Mayor Jacob: Kwa mfumo mpya wa kodi ya majengo serikali imepoteza shs bil 33 tofauti na mwaka jana

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,572
26,885
DAR ES SALAAM

Serikali awamu ya tano chini ya Rais John Pombe Magufuri,imepoteza kiasi cha shillingi billioni 32 kutoka kipindi walipo hamisha kodi ya majengo kwenda TRA kipindi cha July 2016 mpaka may 2017

Katika Matarajio ya halmashauri za Dar es salaam tatu kipindi hicho walitegemea kukusanya Biilion 7 Temeke,Billioni 11 ilala na Billioni15 kinondoni. Hivyo Dar es salaam ilikuwa ikusanye Billioni 33 kutoka chanzo kimoja tuh cha mapato ya kodi za majengo(property tax)

Badala yake TRA kwa mwaka wote wa fedha wamekusanya 1 Billioni tuh.Hivyo hakuna halmashauri yeyote ya Dar es salaam itapata mgao kutoka TRA kwa mwaka huu wa fedha unaoisha.

Imani yangu si kwamba serikali ilikuwa haitambui matarajio ya athari ya kuondoa chanzo hiko kwenye mamlaka za serikali za mitaa(halmashauri)
Ila ulikuwa ni mkakati wa kukomoa wapinzani,wasifanye maendeleo

Fedha hizo zingejenga madarasa,hospitali,zahanati,magari ya wagonjwa,,barabara,mitaro ya maji ya mvua,na fedha za wanawake na vijana.

Je wewe unamaoni gani?

Na Boniface Jacob
Mstahiki Meya
Manispaa ya Ubungo

Senior councilor Ubungo
 
Hili nililiona!Baada ya upinzani kuongoza jiji,wakaamua kuhamisha vyanzo vya mapato vya halmashauri ili viende TRA na hatimaye serikali kuu!Hawakujiandaa,hawakuwa na utaratibu mzuri wa kukusanya na kufuatilia kama halmashauri!Lengo ni kukomoa tu upinzani,matokeo yake ndio hayo!
 
Hivi kwanini viongozi wa serekali hii wamekua wabaguzi wa ubaguzi uliopitiliza? Yani mtu akiwa mshabiki tu si uanachama ni mshabiki tu wa chama kengine, viongozi umuhesabu km si raia. Athari ya haya Mambo uwezi kuiona kwa kiwango kikubwa leo ila kuanzia miaka sita huko na kuendelea mtajuta kwa mnachokitengeneza leo
 
Back
Top Bottom