Mawaziri saba wajiuzuru

Mawaziri saba wajiuzuru

Mtego wa Noti

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2010
Posts
2,631
Reaction score
1,657
Hawa magamba watakoma mwaka huu!
Mawaziri saba wang’oka


HATIMAYE mawaziri saba kati ya nane wakiwemo wanaokabiliwa na tuhuma za
ubadhirifu, wamekubali kuandika barua za kujiuzulu wenyewe kwa kile
kilichoelezwa kuwa ni kukinusuru Chama cha Mapinduzi (CCM).

Habari za kuaminika kutoka mjini Dodoma zimesema kuwa mawaziri hao,
walilazimishwa kujiuzulu katika kikao cha dharura kilichokuwa chini ya uenyekiti
wa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kilichofanyika mara tu baada ya kumalizika kwa
kikao cha Bunge.

Taarifa zimewataja waliokubali kujiuzulu kuwa ni pamoja na Waziri wa Viwanda
na Biashara, Cyril Chami; Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa
na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Mkuchika; Waziri wa Uchukuzi Omari
Nundu; na Waziri wa Afya, Dk. Haji Mponda.

Wengine wanaodaiwa kujiuzulu ni Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja;
Naibu Waziri wa Afya, Lucy Nkya; na Naibu Waziri wa Viwanda, Lazaro
Nyarandu.

Hata hivyo, Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo, ambaye alishambuliwa vikali kwa
kuitwa kinara wa ufujaji, hakuwepo katika kikao hicho kwa madai kuwa yuko nje ya
nchi, anasubiriwa aungane na wenzake kuachia ngazi.

Kujiuzulu kwa mawaziri hao kumekuja baada ya kuzuka kwa mjadala mzito ndani ya Bunge kwa siku mbili mfululizo kuhusiana na tuhuma za ufujaji wa kutisha wa fedha za umma, kiasi cha kusababisha kuwepo kwa azimio la kupiga kura ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu Mizengo Pinda.

Wakati wa majumuisho ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za
Mashirika ya Umma, mwenyekiti wa kamati hiyo, Zitto Kabwe, alilitaka Bunge
kuweka ushabiki na itikadi za kisiasa pembeni na kuazimia kwa pamoja kupiga kura
za kutokuwa na imani na Pinda kutokana na uzembe wa mawaziri wake.

Kabla ya kujiuzulu huko Spika wa Bunge, Anne Makinda, jana alizima hoja ya
kumwajibisha Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, akidai kuwa utaratibu mzima umekiukwa
na hivyo hauwezi kufanyiwa kazi katika kikao cha sasa cha Bunge.

Makinda alisema hayo alipokuwa akitoa mwongozo uliyoombwa na Mbunge wa
Bumbuli, January Makamba (CCM) kuhusu suala hilo na kudai kuwa wanaoendesha
mchakato huo itabidi wasubiri hadi Bunge lijalo.

Makinda ametoa hoja hiyo, wakati idadi kubwa ya wabunge
wakiwa wametia saini za kumwajibisha Waziri Mkuu kutokana na ubadhirifu
mkubwa unaowahusisha mawaziri watano wa serikali.

Mchakato wa utiaji saini unaosimamiwa na Zitto Kabwe, ulikuwa
ukiendelea kwa kasi na habari za kuaminika zinasema kuwa idadi ya walio tayari
kuweka saini zao inaweza kufika wabunge 200.

Akuzungumza jana mchana, Zitto alisema kuwa hadi muda huo alikuwa na
saini za
wabunge 66, huku akidai kuwa wabunge wote wa CUF walikuwa
wameandikiwa barua na chama chao kusaini azimio hilo, jambo ambalo litafanya
idadi ya
wabunge kufikia 80.

Zitto ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya kusimamia
Mashirika ya Umma (POAC) alisema kuwa hadi jana majira ya saa 7 mchana, wabunge wa
vyama vyote walikuwa wameweka saini azimio hilo isipokuwa wa UDP.

Mawaziri wanaotakiwa kuwajibika ni Waziri wa Fedha, Mustafa Mkulo; Waziri wa Viwanda na Biashara, Cyril Chami na naibu wake, Lazaro Nyalandu; Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Mkuchika; Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja; na Waziri wa Uchukuzi, Omar Nundu.

Zitto ambaye pia ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA), alisema wabunge wa
CUF 12 wameshasaini azimio hilo na kwamba maagizo yametoka makao makuu ya chama
hicho kutaka
wabunge wake kusaini kusudio hilo.

