Mawakili wa Lissu wamfungulia kesi Kamishna Magereza, Mkuu wa Gereza la Ukonga

Mawakili wa Lissu wamfungulia kesi Kamishna Magereza, Mkuu wa Gereza la Ukonga

Parabolic

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2013
Posts
2,743
Reaction score
2,599
HEVkxjnaUAA5CBo.jpg
Sisi mawakili Maduhu William,, Nashon Nkungu na Paul Kisabo tumefungua shauri la Kikatiba ambalo ni Shauri No. 7300dhidi ya Kamishina Jenerali wa Magereza, Mkuu wa Gereza la Ukonga na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Shauri hili limefunguliwa katika mahakama kuu masijala kuu ya Dodoma.
Tumefungua shauri hili kuhoji uhalali wa Jeshi la Magereza kuzuia na kuwawekea,,,vingiziti au vikwazo mawakili pale wanapotembelea Magereza kwa ajili ya mashauriano ya kisheria na wateja wao ambao ama ni wafungwa au Mahabusu.

Soma Pia:

Shauri hili litatajwa kwa mara ya kwanza tarehe 14 Aprili 2026 mbele ya jopo la Majaji watatu ambao ni Mruma,, Dr. Rumisha na Dr. Longopa, JJJ's.Tutaipigania Heshima na hadhi ya uwakili usiku na mchana na bila kuchoka. Wakili Maduhu
 
Je, mamlaka ya magereza yanaweza kuweka vikwazo kwa mawakili wanapokutana na wateja wao?
🤔🤔🤔
 
Hii nchi imeoza kila mahali, Ngoja tuone itakuaje na hii kesi
 
Nikuwapelekea moto tu makatili yote huku Israel anaruka nao mmoja baada ya mwengine hadi watubu
 
Hii imekuja kwa kuchelewa sana. Hii ilibidi ifanyike kitambo sana. Ilitakiwa pawe na kesi nyingi dhidhi ya hawa jamaa, kwa lengo tuu la kuwafanya waogope kupindisha taratibu.
Hongereni Mawakili, japo mmestuka kumekucha.
 
Shaur litatupiliwa MBALI hilo hii nchi Sheria hazifanyi kazi tena

Lengo sio kuwashinda, lengo kuwakumbusha wajibu wao wa msingi kufuata taratibu na kuwafanya waone aibu na ufala wao ambao dunia yote imeuona. Sio kila kesi inafunguliwa ili umshinde mtu.
 
Kesi kama hii ni ile ya
Mchmchum marwa vs musson prisoner officers
Deportation ordinance act
 
Sisi mawakili Maduhu William,, Nashon Nkungu na Paul Kisabo tumefungua shauri la Kikatiba ambalo ni Shauri No. 7300dhidi ya Kamishina Jenerali wa Magereza, Mkuu wa Gereza la Ukonga na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Shauri hili limefunguliwa katika mahakama kuu masijala kuu ya Dodoma.
Tumefungua shauri hili kuhoji uhalali wa Jeshi la Magereza kuzuia na kuwawekea,,,vingiziti au vikwazo mawakili pale wanapotembelea Magereza kwa ajili ya mashauriano ya kisheria na wateja wao ambao ama ni wafungwa au Mahabusu.

Soma Pia:

Shauri hili litatajwa kwa mara ya kwanza tarehe 14 Aprili 2026 mbele ya jopo la Majaji watatu ambao ni Mruma,, Dr. Rumisha na Dr. Longopa, JJJ's.Tutaipigania Heshima na hadhi ya uwakili usiku na mchana na bila kuchoka. Wakili Maduhu
Huyo 4th Respondent, ameunganishwa hapa kwa makosa au vipi?
 
Dawa ya wapumbavu wanaoshindwa kusimamia matakwa ya kisheria ya kazi zao, na badala yake wanafanya kazi zao kwa kuwafurahisha wanasiasa vilaza, ndiyo hii sasa.
 
Back
Top Bottom