Maziko ya Abdulwahid Sykes 1968

Idu...
Ndiyo nasema kuwa unapenda kujadili historia hii lakini bahati mbaya huna ujuzi wa mengi katika somo hili.
Chukua muda uisome hii historia ndipo uje tufanya mjadala.

Kuondolewa majina ya Abdul Sykes, Sheikh Hassan bin Ameir, Sheikh Suleiman Takadir, Mshume Kiyate kwa kuwataja wachache katika historia ya TANU haikuwa uzembe.

Hassan Upeka aliyekuwa moja wa watafiti na waandishi wa historia hiyo chini ya Chuo Cha CCM Kivukoni anasema kuwa Dr. Mayanja Kiwanuka aliyekuwa kiongozi wa jopo alikataa kupokea taarifa za Abdul Sykes.

Haya nimeyaeleza katika kitabu cha Abdul Sykes.
Hiyo book review ya Brian Eccles naifahamu sana.

Nyingine ni ya John Iliffe na James Brennan.
Sishangai aliyoandika.

Ila nashangaa kwa nini hakueleza kuwa kuwa kweli hao, '' Abdul Muslim associates,'' hawamo katika historia lau kama mchango wao ni muhimu.

Yawezekanaje kuwa baba na watoto wake wote wameshika uongozi katika harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika na wote hawamo katika historia ya TANU.

Baba muaisisi na wanae wote waasisi.
Tuje kwa Martin Kayamba.

Martin Kayamba hakuhusika katika kuunda AA.
Hili si jambo la sisi kuvutana.

Kleist Sykes kawataja wote walioasisi AA katika mswada wa kitabu alioandika kabla hajafa.
Sasa mswada huu ni kitabu: Daisy Sykes Buruku, ''Kleist Sykes The Townsman,'' ''Modern Tanzanians,'' Ilife (Ed) 1973.

Kleist Sykes yuko pia katika Dictionary of African Biography (DAB), Oxford University Press, New York, 2011 na mwandishi wa maisha yake ni Mohamed Said.

Nahitimisha kwa kukufahamisha kuwa gazeti la Africa Events lililokuwa na makala yangu, ''In Praise of Ancestors,'' lilikusanywa lote na kutolea katika mzunguko lisisomwe.

View attachment 1797778

View attachment 1797782

Kleist Sykes muasisi wa AA 1929, Abdul, Ally na Abbas waaaisi wa TANU 1954 kadi no 2,3, na 7.
Nina mengi katika historia ya TANU.
Ngumu kumeza. Nitarudi baadae naenda kulima shamba.
 
Ngumu kumeza. Nitarudi baadae naenda kulima shamba.
Idu...
Nilikuwa nasoma Nyaraka za Sykes kisha naziweka pembeni.

Nashindwa kukubali.
Akili yangu inakataa.

Hivi kweli Earle Seaton kashiriki katika kupanga mikakati ya TAA kwenda UNO kutokea 1950 akiishauri TAA Political Subcommittee kwenye mambo mbalimbali.

Jina la Mufti Sheikh Hassan bin Ameir naliona pale kama mwanakamati limeandikwa.
Kwangu kama kwako ilikuwa tabu kumeza.

Sishangai kwa wewe kuona uzito wa historia ya Abdul Sykes.
Nakukaribisha wakati wowote njoo hapa barzani tutajadili historia ya kweli ya nchi yetu.
 
Ni sababu gani zilimfanya ajitoe?
Madagascar,
Kleruu alikuwa hana moja alijualo katika historia ya AA.

Abdul Sykes kwanza alikuwa na mswada wa kitabu alioandika baba yake.

Mswada huu ulikuwa kumbukumbu za baba yake akieleza historia ya vipi babu yake Sykes Mbuwane alikuja Germany Ostafrika kama askari mamluki chini ya Hermann Von Wissman.

Ndani ya mswada huu anaeleza maisha yake chini ya utawala wa Wajerumani hadi WW I akiwa askari ndani ya jeshi la Kamanda Von Lettow Vorbeck.

Anaendelea kueleza utawala wa Waingereza baada ya WW I 1918.
Anaeleza alivyounda African Association 1929 baada ya kukutana na Dr. Kweggiyr Aggrey 1924.

Anaendelea kueleza kilichomsukuma kuunda Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika 1933 kikiwa chama pembeni ya AA.

Hapa katika miaka ya 1930s anaeleza juhudi za Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika katika kujenga shule ili Waislam kama Wamishionari wawe na shule zao akiweka msisitizo wa Qur'an kusomeshwa kama somo katika shule.

Kleist anaeleza ushawishi wa Waislam katika taasisi hizi mbili AA na Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika na nguvu iliyozuka katika kukabiliana na ukoloni.

Abdul haya licha ya kuwa yameandikwa na baba yake lakini kazaliwa na kukua ndani ya historia hii na baada ya WWII na akiwa askari wa KAR ndani ya Burma Infantry akawa anaandika vipi vita hivi vilivyowasaidia Waafrika kujitambua na kuamua kudai uhuru wa Tanganyika.

Yeye binafsi alikuwa na mchango wake katika kuwakabili Waingereza kwanza kupitia Dockworkers Union 1948 akiwa na miaka 24 tu kisha haada ya kuchukua uongozi wa TAA 1950 akiwa na Dr. Vedasto Kyaruzi.

Kipindi hiki ndicho kipindi muhimu sana katika historia ya TAA kwani vijana wengi kutoka Makerere College walijiunga na TAA mjini Dar-es-Salaam pale New Street.

Hiki ndicho kipindi cha bongo za kizazi kipya cha wakati ule akina Hamza Mwapachu na viongozi wengine kutoka Kanda ya Ziwa kama Ali Migeyo, Saadan Abdu Kandoro na Paul Bomani wakaanza kukusanya nguvu zao pamoja kumkabili Gavana Edward Francis Twining.

Abdul na Hamza Mwapachu wanaweka msingi wa kuunda TANU na kutafuta kiongozi mmoja kuongoza harakati za uhuru.

Abdul yeye alimtaka Chief David Kidaha Makwaia ndiye aje TAA waunde TANU.

Mwapachu yeye mtu wake alikuwa Julius Nyerere lakini mwaka wa 1950 Nyerere alikuwa hajulikani wakati Chief Kidaha alikuwa mjumbe wa LEGCO toka mwaka wa 1945.

Abdul Sykes 1950 tayari alikuwa kijana maarufu na kiongozi wa TAA na alikuwa mjumbe katika TAA Political Subcommitee pamoja na Mwapachu, Kyaruzi, Sheikh Hassan bin Ameir na Steven Mhando kwa kawataja wachache.

Huu ndiyo mwaka Abdul Sykes alikwenda Nairobi kufanya mazungumzo na Jomo Kenyatta.
Hii kamati ndani yake alikuwapo Mwanasheria Earle Seaton akitoa ushauri nyuma ya pazia.

Hii ndiyo kamati iliyokuja kuunda chama cha TANU 1954.

Lakini muhimu alieleza mkutano nyumbani kwa Hamza Mwapachu, Nansio, Ukerewe alipokwenda kaongozana na Ali Mwinyi Tambwe agenda kuu ikiwa kupata kauli ya Mwapachu kuhusu kumtia Nyerere kwenye uongozi wa juu kabisa wa TAA.

Hamza alimshauri Abdul kuwa Nyerere asaidiwe ashinde uchaguzi wa 1953 awe President na 1954 TANU iundwe.


Madagascar,
Kuna kitu hapa nataka uzingatie.

Baada ya kurejea kutoka Nansio TAA ikaitisha uchaguzi Ukumbi wa Arnautoglo na Nyerere akagombea nafasi ya urais dhidi ya Abdul Sykes.

Nyerere akapita katika uchaguzi ule kama ilivyopangwa.

Lakini hakuna popote katika historia ya TANU hili limeelezwa wala Nyerere mwenyewe hajapatapo kusema kuwa aligombea nafasi hiyo dhidi ya Abdul Sykes.

Jiulize kwa nini?

Haya ndiyo Abdul aliyoandika katika kueleza chimbuko la TANU na Abdul akaeleza vipi alikuja kujuana na Nyerere 1952.

Inasemekana Nyerere hakupendezewa na historia hii.
Abdul akajitoa katika ule mradi akamwacha Dr. Kleruu.

1622025355365.png


1622025443033.png

Kulia Abdul Sykes na Hamza Mwapachu

1622025633732.png
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom