Maumivu ya tumbo chini ya kitovu kwa mama mjamzito: Fahamu visababishi, ushauri na tiba

Pole sana kwa maumivu unayoyapata, nahisi huu ni ujauzito wako wa kwanza! Haya maumivu unayo yapata yanasababishwa na mvutano unaotokea ndani ya tumbo na misuli ya kizazi, lakini pia mlalo na activities za mtoto awapotumboni hii pia hutokea.

Kina mama wenye retroverted uterus pia hupata maumivu kama haya. Ni vizuri ukaanza mazoezi sasa badala ya hiyo bedrest uliyopewa. Unapolala tumia zaidi ubavu wa upande wa shoto hii pia husaidia. Otherwise nakutakia kila la kheri na Mungu akujalie mtoto kwa usalama.
 
Pole sana, maumivu unategemea Kama ni wakati wote, am ukipata mkojo unauma na Mara kwa Mara, uterus ni pelvic organ na mimba inapokuwa then uterus grows to become abdominal organ, mie nimepata msaada pale Mawenzi hospitali nenda wodi number 5 pale siku za kazi utawakuta Madokta watakusaidia.


Heshma yenu doctoz na members wote, mimi ni mjamzito wa meizi 4 na siku 12, tatizo langu ni kuumwa tumbo mara kwa mara anzia kwenye kitovu kuelekea chini, nimeshaeleza tatizo langu KCMC wakaniambia nipunzike nisifanye kazi yyt lakini bado tatizo halijaisha, wakati mwingine nahisi km nimebanywa na haja kubwa nikienda chooni haitoki na maumivu yanaendelea,WAPENDWA WANGU NISAIDIENI JAMANI MANA NAOGOPA SANA. MUNGU AWABARIKI.
 
halafu na kutoka nje ya ndoa inasababisha. inabidi mtulie nyote. wewe na mmeo pia. nakutakia afya njema.
 
Nasumbuliwa na maumivu ya tumbo chini ya kitovu na maumivu ya nyonga sana adi napata shida kutembea mimi ni mjamzito wa miez 5 na nusu,tatiźo nini?na nifanye nini kuzuia tatizo hili? MSAADA PLEASE!
 
Habari yako Henya,
Una tatizo linaloitwa PPGP(Pregnancy-related pelvic grindle pain) ambalo husababisha maumivu kwenye maeneo ya fupa la mbele au nyuma(pelvic bone).
Dalili za tatizo hili ni:

  • pain over the pubic bone at the front in the centre
  • pain across one or both sides of your lower back
    [*=left]pain in the area between your vagina and anus (perineum)

Maumivu haya huongezeka pia ukiwa una tembea,unapanda ngazi,ukisimama kwa mguu mmoja au ukigeuka kitandani.

Hali hii husababishwa na kuonegezeka kwa uzito wa tumbo(ujauzito) au kama ulikuwa na historia maumivu ya mgongo na nyonga kabla,ajali au kuanguka na kufanya kazi nzito.

Hali hii utaiepuka vipi:
- Kufanya mazoezi ya kwenye maji au mazoezi kwaajili ya hio pelivic bone
- Kukandandwa
- Epuka kufanya kazi nzito na kubeba vitu vizito,kusimama muda mrefu,kutembea muda mrefu
- Pumzika vyakutosha
- Ukigeuka kitandani jaribu kugeuka na magoti pamoja,unaweza pia kujaribu kuweka mto kati kati ya miguu
- Usivae viatu virefu

Haya mazoezi yatakusaidia kupunguza maumivu
  • Get on your hands and knees with your back straight. A mat can help cushion your knees.
  • Try to pull your abdominal muscles in. Tuck in your buttocks. This will tilt your pelvis up. As your pelvis tilts, your back will rise toward the ceiling.
  • Hold and count to 5, then relax.
Leg Lifts

This strengthens the muscles of your back, buttocks, and abdomen.

