Mtaani kwetu Manzese kuna tatizo kubwa la rushwa
Yawezekana wengine mkaliona dogo lakini kwa watu wa chini ni maumivu makubwa iko hivi.
Kila mwezi kwenye baadhi ya serikali za mitaa ya kata ya Manzese anakuja mgambo ajiitaye afisa mazingira, na kazi yake kwa kushirikiana wstendaji wa mitaa kukusanya fedha za uchafuzi wa mazingira na hawatoi risiti.
Wakikuta alama za maji mlangoni kwako wanakupela ofisi za serikali ya mitaa na kwa kitisho Cha kulipishwa elfu hamsini wana kulazimisha "kuwapooza" kwa elfu ishirini hadi arubaini bila risiti
Mhusika mkuu ni mlevi maarufu Sandton bar
Sasa simu ya Takukuru 113 haifanyikazi , simu zao hazipokelewi na hata e mail yao haifanyi kazi
Msaada kwa anaye jua mawasiliano yao na tufanyaje kwani hii Ni tozo la Kila mwezi na hata asie husika hubambikiwa