Maumivu ya tumbo na kujaa gesi baada ya kunywa maziwa

kind2

Senior Member
Mar 6, 2016
102
45
Kama heading inavyojieleza. Napenda kufahamu sababu zinazopelekea kila nikinywa maziwa freshi. Nasumbuliwa sana na kuumwa tumbo au tumbo kujaa gesi.
 
Tuko wengi mkuu,mimi ndio siyanywi kabisa maana nikinywa napata mateso ya ajabu yaani tumbo linajaa utafikiri nimejaza gas kwa pump.
 
Tusubiri Madokta waje mi naona hii inanifanya nisiwaze kabisa kunywa maziwa ya aina yeyote maana nikinywa tu ni shida inaanza hadi nashindwa kufanya kazi kwa ufanisi. Na haiishi mpaka nianze kuendesha kama mara tatu nne
 
Kapime choo. Huenda una minyoo au amoebiasis (amoeba)...
Hakuna cha Amoeba wala cha nini nimeuliza mpaka baadhi ya madaktari bingwa hawana majibu ya maana kulisema hili tatizo.Ni tumbo tu linakataa baadhi ya vyakula,kwa mfano mimi nikila nyama nyekundu N'ombe ,Mbuzi,Kondoo ninaumwa tumbo mpaka kuna wakati ilitokea nikapoteza fahamu kwa maumivu lakini nikila Nguruwe,Kuku,samaki na hata utumbo wa Ng'ombe sipati tatizo la namna yoyote,nimelifuatilia hili swala mpaka kwa madaktari bingwa laikini hawana majibu ya maana ya kunisaidia,nilisoma hii mada kwenye gazeti la Uwazi miaka ya 2000 nikakutana na hii mada nilipoamua kuachana nazo ndio ikawa salama yangu.
 
Nimewahi kusikia kwamba kuna watu miili yao inashindwa kumeng'enya sukari ya asili ya kwenye maziwa hivyo huleta kama mzio/yaani mwili huhisi ni kitu kigeni. Wengine wanadai asidi nyingi ya tumboni inachachisha maziwa na kuzalisha gesi tumboni
 
kaka hilo nahisi un vidonda vya tumbo, hata mimi nina matatzo hayo, kapime vidonda vya tumbo
 
Mkuu nimeshapima vidonda vya tumbo zaidi ya mara mbili sehemu tofauti sina,nimetumia dawa nyingi nikihisi nina vidonda vya tumbo ikiwemo dawa za Rahabu lakini hola,nimetumia mpaka mchanganyiko wa dawa za hospitali ambao unatibu vidonda vya tumbo(antibiotics for h.pylori) nazo zimedunda.Kwahiyo ninaishi kwa kuepuka hivyo vyakula ndio salama yangu.
 
Kama heading inavyojieleza. Napenda kufahamu sababu zinazopelekea kila nikinywa maziwa freshi. Nasumbuliwa sana na kuumwa tumbo au tumbo kujaa gesi.
PIA mwenyewe ninatatizo Hilo la maziwa kidogo. ILA tatizo kubwa nikila karanga mbichi Na za kukaangwa. PIA nimepima vidonda vya tumbo, minyoo sina. Kwenye kujua tujikwamue vipi maana unaweza usile vizuri hadi wiki moja ukila karanga.
 
Kama heading inavyojieleza. Napenda kufahamu sababu zinazopelekea kila nikinywa maziwa freshi. Nasumbuliwa sana na kuumwa tumbo au tumbo kujaa gesi.
Unaupungufu wa Enzyme Aitwaye Lactase... Au Defiency iitwayo lactose Intolerance

Hii inasumbua sana Jamii ya Africa Na Asia.. maana Hatuna Tamaduni ya unywaji wa maziwa Mara kwa Mara has tukivuka Umri wa utoto ... So production ya Lactase hupungua Mwilini
 
You have lactose intolerance.Hauna vimeng'enyo vya kuvunja vunja maziwa baada ya kunywa.Epuka maziwa fresh.Unaweza kunywa mtindi badala yake.
 
Tatizo litakuwa upo allergy na maziwa kwani hata wife wangu nae yupo hivyo hivyo pia. Akila kitu chochote chenye maziwa tumbo humjaa na kuanza kusokotwa na kuleta maumivu tumboni. Alibahatika kwenda hospital USA akaambiwa yupo allergy na maziwa kwahio hata yogurt na ice cream hawezi kula. alijaribu maziwa ya Lactaid baadhi ya siku huwa poa lakini baadhi ya siku humpelekesha.
 
Hata mimi inawezekana nina hiyo shida,vipi kwa upande wa nyama nyekundu nayo shida inaweza kuwa ni nini maana mimi nikila tatizo linakuwa kama lile ninalopata nikinywa maziwa.
 
Kuhusu nyama nyekundu sijui ila mimi pia nilikuwa napenda sana kuila mpaka kuna siku nilisoma kwenye mtandao mmoja ukasema kama nyama iliokuwa haijawiva (nyama nyekundu) bacteria wake hawajafa vizuri kwahio wanaweza kukuletea madhara tumboni.
 
Lactose intolerance. Hata watoto wachanga wapo wa aina hiyo. Mme wangu yupo hivyo. Pole.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom