Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 360,354
- 829,593
Uzezeta ni hali ya kutokuwa na akili kamili..kwahiyo karibia kila kitu hutegemea kufanyiwa na wengine ..kwamba ni hali ya kutojiweza wala kujimiliki kwa asilia miamoja. Kuna uzezeta wa aina mbili
1. Ulemavu kwa kuzaliwa
2. Uzezeta kutokana na malezi na mifumo
Zezeta ni mtu mwanadamu mwenye uzezeta. Kuna wanyama pia mazezeta kwa kuzaliwa na kwa malezi. Kama ukikuta panya inakula sahani moja na paka, basi hiyo paka tayari ishakuwa zezeta.
Mitaani kuna wale watoto wa kishua ama wa geti kali, hawa tunawaita mazezeta, hawajui mengi hawafanyi mengi na wengi wamelainika kama mlenda ama ni bonyebonye kama supu ya mapupu. Kuna baadhi yao.
. Hata ukiwapiga na maganda ya mayai huumia au
. Hawawezi hata kuvunja biskuti achilia mbali kutafuna
Hakuna waoga kama watoto wa geti kali
Wanyama wapo wa aina mbili. Wa porini na wa kufugwa; na hawa wa kufugwa nao wako wa aina mbili. Wa kufungiwa muda wote wakipewa kila kitu humo humo na wale wa kufunguliwa asubuhi na kufungiwa jioni.
Chukulia mfano rahisi wa kuku wa kienyeji na kuku wa kufugwa. Kuku wa kienyeji hapangiwi pa kwenda, hapangiwi chakula, hapangiwi cha kufanya. Ni utashi wake binafsi ndio humkumbusha kurudi nyumbani ama kudoea chakula cha nyumbani. Huko nje huona mengi, hujua mengi, hukutana na mengi. Kwahiyo kuku wa kienyeji ni sharp na yuko imara kimwili na kiakili.
Njoo kwenye kuku wa kufugwa sasa. Huyu dunia yake ni kwenye banda 24/7. Malezi ya aina hii humlemaza akili na viungo. Mwisho hubaki kuwa zezeta
Hawezi kujitafutia chakula
Hawezi kujitafutia kinywaji
Hawezi kukimbia hatari
Hajui chochote zaidi ya kunywa, kula, kunya na kulala mpaka siku atakapochukuliwa machinjioni
Washika kalamu wetu wa ndani wamekuwa kama kuku wa kufugwa. Ni mazezeta;
Hawana uwezo tena wa kutafiti habari
Hawana uwezo tena wa kuandika habari za kiuchunguzi
Hawana uwezo tena wa kuandika habari fikirishi kwa maslahi mapana ya taifa
Hawana uthubutu wa kuandika uhalisia...wamebaki kuandika kile wanachopewa..kile kilichokwisha andaliwa..
Hakuna kuhoji
Hakuna kudadisi
Hakuna kuuliza
Hakuna kuchagiza
Hatuwalaumu sana kwakuwa mfumo ndio umeshawalea hivyo nao wameshaona ndio uhalisia. Sasa wanapotokea wa nje wenye uhuru kamili kuhoji, kudadisi na kuandika mambo yanayotuhusu bila woga na bila kificho. Wao wanabaki kuwashangaa na pengine kuwabeza ama kuwakejeli.
Methali kuntu ya leo: KUFA KUFAANA!