Mawio limefutwa, wachochezi wanadunda!

Paul Alex

JF-Expert Member
Jul 14, 2012
4,342
9,824
Waandishi wawili wa habari, Simon Mkina na Jabir Idrissa walitoka mahabusu juzi, Jumanne jijini Dar es Salaam, ambamo waliswekwa baada ya gazeti lao, Mawio kufutwa na Serikali.
Wamepoteza gazeti. Wakaporwa uhuru kwa kuhojiwa na polisi mchana wote na sehemu ya usiku; na hatimaye kutupwa mahabusu.
Sasa kila siku ni kiguunjia, kuripoti polisi hadi watakapopelekwa mahakamani au kuambiwa ‘yameisha.’
Haya yote yanatokana na Serikali, kupitia Waziri wa Habari, Nape Nnauye kufuta gazeti la Mawio kwa madai kuwa linaandika uchochezi; na hivyo wahariri wake kuitwa wachochezi.
Mawio limekuwa likiripoti yaliyopo kwa njia ya uchunguzi kama wizi, migogoro na taharuki; mengi yakiwa yale yaliyosababishwa na watawala au wenza wao; na lengo likiwa kufahamisha umma na kuhimiza watawala kuchukua hatua.
Zawadi pekee kwa maripota na wahariri kwa jitahada zao za kuanika mambo na kuonya kabla hali haijawa mbaya, ni kuwaita wachochezi, kuwasaka kama wahalifu, kufuta gazeti lao na kuwasweka rumande.
Kumbe Serikali ina maana tofauti ya uchochezi. Tuangalie kauli zifuatazo na kuzilinganisha na maandishi ya gazeti linalotoa hadhari na lililofutwa.
Mara ngapi tumesikia kauli hii: “Ikulu mtaisikia redioni.” Ikiwa na maana kwamba hata mkishinda katika uchaguzi, hamtaingia Ikulu. Haya ni manukato? siyo uchochezi? Wanaoambiwa wajisikie vipi? Wafanye nini?
Umewahi kusikia hili? “Mapinduzi yalikuwa Unguja, hayakuwa Pemba; na Serikali itakuwa ya Unguja!”
Hivi wanaoambiwa kwa kauli ya kibaguzi na jeuri ya kifisadi, wanyenyekee na kusema “Insha Allah?” Wanafikiri nini? Wahusika ‘hawajafutwa’
Hili je? “Serikali ya Zanzibar haikupatikana kwa vikaratasi” na pengine wakisema “hatuwezi kutoa urais kwa makaratasi” – wakiwa na maana ya karatasi za kupigia kura na kuongeza, “Kama nanyi mnataka, basi pindueni.” Kauli chokozi inayotia kidole jichoni. Anayeambiwa ajisikie vipi? Wahusika ‘hawajafutwa.’
“Wewe (Maalim Seif), utaishia umakamu wa rais. Basi!” Anayeambiwa ndiye amekuwa akipigana kisiasa tena kwa utulivu; katikati ya propaganda kuu, kwamba “nchi yetu ni ya kidemokrasia na haina ubaguzi wa aina yoyote!” Soma kishindo cha radi ya kiangazi: “Mmekuja Unguja na njaa zenu; rudini kwenu!” Wanaoambiwa wanajisikiaje? Wafanye nini?
Waweke maneno pembeni na kuanzisha vita vya kuondoa ubaguzi; kwa misaada na ushirikiano kimataifa? Mhusika “hajafutwa.”
Eti nini? Sikilizeni anayejiita mnyofu. “…tutashinda hata kwa bao la mkono…” Ni kauli katikati ya vuguvugu la kampeni za Uchaguzi Mkuu mwaka jana. Ofisa wa “chama tawala” anatangazia taifa na dunia; kwa kiburi na jeuri isiyomithilika.
Anapeleka ujumbe gani kwa washindani kutoka vyama vingine? Anaeneza demokrasia? Anataka washindani wafanye nini? Anataka Tume ya Uchaguzi ikitangaza kuwa wameshindwa; wafanye nini na Serikali ijibu vipi? Mhusika “hajafutwa.”
Nina zaidi ya kauli 100 za aina hii zilizotoka vinywani mwa viongozi wa Serikali na chama kinachopanga Ikulu. Wahusika wanafyatua maneno kwa jeuri: Maneno ya kukera, kuudhi, kuchukiza, kutisha, kuchokoza, kudhalilisha, kubagua; yote kwa shabaha ya kuchochea majibu kwa njia ya mapigano – vita! Vyombo vya habari vimenukuu baadhi ya kauli hizi na nyingine zimesomwa katika maandiko mbalimbali; katika vijarida na mbao kwenye vijiwe vya vijana na wazee.
Wako wapi walio wakali sana ndani ya Serikali, wawezao kupambana na uchochezi huu, unaoweza kuangamiza Taifa? Uko wapi ‘mkono mrefu’ wa Serikali ambao hutamkwa kwa majigambo pale polisi wanapokuwa wakikimbiza “mwizi wa karanga.”
Upande huu kuna watoa kauli zinazotaka watu wachukie, wakasirike, waghadhibike; wachukue walichonacho na kuanza kumalizana; huku Serikali ikiwaangalia kana kwamba imewafadhili kwa kazi hiyo.
Upande mwingine kuna habari na taarifa za ‘kigazeti’ Mawio, kinachoanika wanaopanda mbegu ya maangamizi na kuonya juu ya mifarakano iwezayo kuleta umwagaji damu.
Waziri Nape anasema Mawio ndilo linafanya uchochezi. Analifuta. Hawezi kujifuta. Hawezi kufuta wengine waliobobea katika uchokozi wa kibabe na uchochezi.
Kufuta chombo cha habari ni kurejesha jamii katika nyakati za ujima. Ni kukataa elimu na maarifa. Ni kupora uhuru wa habari. Ni kupanda mbegu ya woga miongoni mwa wananchi. Ni kuingiza Taifa gizani.
Nape hana tofauti na mawaziri waliomtangulia, waliotumika kudhibiti habari kwa kukaa wamepakata na kubusu sheria ya kidikteta inayotumika kufuta vyombo vya habari, Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976.
 