Alisema kuwa baadhi ya watu wanasema Waziri Mkuu hana makosa na kwamba
anaonewa na kueleza kuwa wanampenda sana, lakini wanaiheshimu zaidi
Tanzania.

Alisema kulingana na kanuni za Bunge, wabunge
wanaweza kumwajibisha Waziri Mkuu kwa kumpigia kura ya kutokuwa na imani
naye.

“Miongoni mwa majukumu ya Waziri Mkuu ni kusimamia shughuli za serikali
pamoja na utendaji wa baraza la mawaziri. Mawaziri wameonekana kusimamia wizara
zao ambazo zina wizi na ubadhirifu.

“Kuwepo kwa ubadhirifu ni kushindwa kwa Waziri Mkuu kutekeleza majukumu
yake…tunajua hawezi kuwawajibisha mawaziri na ndiyo moja ya mambo tunayotakiwa
kuyarekebisha kwenye Katiba, lakini yeye tuko naye hapa na sisi ndiyo
tuliomthibitisha na tuna uwezo wa kuondoa uthibitisho wake.

“Kwa hiyo katika hilo hatuna mbadala hatuna muafaka kama mawaziri waliotajwa
kuhusika na aina ya ubadhirifu kwenye wizara zao, idara zao, mashirika hayo na
halmashauri kama hawajachukua hatua tunaanzia na Waziri Mkuu. Atakuwa Waziri
Mkuu wa kwanza nchini kupigiwa kura au kutolewa hoja ya kutokuwa na imani
naye.

“Tumempa muda mpaka Jumatatu tutawasilisha rasmi hoja yetu kwa
Spika kwa mujibu wa mamlaka ya kanuni 133 inayotutaka kukusanya
saini ya wabunge asilimia 20 ya wabunge
wote ambao kwa hesabu zetu ni wabunge 70 na tutapata zaidi hao,”
alisema.

Alisema kwamba wanatimiza matakwa hayo ya kikanuni na
kisha kuwasilisha kwa Spika, ili baadaye Bunge liweze kuonyesha meno
yake.

Alibainisha kuwa ili Waziri Mkuu aweze kutoka katika kitanzi hicho, anapaswa
kumshauri Rais Jakaya Kikwete awafukuze kazi mawaziri hao ama mawaziri hao
wajiondoe mapema.

“Lakini kama wanataka kumuweka kiongozi wao, kiraja wao rehani, wanataka
Waziri Mkuu aingie katika hoja ya kupigiwa kura ya kutokuwa na imani naye ni
jukumu lao, wachague wao wenyewe,” alisema.

Hata hivyo, Spika kwa upande wake alisema kwa mujibu wa kanuni za
Bunge ambazo zimetokana na Katiba zinataka hoja kama hiyo iwasilishwe bungeni
angalau siku 14 kabla ya siku iliyokusudiwa, na sio wiki ijayo kama ilivyoelezwa
juzi na Zitto Kabwe bungeni.

“Sasa hii habari ya kusema waheshimiwa njooni njooni kusaini huo sio
utaratibu. Hiyo haikubaliki kwa sababu mimi sijapata hiyo hoja mpaka sasa. Bunge
hili tunaahirisha Aprili 23 maanake Jumatatu. Leo (jana), kesho (leo), Jumapili,
Jumatatu haikidhi siku 14 sana sana anaweza (Zitto) kukusanya nyaraka labda
kuwasilisha Bunge lijalo,” alisema Spika.

Aliendelea kusema kuwa kanuni na utaratibu alioutangaza
Zitto hauwezekani na kwamba zoezi la kukusanya saini za wabunge ni
batili. Aliwashauri wanaotaka hoja hiyo wavute subira hadi Bunge lijalo, akidai
kuwa kuitimiza ndani ya siku tatu zilizobaki ni kukosa mashiko.

Hata hivyo alikiri kuwa wabunge wana madaraka na Waziri
Mkuu kulingana na Katiba kwa kuwa ndiyo wanaomwidhinisha baada ya
uteuzi.

Alinukuu ibara ya 53(a) (3) kwamba Waziri Mkuu anapitishwa na wabunge
ambao wanamthibitisha. “Msingi wa Zitto ni kwamba huyu ni mtu
tuliyempitisha sisi wenyewe. Kwa hiyo tuna mamlaka naye kwani ndiye tulimpitisha
sisi,” alisema.

“Waziri ndiye atakayekuwa mkuu wa shughuli za serikali bungeni. Serikali
chini ya mamlaka ya Rais ndiyo itakayofanya maamuzi juu ya sera. Na mawaziri
chini ya uongozi wa Waziri Mkuu watawajibika kwa pamoja katika utekelezaji wa
shughuli za serikali. Hivi vifungu ndivyo vinatupa nguvu ya kuwa na uwezo na
Waziri MKuu.”

