Mawaziri wa Tanzania

Mawaziri wa Tanzania

Mr Anold

JF-Expert Member
Joined
Jan 19, 2012
Posts
218
Reaction score
47
Waziri ni kiongozi anaeongoza mamilioni ya watu, ukiachilia mbali wakuu wa mikoa, wabunge, makamanda wa jeshi wa mikoa nk, kumekuwa na ubabaishaji wa hali ya juu katika utendaji na kutufanya watanzania wote kuonekana wapuuzi.

Waziri anropoka hovyo hovyo kama vile yuko juu ya sheria na kuongea tu bila kufanya utafiti na kuhoji kwa kina. Mfano waziri wa elimu kutangaza matokeo bila kufikiria wanaomsikiliza ni watu wenye uwezo gani wa kufikiri.

Waziri kusifia wauaji na kutamba kuwa amefanya kazi nzuri kuua mwandishi Mwangosi, mkuu wa mkoa kutoa kauli tata mfano Mulugo aliwaambia waandishi wa habari Arusha wanapoandika taarifa za serikali wajue wanaweka maisha rehani kwani serikali ina nguvu.

Mimi napendekeza watu hawa wajiuzulu na wafungwe kifungo cha maisha jerezani ili ujuha wanaotubambikiza sisi watanzania waujutie na iwe fundisho kwa wengine.
 
hoja unazo ila uko too general, weka fact, alafu panga hoja zako
 
Ulitaka waziri wa elimu atangaze vipi matokeo? Au ulitaka ayabadilishe?
Mimi nampongeza kwa ujasiri wa kuwa Mkweli.
 
Back
Top Bottom