haha jabir idriss katika ubora wako...nenda tu kaendelee kuripot central hakuna namna nyngne
 
Wanajidanganya sana. Dunia ya leo si ile tena.
Hata baba wa taifa alishashtuka longtime kabla hajang'atuka.

Nape tii masharti ya walioko juu siku wakishuka wewe usiogope kulipa
 
Unachofurahia hapa ni nini?
tatizo kubwa alilonalo jabir ni kwamba, ana uwezo mdogo sana either kielimu au kutafuta ukweli kabla hajarusha habari. nilishawahi kumsikia akieleza kuhusiana na hoja kwenye kipindi star tv, na wanamwita "mwandishi wa habari mwandamizi", hoja zote alizozitoa ni zile zinazotokana na hisia binafsi, sio zile alizofanyia utafiti kabla ya kuongea. nilimwangalia na kumwonea huruma sana kwasababu anaongea akiamini ana uelewa kumbe hakuna kitu. watu wa aina yake serikali yafaa iwashughulikie kabisa wasiwepo kwenye vyombo vya habari, wakae tu kufanya kazi nyingine lakini sio za kulisha wananchi matango. siku nyingine akatoa hoja kwamba dpp amepewa mamlaka makubwa mno hatakiwi kupitia majalada ya pccb. hajawahi kumwona dpp kwanza aelezwe kimisingi ya kisheria ni kitu gani kinamfanya pccb apeleke majalada kwa dpp?....hajui hata utendaji ukoje lakini anavyoongea anajiamini mno kwasababu huwa wanakuwa wamelishwa maneno na upande mmoja. na siamini kama huwa hawapewi hela ili kutumika kama silaha dhidi ya mtu mwingine. nilifurahi kusikia serikali imemkamata. ajifunze kwa waandishi wenzake kama wako kama yeye..na kwanini yeye tu anakamatwa, ina maana ana akili sana au hana akili sana?
 
Wengi bado wanakumbuka kile kituko kilichotokea Muhimbili miaka kadhaa nyuma, aliyetakiwa kufanyiwa operesheni ya kichwa alifanyiwa ya mguu na yule aliyetakiwa kufanyiwa ya mguu akafanyiwa ya kichwa!. Hao ni madaktari ambao wanawekwa kwenye kundi la wasomi, kundi la watu wa tabaka la juu, walifanya madudu ya aibu. Sishangai kuona sekta ya habari na yenyewe ikijaa madudu. Hakuna sekta hapa nchini ambayo haina madudu. Uandishi wa habari wetu na wenyewe ni muendelezo ule ule wa madudu yetu. Badala ya watu kuhabarishwa na kuelemishwa vyombo vya habari vimemezwa kwenye ushabiki na uandishi usio na utafiti. Jamii ikijaa ujinga hata wenye akili na wenyewe huonekana kuwa ni sehemu ya wajinga pia. Too bad.
 
