima ziwe wazi kudhibiti maeneo hayo ili eneo la ardhi kwa asilimia 30 liwe wazi.
Mazingira ni jambo muhimu la kwanza linalopiganiwa na kila nchi hivyo kila mwanachama anatakiwa na anayo dhima ya kutunza mazingira yake bila uchafuzi wa hali ya hewa na kuharibu udongo, serikali inawajibu mkubwa wa kuhakikisha mazingira yanabaki salama kwa kuwapa wananchi wake elimu inayohusu mazingira.