Wakuu nawaza kumnunulia mke kigari kidogo maana anasisitiza yeye anaweza kuendesha kigari kidogo kwa sasa bado hajazoea heka heka za barabara.
Mawazo yangu yanawaza Mazda Demio toleo la 2008 au 2011. Swali langu kwa wataalam wa magari, je gari hili lina changamoto gani?
Napenda mwonekano wake wa ndani kuliko IST hivyo naona itamfaa. Pia naona ina mwonekano wa kike.
Natanguliza shukrano.