Mawakala wa Mungu

fimboyaasali

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2011
Posts
8,606
Reaction score
8,270
Wanandoa nyie ni mawakala wa Mungu,zaeni watoto,muwalee vizuri ili nao waje kuzaa na kuanzisha familia zao.Iki mtimize wajibu huo,acheni migogoro midogo midogo mara,mje kafanya hivi,mara mume kafanya vile,hiyo ni akili ndogo.Maisha yenu ni yenu nyie 2 tu,hakuna haja ya kushirikisha wengine.Pangeni kwa pamoja maisha yenu,mkubaliane kwenye kila kipengele cha maisha,kazi,biashara,nyumba,unyumba,watoto,chakula,matibabu,misaada kwa familia,usulihishi wa migogoro,misaada kwa ndugu,sala kwa kutegemea dini zenu,ngono na starehe
 
mkuu tupe uzoefu wako kwanza
ili ndoa idumu ni lazima kila mtu afuate wajibu wake kwa kutaka au kutotaka. Yaani unalazimika au unalazimishwa kufanya majukumu yanayokupasa. ukileta ujinga unaadhibiwa
Nani anakulazimisha?
ndoa lazima wakubwa wako wahusishwe iwe wazazi au walezi
ndoa ni kitu cha ukoo. ili ukifanya ujinga ,ukoo au familia wakuwajibishe
tunakosea kwa kudhani ndoa ni kitu personal cha wanandoa. ambapo sasa mkihitilafiana hakuna wa kuingilia na inakuwa end of the story
Screening lazima ifanyike vya kutosha kupata mwenzi. wewe binafsi huwezi fanya screening
 
actually sio mawakala tu,

bali pia ni wasaidizi wa wa karibu sana na Mungu na ni wa kipekee sana kwa Mungu...

Tazama,
wamepewa upendo na upendeleo wa ajabu sana. Ndio pekee wenye kibali cha Mungu katika kazi ya uumbaji.

Na kwahiyo wana ndoa hushirikiana na Mungu katika kazi ya uumbaji...

Ndio maana maandiko yanasema, waacheni watoto wadogo waje kwangu...
hii ni kutokana na kukengeuka kwa baadhi ya wanandoa dhidi ya matunda ya ndoa. watoto wanaokataliwa kwa wazazi wao, au ni yatima kwa sababu mbalimbali...
Mungu anawaita kwake , kwasabb alishiriki na wazazi wao katika kazi ya uumbaji...

Ama kweli ndoa ni mpango Mtakatifu tangu mwanzo πŸ’

Hongera sana na Mungu awabariki sana Wanandoa wote πŸ’
 
Tunakumbushana tu, ndoa sio rahisi, unatakiwa ukiwa kwa ndoa uwe na hekima ya Mungu, ukitumia hekima ya kibinadamu pekee utamuona shetani live...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…