tatizo kubwa alilonalo jabir ni kwamba, ana uwezo mdogo sana either kielimu au kutafuta ukweli kabla hajarusha habari. nilishawahi kumsikia akieleza kuhusiana na hoja kwenye kipindi star tv, na wanamwita "mwandishi wa habari mwandamizi", hoja zote alizozitoa ni zile zinazotokana na hisia binafsi, sio zile alizofanyia utafiti kabla ya kuongea. nilimwangalia na kumwonea huruma sana kwasababu anaongea akiamini ana uelewa kumbe hakuna kitu. watu wa aina yake serikali yafaa iwashughulikie kabisa wasiwepo kwenye vyombo vya habari, wakae tu kufanya kazi nyingine lakini sio za kulisha wananchi matango. siku nyingine akatoa hoja kwamba dpp amepewa mamlaka makubwa mno hatakiwi kupitia majalada ya pccb. hajawahi kumwona dpp kwanza aelezwe kimisingi ya kisheria ni kitu gani kinamfanya pccb apeleke majalada kwa dpp?....hajui hata utendaji ukoje lakini anavyoongea anajiamini mno kwasababu huwa wanakuwa wamelishwa maneno na upande mmoja. na siamini kama huwa hawapewi hela ili kutumika kama silaha dhidi ya mtu mwingine. nilifurahi kusikia serikali imemkamata. ajifunze kwa waandishi wenzake kama wako kama yeye..na kwanini yeye tu anakamatwa, ina maana ana akili sana au hana akili sana?
Kwahivyo unataka kusema kilichochangia gazeti la Mawio kufutwa hakishabihiani sana na habari zinazohusu uchaguzi Zanzibar
 
Majuzi kwenye sherehe za Mapinduzi, vijana wa CCM walipita mbele ya wageni waheshimiwa ambao ni viongozi wa kitaifa wa CCM na mabango yao na mengine yakisomeka MACHOTARA HIZBU ZANZIBAR NI NCHI YA WAAFRIKA.

Hivi inawezekanaje waliohusika na uandikaji wa mabango ya hatari kiasi hicho wakaachwa bila hata ya kuchukuliwa hatua na badala yake Wahariri wa gazeti la Mawio ambao wanatahadharisha kupitia uandishi wa makala zao kuwa hilo ni jambo la hatari sana, cha kushangaza hilo ndilo linaonekana kosa kubwa la 'kufa mtu' hadi waziri mwenye dhamana ya Habari anaamua kushusha rungu lake na kulipiga LIFE BAN hilo gazeti!
 
Jecha ndio mchochezi nambari moja wa fujo.Lakini mpaka leo anadunda mtaani.Mawio imeonewa.
Hata Membe na Warioba wamenukuliwa kushangaa yanayoendelea Zanzibar.
 
