Maumivu yatokanayo na mpira wa kutolea mkojo

mamkuu5

JF-Expert Member
Nov 24, 2014
1,139
716
Habari waungwana,binamu yangu alifanyiwa operation,akawekewe mpira wa mkojo(Catheter)toka wamtoe mpira ule anamaumivu makali kama ya mtu mwenye U.T.I inakaribia siku ya tatu sasa.

Naomba kujua tufanyeje yaishe?,Je ni kawaida au anahitaji matibabu mengine?
 
Habari waungwana,binamu yangu alifanyiwa operation,akawekewe mpira wa mkojo(catheter)toka wamtoe mpira ule anamaumivu makali kama ya mtu mwenye U.T.I inakaribia siku ya tatu sasa,naomba kujua tufanyeje yaishe?,Je nikawaida au anaitaji matibabu mengine?
Inabidi afanyiwe upasuaji nenda hospitali kubwa watakupa majibu
 
Habari waungwana,binamu yangu alifanyiwa operation,akawekewe mpira wa mkojo(Catheter)toka wamtoe mpira ule anamaumivu makali kama ya mtu mwenye U.T.I inakaribia siku ya tatu sasa.

Naomba kujua tufanyeje yaishe?,Je ni kawaida au anahitaji matibabu mengine?

hayo ni maumivu tu ya kawaida,with time yataisha.
 
siku tatu!!,
itapita hata miezi miwili kabla hali haijarudi sawa,kudidimiziwa huo mpira kwenye njia y mkojo si mchezo
 
Inabidi afanyiwe upasuaji nenda hospitali kubwa watakupa majibu
Duuuh we jamaa sijui doc wa wapi????m nilipataga iyo kinachotokea ni Ile sindano wanayokuchoma wakati wa kuweka mpira usiwe unachomoka ndio huleta shida baadae wakati wakutoa ikiwa kama yale maji maji hayakuvutwa vizuri, mi nilirudi hospital wakanicheak wakasema yale maji yametengeneza kidonda maana nilikua natokwa na damu kabisa wakati wa haja ndogo nilipewa dawa ya kukausha baada ya week nilikua poa.......mwambie arudi hospital
 
Ushawahi kuchomekewa? Alikuchomekea muuguzi wa jinsia yako

Habari,
Kwa maelezo yako mambo matano yanawezakuwa ni sababu:

1: Kama size ya mpira/catheter ilikuwa ni kubwa ukilinganisha na size ya njia ya mkojo, inawezakuwa ilikujeruhi.

2: Kama wakati wa ballooning/ kutanua sehemu ya mpira ili usichomoke ilifanyika kabla ya kuingia kwenye kibofu/kile kisehemu kinachovimba, inaweza kukujeruhi na kuleta maumivu.

3: Kama wakati wa kuweka hakukutumika kilainishi, pia nafasi ya kukujeruhi ni kubwa na kuleta maumivu.

4: Kama sterility/usafi unaozingatia kutowapa bacteria nafasi ya kuwa sehemu ya tukio zima haukuzingatiwa, kinaeezakuwa ni chanzo cha maambukizi.

5: Kama kipindi cha kukaa na mpira kilizingatiwa kulingana na hali ya mgonjwa au hakikuzingatiwa.

Kama haya yote yakizingatiwa zoezi hili huwa salama na lisilo na maumivu.
Hiyo, ni vyema kwa hali iliyojitokeza kufika hospitali na kuangaliwa kwa karibu zaidi ili kujua tatizo la msingi ni lipi.
 
Back
Top Bottom