Mawaziri wa ccm wana uelewa mdogo

Mawaziri wa ccm wana uelewa mdogo

makesy

Member
Joined
Jan 29, 2013
Posts
75
Reaction score
32
Wana jamvi salam
nimesema mawaziri wa ccm wana uelewa mdogo kutokana na kauli wanazozitoa wakati wanajibu hoja cha upinzani.
Waziri anaposimama bungeni anawakilisha serikali na sio chama waziri anapoulizwa swali huku akijua wananchi wanataka kusikia kauli ya serikali, nayeye badala ya kujibi lile swali akaanza mipasho juu ya chama fulani inasikitisha sana na inaonyeshi jinsi wasivyoelewa kuwa madaraka yao ni zaidi ya chama . Mfano tuliona waziri nchimbi alivyosimama wakati wa kuchangia hoja wa wizara ya maliasili na utalii badala ya kusimama kama serikali akasimama kama mbungu na kuanza kusema yote yaliyozungumzwa juu ya kinana ni uzushi.
Ukimuuliza kama amewahi kulifanyia uchunguzi swala hilo hapana, amejuaje kwamba ni uzushi ni ushabiki tu wa siasa.
Jana tulimuona waziri sitta alipoombwa na chadema kutumia mahakama ya afrika mashariki kuchunguza kesi zinazohusu ujangili wa pembe za ndovu, mimi nilitegemea ata waambia chadema wasubiri akaongee na wahusika kuona kama jambo hilo linawezekanz yeye akaanza mipasho eti jina la kinana linawaogopesha chadema hapa sikuona kauli ya waziri bali maneno ya mhuni fulani.
Mwisho naomba niwaambie mawaziri wetu kuwa wasisahau kuwa wananchi tunafuatilia mijadala hii ya benge na swala la ujangili wa meno ya tembo haliwaumizi tu wabunge wa chadema wala wafuasi tu wa chadema bali linawaumiza watanzania wote wenye mapenzi na uchungu na raslimali ya nchi hii bila kujali ni mshabiki wa chama gani hivyo linapoulizwa swali linalohusu mustkabali wa taifa mawaziri wajaribu kulielezea lieleweke na kila mtu. Wasifikiri mjadala unaishia bungeni tu hata huku mitaani wanachama wa vyama mbalimbali wana bishana kuhusu sakata hilo sasa wakijikita kujibu swali kwa ufasaha watampa na huyu wa mitaani uwezo wa kuwajibu wale wanaomshambulia kuhusu viongozi wake kuwa wanamaliza tunu ya taifa
nawasilisha
 
Back
Top Bottom