Wabunge wa CCM
watishwa


Katika hatua nyingine, imedaiwa kuwa wabunge wa Chama cha Mapinduzi,
wameitwa na kutishwa kuchukuliwa hatua ikiwa watasaini azimio hilo.

Mmoja wa wabunge wa CCM aliyekiri kuitwa ni
Deo Filikunjombe (Ludewa) ambaye alisema alilazimika kusaini kabla ya kuitikia
wito huo.

Filikunjombe, alikiri kuitwa na Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na
Bunge), William Lukuvi, na kumtaka kutosaini azimio hilo, lakini akamwambia
alikwishasaini na alifanya hivyo kwa niaba ya wananchi wa Ludewa ambao
wamechukizwa na ubadhirifu mkubwa uliofanywa na watendaji hao wa serikali.

Kuhusu wabunge wa CCM kutosaini
azimo hilo, Filikunjombe alisema kanuni haikusema wabunge
wote, kwani inafahamika wengine wanarudi nyuma alisema.

Mbunge wa Mtera Livingstone Lusinde alisema suala la hoja ya kikanuni ina
lengo la kuchelewesha mchakato wa kuwaondoa wanaolalamikiwa na kuahidi kuwaondoa
hata kama Bunge litawakingia kifua.

Alisema kama mawaziri wanaolalamikiwa wataendelea kubakia katika nafasi
zao ni bora
wabunge wa CCM wakaondoka na kuwaachia wao majukumu yote.

Alipoulizwa kama msimamo wake hauwezi kuwakera viongozi wake na kuamua
kumchukulia hatua ikiwa ni pamoja na kumuondoa katika chama, Lusinde alisema
kuwa hilo halihofii kwa kuwa hana hati miliki ya ubunge wa Mtera na zaidi
ataendelea kubakia Mtanzania anayepigania maslahi ya nchi yake.

Mbunge wa Simanjiro, Christopher ole Sendeka (CCM), alisema katika
mapendekezo yaliyoafikiwa juzi hakuna azimio katika kamati yoyote lililotaka
waziri aondolewe na kusema kuwa alichokuwa akikifanya Zitto ni usanii.

“Katika taarifa yake ile alipaswa asema Bunge limependekeza mtu fulani
awajibishwe, hivyo alitakiwa kuleta nyongeza katika taarifa yake. Hakuna
aliyeleta. Ile ni burudani tu,” alisema na kuongeza kuwa hoja hiyo haina
mashiko.

Alihoji kuwa iwapo Pinda alishindwa kumuondoa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara
ya Nishati na Madini, David Jairo, atawezaje kumuondoa Waziri wa Fedha, Mustafa
Mkulo.

Alisema kuwa ili hoja hiyo ifanikiwe ni lazima Spika aridhike kwamba
ilifuata taratibu na ina sifa hata ikisainiwa na wabunge 200 kama haina sifa haiwezi
kupita.

Zitto asema wembe ni uleule

Akizungumzia vikwazo hivyo, Zitto alisema haviwatishi na wanaendelea na
mchakato huo, na kwamba watakabidhi hoja hiyo, Jumatatu baada ya kukamilika.

Zitto alisema kama watashindwa kusaini fomu hizo watakuwa wawakilishi wa
ajabu kwa kuwa wao ndiyo waliokuwa wakipiga kelele juzi kutaka waliosababisha
ubadhirifu kuwajibika na kwamba kama watashindwa kuunga mkono litakuwa ni jukumu
la wananchi kupima uwakilishi wao.

Alisema ni jambo la aibu kwa Bunge zima likimaliza kikao bila kuwawajibisha
mawaziri waliohujumu mali za taifa.

“Tukiondoka hapa bila kuwawajibisha watu, wananchi huko nje
watalidharau Bunge kwa hiyo tunalinda heshima ya Bunge na kulinda heshima
ya wabunge
kwa kutaka kuona tunaimarisha uwajibikaji.

“Bila watu kuwajibika madudu haya yatarudia na ndiyo maana tunataka
uwajibikaji ufanyike,” alisema.

Alisema kuwa anajua wabunge wa CCM wamechukizwa na wizi
na ubadhirifu na wamesema kwa nguvu sana juzi na jana na hakuna asiyeona
hilo.

“Mimi sijafanya kama mbunge wa CHADEMA, bali kama mbunge wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania,” alisema.

