Mawakili wa serikali kazeni uzi angalau Lema atoke mwezi wa pili

Good People

JF-Expert Member
Aug 6, 2016
945
1,817
Nitasimamia Ukweli Daima na Mawakili wa Serikali wamekua wanajitahidi sana katika kufanya kazi zao na mimi nawaambia wakaze Uzi ili angalau Lema atoke mapema mwakani mwezi wa Pili kwani atakua kajifunza kufuatia tabia yake chafu ya kumkejeli na kumtukana mheshimiwa Rais.

Ili iwe funzo kwa wote wasioheshimu mamlaka kwa kujivunia eti Mawakili wasomi kama akina Kibatala kuwa watawatoa na kudharau Mawakili wa Jamuhuri.
 
Nilifikiri unataka wajitahidi asitoke kabisa!
Sasa kumbe mnataka achelewe kutoka, Aliwaambia huko ndani anateseka?
 
Kama kukaa kwa Lema ndani kunakuongezea unga debe kwako then endelea kumuombea Mabaya .
Kama ni siasa tu unafanya then bado una practice siasa za Miaka hiyoooo,Miaka ambayo mtu wa chama kingine alikuwa anaonekana mhaini na msaliti na anatakiwa kupotezwa.
We are in new era mkuu wake up siasa za kukomoana au kulipiza kisasi ilishapitwa na wakati,we are in modern political era,siasa za kiuchumi,siasa za maendeleo sio elimination ,hoja kwa hoja ,sio hoja kwa propaganda mkuu.
 
We jamaa unachekesha kweli.... Teaching old dog new trick? Kwa taarifa yako akitoka tu anatupia jingine...huyu ndio alipaswa aitwe 'Sugu' sasa
 
Si vyema kumuombea mwenzio mabaya usiw na sadism character.Lema ni Mtanzania mwenzetu .ila tuombe tu mahakama imalize kesi yake kama anahatia au la na kama anahatia hana budi kutumikia adhabu
 
Sasa hapa sijaelewa,me nadhani hongelea ukweli na haki ya kisheria usiwe mshabiki mambo ya vyama weka pembeni jadili ukweli wa jambo hiki ndo kinachotusumbua watanzania tunashindwa kutumia uelewa wetu na elimu tulizo nazo tunabaki kushabikia kitu bila kuhoji na kujua hualisia kwa jambo lilivyo.Mungu azidi kufungua akili zetu tuweze kujadili vitu kwa hekima na Busara.
 
Daaah, wewe jamaa una ROHO MBAYA sana, hongera sana mkuu.
 
Naunga mkono hoja japo chamoto ameshakipta siyo utani naona hata makalio yamekuwa flat kama ya wahindi.
 
Apende asipende Atarudi Mavumbini tu......kama wote tutakavyo Rudi ni Maamuzi ya Muumba kuamuwa nani aanze na lini....
 
Mheshimiwa kwako wewe. Ikiwezekana mwambie abadili katiba ili at awale milele.
 
Unaongea kwa kuwa unafahamu kuna mhimili uliochimbiwa chini zaidi. Huu mhimili ndio unaburuza mihimili mingine ambayo inaonekana kuwa shallow...
 
Usimlinganishe Mandela na vitu vya kijinga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…