amanda cute
JF-Expert Member
- Oct 27, 2016
- 244
- 456
Nilikua nasikia kuwa mawifi na mashemeji ni mwiba kwa wanandoa nikadhani ni uongo ila kwa sasa ndiyo nimeamini kiukweli. Kuna mawifi zangu kiukweli wamekua ni mwiba mchungu kwangu baada ya kuja kwetu. Nimewashindwa kiukweli kwa majungu na fitina kuwa mimi sifai kuwa na ndugu yao.
Wanadiriki kunisengenya kuwa nimemwekea limbwata mume wangu kuwa hawajali anajali tuu upande wangu. Imetokea siku za karibuni mume wangu kuwa karibu na mimi sana kwa kuzidisha upendo kwangu na kuniona mimi ni muhimu kwake.
Hii imepelekea kuwauma kweli kweli mpaka wanadai nimemwekea limbwata kumbe hakuna lolote hii inatokana na na mahaba ninayompa mpaka kapagawa tuu.
Jamani mawifi tulieni nimpe hubby kitu roho inataka. Inakera sana kwa kweli kuingilia mapenzi ya watu. Huu mchezo hauhitaji hasira acha nimpe vitu adimu.
Poleni na wale wote mnaosumbuliwa na mawifi zenu..