Hivyo, alitaka wabunge wasigawanywe katika misingi
ya vyama na kwamba anayefanya hivyo hana maslahi na nchi na kuhoji iwapo CCM ina
hoja nzuri ambayo inaisimamia.

“Tusiruhusu maneno ya propaganda ya kutugawa na ninyi ndiyo mashahidi
mnalalamika na juzi mlimuuliza CAG,” alisema.

Alisema katika masuala ya kitaifa wabunge wanapaswa kuweka pembeni
itikadi zao na kuwatumikia wananchi wanaowawakilisha na kusisitiza kuwa
wanachokitaka ni mabadiliko na si mapinduzi.

Wasomi waunga mkono

BAADHI ya wananchi wa kada na rika mbalimbali nchini wamesema mwenendo
wa Bunge la sasa ni ishara za kuamka kwa mhimili huo inayotokana na changamoto
za wabunge
wa upinzani.

Wakizungumza na Tanzania Daima kwa nyakati tofauti wananchi hao
walisema msimamo wa wenyeviti ambao ni wabunge kutoka upinzani wanaoongoza
kamati tatu za Bunge umesaidia kuonyesha uozo wa watendaji serikalini hususan
mawaziri wasiotimiza vema wajibu wao.

Wenyeviti wa kamati hizo ni Zitto Kabwe (CHADEMA) Hesabu za Mashirika ya Umma
(POAC), Agustine Mrema (TLP) Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) na John Cheyo
(UDP) Hesabu za Serikali (PAC).

Kwa mujibu wa Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
(UDSM) Profesa Issa Shivji, Katiba ya sasa inaruhusu kupiga kura ya kutokua na
imani japo ni mapema kufanya hivyo huku akisisitiza kwamba jambo la msingi ni
kusubiri uamuzi wa wabunge hao.

Kwa upande wake mhadhiri mwandamizi mstaafu wa UDSM Dk. Azaveli
Lwaitama alisema wabunge hao wanagombana na mfumo wa
kumweka Waziri Mkuu madarakani hali inayoonyesha wazi kwamba hawana imani na
Rais.

“Ninavyoona hapo kinachowachukiza wabunge hao ni uwaziri mkuu na
mfumo wa kumpata waziri mkuu kwa sababu wanalalamikia utendaji wa baadhi ya
mawaziri lakini waziri mkuu hana uwezo wa kuwafukuza mawaziri hao.

“…Hebu tukumbuke wakati wa Jairo, Waziri Mkuu alitamani kumfukuza akashindwa
lakini Katibu Mkuu Kiongozi alikuwa na uwezo; ndiyo maana alimpa likizo yenye
malipo.

“Tatizo ni mfumo wa utawala walioteuliwa wanawajibika kwa aliyewateua lakini
waliochaguliwa wanatumwa na wananchi ndiyo,” alisema Dk. Lwaitama na kuongeza
kwamba lazima mambo hayo yaingie kwenye Katiba mpya.

Mjasiriamali Celina Ezekiel wa Isimani Iringa alisema Bunge limeanza
kutambua mamlaka yake ya kuisimamia serikali hasa kwa wabunge wa
CCM.

Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) Profesa Sifuni
Mchome alisema wabunge wana uhuru wa kufanya hivyo
kwa maslahi ya nchi na kuongeza kwamba ni jambo la kawaida.

Mkazi wa Igunga mkoani Tabora Nicholous Ngassa alisema haafikiani na suala la
kumwondoa Waziri Mkuu madarakani badala yake mawaziri walioguswa na ripoti ya
CAG wanapaswa kuwajibika na kupelekwa mahakamani.

“Hali ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu na serikali yake kunashusha thamani
Chama cha Mapinduzi (CCM) katika jamii na kujiondoa kwenye ramani ya siasa
nchini na Afrika,” alisema Ngassa.

Naye Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Idara ya
Sayansi ya Siasa na Utawala Dk. Benson Bana alisema wabunge
wametimiza wajibu wao na kuwataka mawaziri wanaotuhumiwa kuchukua
hatua.

Akitolea mfano wa ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali
(CAG) Dk. Bana ambaye ni mwenyekiti mwenza ya Taasisi ya Utafiti wa Elimu ya
Demokrasia Tanzania (Redet) alisema umaskini unaongezeka kwa sababu ya wachache
walio kwenye ngazi za uamuzi.

“Ripoti ya CAG inaonyesha kushuka kwa kiwango cha uwajibikaji
serikalini hususan eneo la matumizi ya fedha za walipa kodi… kwa nini wanaotajwa
kwenye ripoti hiyo wasijiuzulu?” alisema Dk. Bana na kutaka wabunge
washikamane katika hilo.

