Mtaka haki2021
Member
- Jul 20, 2021
- 5
- 13
MAZINGIRA BORA YA BIASHARA KUCHAGIZA UKUAJI WA UCHUMI.
Unapozungumzia uchumi imara wa nchi huwezi acha kuzungumzia biashara kama kiungo muhimu katika sekta hio kwani shughuli nyingi zinategemea biashara mfano mzuri wa shughuli hizo ni uvuvi, kilimo, uchimbaji madini, utalii na shughuli nyinginezo.
Tunapozungumzia mazingira wezeshi ni pamoja na ulinganifu wa kodi sambamba na ukubwa wa biashara hii inamaanisha kwamba kila mtanzania kwa nafasi yake anao wajibu wa kulipa kodi ili kuchangia maendeleo ya nchi kwa namna moja au nyingine.
Lakini kwa sasa kodi imeonekana kama adhabu hasa kwa wafanyabiashara kwani wamekua wakikwepa suala hilo kwa kutumia kila mbinu, hii inawezekana kwa sababu ya kutokua na elemu ya umuhimu wa kulipa kodi, au utitili wa kodi ambao umekua ukilalamikiwa na wafanyabiashara wengi.
Serikali ikiweka utaratibu mzuri wa ulipaji wa kodi ambao hautaathiri shughuli hii huenda wafanyabiashara wengi watalipa kodi na kuongeza wigo kwa wajasiriamali wengine kuingia zaidi katika shughuli za biashara. Lakini pia serikali na wadau wa biashara na uchumi wanatakiwa kutoa elimu ya ulipaji kodi kwa wananchi ili kuongeza uelewa kwa wananchi ambao ndio walipa kodi.
Dunia ya sasa uchumi umekua ukichagizwa na biashara kutokana na umuhimu wa sekta hio ndio maana nchi nyingi zimekua zikipambana kuimarisha nyanja hiyo.
Mwaka 2015 Tanzania ilikuja na sera ya uchumi wa viwanda lengo likiwa ni kuimarisha uchumi kupitia shughuli mbalimbali ikiwemo sekta ya biashara nakadhalika.