Akiwa ziarini nchini Brazil Rais J.M Kikwete amekutana na aliyekuwa kocha wa Timu ya Taifa ya Tanzania.Marcio Maximo.
Maximo alichukua fursa hiyo kwa kushauri vilabu vya soka Tanzania lazima vianze maandalizi kuanzia ngazi ya chini kuanzia umri wa miaka minane na kuendelea ili kupata wanasoka na timu bora.
Pia alimshukuru Raisi kwa ushirikiana aliompa kwa muda wote alikuwa nchini kama kocha wa Timu ya Taifa.
Kwa upande wake Raisi alimshukuru Maximo kwa kuwa uwepo wake Tanzania ulisaidia kuiweka nchi katika ramani ya mchezo huo.
Wakati huo huo Maximo amekanusha uvumi ulizaga kuwa huenda akarudi Tanzania kuja kuzifundisha kati ya Timu za Azam au Yanga na kusema kuwa hajafanya mazungumzo na vilabu hivyo na kwa sasa ana mkataba na Timu ya Demokrata ya nchini Brazil.
unajua tunaweza kwenda mbali na kufikiria juu ya masuala ya 'strategies', sera, mikakati nk juu ya mikutano kama hii lakini mwishowe sio ajabu unakuta hakuna lolote bali target kubwa za wawakilishi wetu ni mambo haya haya! Anaendelea kuweka rekodi na najua itachukua miaka mingi Mtanzania mwingine kuifikia