Mazingatio ya Maisha yako ya kila siku

biasharaTz

Senior Member
Apr 14, 2016
154
225
Maelekezo ya maisha katika Qur'an

*1_Usizungumze kwa ukali (3:159)*

*2_Jizuie na hasira (3:134)*

*3_Kuwa mwema kwa wengine (4:36)*

*4_Usiwe mwenye kiburi(7:13)*

*5_Samehe wanaokukosea (7:199)*

*6_Zungumza na watu kwa upole (20:44)*

*7 _Shusha sauti yako (31:19)*

*8_ Usiwakejeli wengine (49:11)*

*9_Watendee wema wazazi wako (17:23)*

*10 _Usiseme maneno ya kuwakosea adabu wazazi wako (17:23)*

*11_ Usiingie chumba cha wazazi wako bila kuomba idhini (24:58)*

*12_Andikishianeni mnapokopeshana (2:282)*

*13Usifuate rai ya yeyote kibubusa (2:170)*

*14_Muongezee unayemdai muda wa kulipa deni kama ana hali ngumu (2:280)*

*15_ Usile riba (2:275)*

*16_ Usijihusishe na rushwa (2:188)*

*17_ Usivunje ahadi (2:177)*

*18_Tunza amana (2:283)*

*19_ Usiufiche ukweli unaoujua (2:42)*

*20_ Wahukumu watu kwa haki (4:58)*

*21_Simamia haki (4:135)*

*22_Mali za marehemu zigawiwe kwa warithi wao (4:7)*

*23_Wanawake pia wana haki yakurithi (4:7)*

*24_Usile Mali ya yatima (4:10)*

*25_ Watunze yatima (2:220)*

*26_Msiliane Mali zenu kwa dhuluma (4:29)*

*27_Patanisheni miongoni mwa wanaogombana (49:9)*

*28_Jiepushe nakuwajengea watu Dhana mbaya (49:12)*

*29_ Msipelelezane na msisengenyane (2:283)*

*30_Msipelelezane au msisengenyane (49:12)*

*31_ Toeni katika njia ya Mwenyezi Mungu (56:7)*

*32_Jihimizeni kuwalisha maskini (107:7)*

*33_ Watafuteni wenye kuhitaji muwasaidie (2:283)*

*34_Usitumie ovyo pesa zako (17:29)*

*35_Msiharibu sadaka zenu kwa masimulizi (2:264)*

*36_ Wakirimu wageni (51:26)*

*37._Waamrishe watu kutenda mema baada ya wewe mwenyewe kuyatenda (2:44)*

*38_Msifanye uharibifu katika Ardhi (2:60)*

*39_Msiwazue watu kuingia misikitini (2:114)*

*40_Piganeni na wale wanaowapigeni tu (2:190)*

Hakika Mwenyezi Mungu anajua zaidi
 

mwenye shamba

JF-Expert Member
May 31, 2015
872
1,000
Hiyo namba 40 ikizingatiwa ulimwenguni tutamalizana.hko juu umetiririka vzr ila hyo 40 ndo inazaa wale jamaa wa somalia,nigeria na siria
 

nzalendo

JF-Expert Member
May 26, 2009
7,824
2,000
Kama kweli hayo yangefuatwa,basi DUNIA ingekuwa salama kuishi na hata kule ALEPO tusingepafahamu.
 

biasharaTz

Senior Member
Apr 14, 2016
154
225
Hiyo namba 40 ikizingatiwa ulimwenguni tutamalizana.hko juu umetiririka vzr ila hyo 40 ndo inazaa wale jamaa wa somalia,nigeria na siria
Kwa hiyo unakubaliana na hiyo aya kuwa jamaa wanajitetea?? Hivi kwa mtazamo wa haki nani alieanzisha uharibifu katika uso huu wa dunia kama sio mataifa ya magharibi na huku yakijinasibu kuwa yanatengeneza ilhali yanaharibu!!??
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom