Ni kweli baada ya mapumziko ya chakula cha mchana,wabunge wa CCM walianza kulaumiana sana na kumlaumu kwa chinichini Mh.Lembeli na Kangi Lugola kuwa wanamshupalia sana waziri mkuu.
Lawama zinaenda kwa Mwenyekiti wa kamati ya Maliasili na Utalii ndugu LEMBELI kwamba ni kwa nini ameileta report hiyo bungeni badala ya kwenye Chama??kama angeileta ktk chama maanake aibu hii ingemalizwa bila kuipaka matope serikali ya CCM.
Wabunge wa CCM wameadhimia kumlinda Pinda kwa ghalama yoyote asijiudhulu,na badala yake ktk michango yao ya jioni watachangia zaidi kwa mawaziri wanne kujiudhuru na si Waziri Mkuu,mpaka mchana huu tayari kumetokea mpasuko mkubwa,wapo ndani ya CCM wanaoona kujidhuru kwa Waziri Mkuu itakuwa ni sifa mbovu kwa serikali na chama chao..nguvu nyingi ni kumlinda Pinda na kuwatoa kafara wengine.
Wabunge wa CCM mpaka sasa wanarudi mjengoni kupunguza makali ya Lugola na Report ya Lembeli...