Naye Mahadhiri wa Chuo Kikuu cha Kiislam cha Morogoro (MUM) Profesa
Juma Mikidadi alisema wabunge wako sahihi katika uamuzi
wa kutaka kumjadili Waziri Mkuu kwa sababu ya mawaziri wa chini yake kushindwa
kuwajibika.

Sheikh Jabir Ramadhan aliwashauri wabunge hao kutoa muda wa mwisho
kwa mawaziri hao ili kabla hawajaondoka waanze kuchunguzwa huku akiwashauri
wasifanye hivyo kwa chuki.

Mkazi wa Tabata Jamila Athuman alisema serikali ya awamu ya nne imeongeza
pengo kati ya matajiri wachache na maskini wengi hali inayowafanya wananchi
kuichukia serikali yao.

“Walioteuliwa hawana uchungu wa nchi ndio maana wanafanya ufisadi huku Rais
akiwakingia kifua kwa kuendelea kuwaacha madarakani na wakati mwingine
anawahamisha vituo vya kazi,” alisema Jamila.

Joseph Mhimbilila alisema wananchi wamechoka kuvumilia wizi wa mali ya
umma unaofanywa na watawala wao sasa wananchi wamechoka hivyo wabunge
hao wakishindwa kuwasaidia watachukua hatua kali zaidi.

“Hili linaweza kuwa fundisho kwa viongozi wenye ndoto za kuliibia taifa
hili,” alisema.

Kwa Upande wake Mwanasheria Alex Mgongolwa alisema sheria inampa mamlaka
Waziri Mkuu kusimamia shughuli zote za serikali na kuhakikisha kunakuwepo na
uwajibikaji.

Alisema katika Katiba ibara ya 53 (A 1-6) inasema hoja ya kutokuwa na imani
na Waziri Mkuu inaweza kuwasilishwa bungeni kukiwa na sababu za msingi juu ya
majukumu ya Waziri Mkuu na kushindwa kuyatekeleza.

“Nafuu inayoweza kupatikana ni kama anayetolewa hoja hajapitisha miezi sita
tokea kuteuliwa kwake au kabla ya miezi tisa kupita tokea hoja kama hiyo
kuwasilishwa bungeni, na hapa ni lazima Spika ajiridhishe kuwa masharti
yamezingatiwa,” alisema Mgongolwa.
 
Ccm kwishaaaaaaaaaaa,,,,Kwiiiiiiiiiiii Kwiiiiiiiiiiii Kwiiiiiiiiiiii Kwiiiiiiiiiiii Kwiiiiiiiiiiii Kwiiiiiiiiiiii Kwiiiiiiiiiiii Kwiiiiiiiiiiii....
 
Pongezi kwa waheshimiwa wabunge aliotia saini zao. Wanatuwakilisha vema. Zito endelea tunakuombea kwa Mola bwana akulinde na akujaze ushuja wa kukemea maovu.
 
Uwe unasoma kwanza post za wenzako kabla ya kupost ya kwako. Yaani wewe jioni hii ndo unakurupuka na hii habari ilihali wenzako waliipost tangu saa kumi na mbili asubuhi?
 
wengine hawajaiona hiyo ya sa 12...ndiomaana nimeweka mida hii...kwa hiyo isishangae...
Uwe unasoma kwanza post za wenzako kabla ya kupost ya kwako. Yaani wewe jioni hii ndo unakurupuka na hii habari ilihali wenzako waliipost tangu saa kumi na mbili asubuhi?
 
wengine hawajaiona hiyo ya sa 12...ndiomaana nimeweka mida hii...kwa hiyo isishangae...
Ok, basi inapendeza! Sasa tuletee ushahidi wa kwamba kweli wamejiuzulu, maana hatujaona kwenye chombo chochote cha habari kinachothibitisha hilo.
 
StarTv wametangaza katika taarifa yao ya habari ya saa 11 kuwa mawaziri wafuatao wamejiuzuru...nao ni Mkulo wa noti, Chami wa viwanda, Nundu wa uchukuzi, Maghembe wa kilimo, Maige wa maliasili, mponda wa afya, mkuchika wa Tamisemi na ngeleja wa umeme...
 
Bado hawajajiuzulu.
Waziri mkuu ameahidi kutoa maamuzi ya ama mawaziri kujiuzulu ama yeye mwenyewe kujiuzulu, ama CAG kutuhumiwa either kwa kutoa ripoti feki siku ya J3.

Waziri mkuu ameonyesha dhahiri hajakereka na ufisadi uliofanywa na mkulo
 
Back
Top Bottom