Waandishi wawili wa habari, Simon Mkina na Jabir Idrissa walitoka mahabusu juzi, Jumanne jijini Dar es Salaam, ambamo waliswekwa baada ya gazeti lao, Mawio kufutwa na Serikali.
Wamepoteza gazeti. Wakaporwa uhuru kwa kuhojiwa na polisi mchana wote na sehemu ya usiku; na hatimaye kutupwa mahabusu.
Sasa kila siku ni kiguunjia, kuripoti polisi hadi watakapopelekwa mahakamani au kuambiwa ‘yameisha.’
Haya yote yanatokana na Serikali, kupitia Waziri wa Habari, Nape Nnauye kufuta gazeti la Mawio kwa madai kuwa linaandika uchochezi; na hivyo wahariri wake kuitwa wachochezi.
Mawio limekuwa likiripoti yaliyopo kwa njia ya uchunguzi kama wizi, migogoro na taharuki; mengi yakiwa yale yaliyosababishwa na watawala au wenza wao; na lengo likiwa kufahamisha umma na kuhimiza watawala kuchukua hatua.
Zawadi pekee kwa maripota na wahariri kwa jitahada zao za kuanika mambo na kuonya kabla hali haijawa mbaya, ni kuwaita wachochezi, kuwasaka kama wahalifu, kufuta gazeti lao na kuwasweka rumande.
Kumbe Serikali ina maana tofauti ya uchochezi. Tuangalie kauli zifuatazo na kuzilinganisha na maandishi ya gazeti linalotoa hadhari na lililofutwa.
Mara ngapi tumesikia kauli hii: “Ikulu mtaisikia redioni.” Ikiwa na maana kwamba hata mkishinda katika uchaguzi, hamtaingia Ikulu. Haya ni manukato? siyo uchochezi? Wanaoambiwa wajisikie vipi? Wafanye nini?
Umewahi kusikia hili? “Mapinduzi yalikuwa Unguja, hayakuwa Pemba; na Serikali itakuwa ya Unguja!”
Hivi wanaoambiwa kwa kauli ya kibaguzi na jeuri ya kifisadi, wanyenyekee na kusema “Insha Allah?” Wanafikiri nini? Wahusika ‘hawajafutwa’
Hili je? “Serikali ya Zanzibar haikupatikana kwa vikaratasi” na pengine wakisema “hatuwezi kutoa urais kwa makaratasi” – wakiwa na maana ya karatasi za kupigia kura na kuongeza, “Kama nanyi mnataka, basi pindueni.” Kauli chokozi inayotia kidole jichoni. Anayeambiwa ajisikie vipi? Wahusika ‘hawajafutwa.’
“Wewe (Maalim Seif), utaishia umakamu wa rais. Basi!” Anayeambiwa ndiye amekuwa akipigana kisiasa tena kwa utulivu; katikati ya propaganda kuu, kwamba “nchi yetu ni ya kidemokrasia na haina ubaguzi wa aina yoyote!” Soma kishindo cha radi ya kiangazi: “Mmekuja Unguja na njaa zenu; rudini kwenu!” Wanaoambiwa wanajisikiaje? Wafanye nini?
Waweke maneno pembeni na kuanzisha vita vya kuondoa ubaguzi; kwa misaada na ushirikiano kimataifa? Mhusika “hajafutwa.”
Eti nini? Sikilizeni anayejiita mnyofu. “…tutashinda hata kwa bao la mkono…” Ni kauli katikati ya vuguvugu la kampeni za Uchaguzi Mkuu mwaka jana. Ofisa wa “chama tawala” anatangazia taifa na dunia; kwa kiburi na jeuri isiyomithilika.
Anapeleka ujumbe gani kwa washindani kutoka vyama vingine? Anaeneza demokrasia? Anataka washindani wafanye nini? Anataka Tume ya Uchaguzi ikitangaza kuwa wameshindwa; wafanye nini na Serikali ijibu vipi? Mhusika “hajafutwa.”
Nina zaidi ya kauli 100 za aina hii zilizotoka vinywani mwa viongozi wa Serikali na chama kinachopanga Ikulu. Wahusika wanafyatua maneno kwa jeuri: Maneno ya kukera, kuudhi, kuchukiza, kutisha, kuchokoza, kudhalilisha, kubagua; yote kwa shabaha ya kuchochea majibu kwa njia ya mapigano – vita! Vyombo vya habari vimenukuu baadhi ya kauli hizi na nyingine zimesomwa katika maandiko mbalimbali; katika vijarida na mbao kwenye vijiwe vya vijana na wazee.
Wako wapi walio wakali sana ndani ya Serikali, wawezao kupambana na uchochezi huu, unaoweza kuangamiza Taifa? Uko wapi ‘mkono mrefu’ wa Serikali ambao hutamkwa kwa majigambo pale polisi wanapokuwa wakikimbiza “mwizi wa karanga.”
Upande huu kuna watoa kauli zinazotaka watu wachukie, wakasirike, waghadhibike; wachukue walichonacho na kuanza kumalizana; huku Serikali ikiwaangalia kana kwamba imewafadhili kwa kazi hiyo.
Upande mwingine kuna habari na taarifa za ‘kigazeti’ Mawio, kinachoanika wanaopanda mbegu ya maangamizi na kuonya juu ya mifarakano iwezayo kuleta umwagaji damu.
Waziri Nape anasema Mawio ndilo linafanya uchochezi. Analifuta. Hawezi kujifuta. Hawezi kufuta wengine waliobobea katika uchokozi wa kibabe na uchochezi.
Kufuta chombo cha habari ni kurejesha jamii katika nyakati za ujima. Ni kukataa elimu na maarifa. Ni kupora uhuru wa habari. Ni kupanda mbegu ya woga miongoni mwa wananchi. Ni kuingiza Taifa gizani.
Nape hana tofauti na mawaziri waliomtangulia, waliotumika kudhibiti habari kwa kukaa wamepakata na kubusu sheria ya kidikteta inayotumika kufuta vyombo vya habari, Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976.
NA BADO MWANAHALISI. NA MIMI NASEMA LIFUTWE TU MAANA HAKUNA NAMNA !!
 
