Godfreymkolokoti
Member
- Sep 3, 2014
- 11
- 3
KOCHA wa Yanga, Marcio Maximo na kiungo Mbrazil, Andrey Coutinho, wamewasikia Simba kisha wakacheka sana, unajua kwanini? Simba baada ya kumuona straika,Genilson Santos ¡®Jaja¡¯ juzi Jumatano Uwanja wa Taifa walibeza sana wakadai kumbe hana lolote ni maneno tu ya kishabiki mtaani.
Simba waliwakejeli Yanga kwa madai kwamba licha ya mchezaji huyo kufunga bao pekee kwenye mechi hiyo ya kirafiki dhidi ya Thika United ya Kenya, lakini hatishi kama Emmanuel Okwi wao au Pierre Kwizera.
Lakini Maximo na Coutinho wamewajibu kwa mkato na kuwaambia kwamba watulie ligi ianze ndiyo watamjua Jaja ni nani.
Maximo na Coutinho wamesisitiza kwamba Jaja hana mambo mengi kama wanavyodhani, yeye ni mtu wa kutengenezewa na kutupia tu hataki wala hajui vyenga. Maximo alisema: ¡°Unapomzungumzia Jaja huwezi kumfananisha na mchezaji kama Coutinho au Ngassa (Mrisho) au Niyonzima (Haruna).¡±
¡°Jaja ni mtu wa kusimama kati na kazi yake ni kufunga mabao, mpasie mpira afunge na siyo kutembea pembeni kusaka mpira, yeye anatumbukiza tu.¡±