Mawazo na Mitizamo migumu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mawazo na Mitizamo migumu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rweye, Apr 5, 2012.

 1. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #1
  Apr 5, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,053
  Likes Received: 3,083
  Trophy Points: 280
  Ndugu zangu napenda nitumie nafasi hii ili niweke mawazo yangu huru juu ya kile ninachokifikiria kuhusu nini CDM ifanye pale Arusha

  Leo hii tumeshuhudia mahakama ikiacha kazi yake na kuvamia siasa kwa kuamua kutumika kifisadi na kuacha weledi kuchukua mkondo wake na baadae kutoa maamuzi eti CDM wanaweza kukata rufaa ili kesi isikilizwe upya,katika hili nashauri CDM wasiende mahakani tena kwa sababu kuu mbili

  Mahakama ya mwisho katika hili ni wananchi wapiga kura wa Arusha mjini waachwe waamue wenyewe,waliopiga kura na kumchagua Lema walikuwa wana wa Arusha na nina imani kama walimchagua Lema basi hapana shaka Lema ni chaguo lao hata kesho

  Pili,kama CDM kikiamua kurudi mahakamani naiona hasara mara2,kwanza kwa chama make kesi hii itakaa kule mpaka iamriwe nina uhakika si leo na hivyo CDM kukosa jembe hili pale mjengoni,pili hasara kwa wananchi make CCM hawana mpango wa kuwajali wananchi badala yake wanataka kuwatesa wananchi hawa wakae pasipo kuwa na mwakilishi ili kuwakomoa

  Kwa vile CDM wana uhakika wa jimbo na mgombea tayari wanaye nawasihi waambieni NEC waandae uchaguzi ili ndani ya miezi 4 kutoka sasa tuwe na idadi yetu ya makamanda mjengoni,jimboni na katika harakati za ukombozi kupitia M4C

  Ama vipi makamanda?
   
Loading...