Tatizo si magazeti tatizo ni viongozi wetu vihiyo, hawataki kufikiri zaidi. huu mtindo wa kufungia vyombo vya habari haufai ingawa navyo visiandike mambo kinyume na maadili yao
UCHOCHEZI HAUTAKUBALIKA KAMWE. MAADILI YA UANDISHI LAZIMA YAZINGATIWE
 
mahala popote duniani penye uhuru wa habari lazima kuna limitations zake na ndio maana sheria zinatungwa ili kujaribu kuvi manage kwa sababu bila ya hivyo vyombo hivi ni rahisi sana kuyumbisha na kuleta machafuko nchini. kuhusu sakata hili tumeshasikia maelezo ya serikali ya kwamba ni mara ngapi chombo hiki cha habari, Mawio kimepelekewa onyo kwamba kinakiuka misingi yake lakini hakifuati maelekezo na utaratibu iliopo tangu mwaka 2013. hivi ni serikali gani ambayo ni vumilivu kiasi hiki. tuwe wakweli sometimes. hakiyanani ingekuwa mimi ndio rais nisingekuwa na uvumilivu huu hata kidogo. halafu sasa mbaya zaidi eti wanakimbilia kutoa sababu kuwa wananchi wananyimwa haki yao ya kupata habari ili wapate huruma ya wananchi wakati utumbo wanaufanya wenyewe. ni tabia ya ajabu sana.
Kubenea kwanza hakidhi vigezo vya kuwa mwandishi wa habari na hana maadili hayo. tunajua anawatumikia watu wenye pesa na mifano tunayo.
amekuwa anamtuhumu to the public Lowasa kuwa ni fisadi wa richmond. kila mwananchi mwenye akili anajua nchi nzima. kabla hata hajaamia chadema. akijigamba anaandika habari za kiuchunguzi na za ukweli. kwa maana hiyo ana ushahidi kwa nini Lowasa ni fisadi. lakini leo kafanya nini? ?? Lowasa kaenda wamempokea wamesafisha na basi akaanza kuandika kwenye magazeti yake Lowasa sio fisadi wamemsafisha tayari. hahahahahahah! !! siasa hizi zitatufikisha kweli kwenye uchumi wa kati hizi? ?
itakiwa watu kama kina Kubenea waondolewe kwwnye mfumo wa kujenga taifa kabisa. kwa sababu kwa maadili mabovu alitokuwa nayo anaweza ambukiza wengine wengi. taifa haliwezi songa mbele kama litakuwa na viongozi makanjanja kama hawa! never.
 
chadema asilia tunasema ikiwezekana hata Mwanahalisi walifute nalo. halitusaidii lolote ni wizi tu wa kuwaibia wananchi kwa kununua gazeti lisilo na mwelekeo. eti linajitapa ni gazeti la uchunguzi. watuambie uchunguzi gani ambao tangu waandike umelisaidia taifa hili. mfano uchunguzi waliokuwa wakiandika kwamba Lowasa kafisadi richmond umesaidiaje taifa? ??.
 
UCHOCHEZI HAUTAKUBALIKA KAMWE. MAADILI YA UANDISHI LAZIMA YAZINGATIWE
Na wale waliobeba mabango ya Machotara
Au wale wanaoandika maneno yauchochezi kkwenye Tawi la CCM.
Damu ya ubaguzi itawaumiza.Na hii double standard itafika mahali haitawasaidia
 
Ningesikia Raia Mwema limefutwa, ningeumia sana, kumbe Mawio! Hongera sana Nape Nauye kumbe unafanya kazi? Na hii ndiyo faida ya kuwa na Mawaziri vijana kama yinyi. Mawio laana ya kumponda na kumkejeri Dr.Slaa imewatafuna mpaka wamefutiwa gazeti lao. Kweli nimekubali, malipo ni hapa hapa duniani.
 
Back
Top Bottom