  • Get down on your hands and knees. Put your arms directly under your shoulders. Keep your knees shoulder-width apart.
  • Round your back. Then lift your left knee and gently bring it toward your elbow. Look at your knee as you raise it. (Stop moving your knee if you feel pressure in your abdomen.)
  • Keeping your knee slightly bent, extend your leg. Lift your leg until you feel a stretch in your low back. Dont lift your leg higher than your hip.
  • Hold for 5 counts, then lower your left leg. Repeat the exercise with your right leg.
Au jaribu mazoezi haya:

Lala kawaida,kunja magoti (60 degrees),miguu ikiwa sakafuni,then jaribu kujiinua sehemu ya kiuno/mgongo,unaweza kujaribu mazoezi haya mara 8-10 kwa siku
  • pelvic rocking.jpg
 
Thanx mimi49 kwa maelezo na ushauri wako.Nami nina swali kuhusu hayo maumivu..Nina dada yangu ana ujauzito wa miezi 2 na anayapata haya maumivu hadi anashindwa kunyanyua mguu,je yanaweza kusababisha madhara yoyote kwenye ukuaji wa mimba? (Miscarriage)
 
Maumivu ya tumbo wakati wa miezi mitatu ya kwanza ya mimba ni mojawapo ya matatizo yanayolalamikiwa na kina mama wengi. Kuna matatizo mengi ambayo yanahusiana tu na mimba, hata hivyo, ni muhimu kukumbuka kwamba hali yoyote ambayo husababisha maumivu katika mgonjwa asiyekuwa na ujauzito inaweza pia kutokea kwa mama mjamzito, ingawaje historia na uchunguzi vinaweza kuwa tofauti.

Kwa asili kutathmini maumivu ya tumbo kwa mama mjamzito ina changamoto kwa sababu kichefuchefu, kutapika, na maumivu ya tumbo hujitokeza mara nyingi kwa wajawazito wengi . Mfuko wa uzazi unapotanuka unaweza kusukuma viungo vingine kando ndani ya tumbo, upungufu wa damu na leukocytosis ni kawaida katika mimba ya kawaida na si viashiriwa vya upungufu wa damu au maradhi. Mgonjwa ambaye mimba imetunga nje ya mfuko kipimo cha ultrasound kinaonyesha majimaji na uchafu ndani ya mfuko wa uzazi bila ushahidi wa mimba.

Kiinitete kinapojipandikiza katika kuta za ndani za mfuko wa uzazi inaweza kusababisha maumivu ya tumbo , ambayo huchukua muda wa siku 1- 2 na kiasi kidogo cha damu ukeni. Mara nyingi kiasi hiki ni kidogo na hutokea kati ya siku 6 -12 baada ya tarehe inayohisiwa mimba kutungwa , mara nyingi kipindi hiki hukaribiana na siku ambayo mwanamke alikuwa anatarajiwa kuingia hedhi. Hivyo, wagonjwa mara nyingi hufanya makosa kwa kufikiri kuwa wameingia katika siku zao kama kawaida.

Mimba iliyotunga nje ya mfuko ni tatizo linaloongoza kusababisha maumivu kwa kina mama wengi sehemu mbalimbali duniani. Tatizo hili linaweza kubainika kwa kutumia Ultrasounda na kipimo cha homoni HCG. Hata hivyo tatizo hili linatibiwa kama dharura kwa mama kufanyiwa upasuaji.

Sababu nyingine ni kutoka kwa mimba. Mimba inaweza kutoka yenyewe au kutolewa kwa makusudi. Tatizo hili huambatana na maumivu pamoja na kuvuja damu. Utoaji wa mimba usiokuwa salama unaongoza kusababisha vifo vya kina mama katika nchi zinazoendelea.

Uvimbe kwenye mirija ya mayai (Ovarian cyst). Wakati mwingine uvimbe huu hupasuka au kujizungusha. Hata hivyo unaweza kupungua na usipopungua unaweza kuondolewa kwa njia ya upasuaji hasa wakati wa muhula wa pili wa ujauzito.

Sababu nyingine ni kujizungusha kwa mirija ya mayai (Ovarian torsion). Hii hujitokeza mara chache.
Uvimbe kwenye mfuko wa uzazi pia husababisha maumivu hasa unapokuwa mkubwa. Tatizo hili linaweza kusababisha ujauzito kutoka hasa katika miezi ya awali.

Kidole tumbo (appendicitis) hujitokeza kwa uwiano sawa kama wanawake ambao hawana ujauzito. Matibabu ya ugonjwa huu ni upasauji. Mara nyingi wanawake wengi hupata uchungu baada ya upasuaji.

Kutokana na mabadiliko ya homoni wanawake wengi hupata tatizo la mawe kwenye mfuko wa nyongo. Tatizo hii huweza kugunduliwa kwa njia ya ultrasound.Matibabu hutegemea na dalili

Uvimbe(inflammation) kwenye mfuko wa nyongo ni tatizo la ghafla linalosababisha maumivu makali ambalo pia hujitokeza wakati wa mimba. Tatizo hili mara nyingi husababishwa na mawe kweny mfuko wa nyongo. Antibiotics hutumika katika matibabau ya uchongo huu.

Wanawake wengi wakati wa hujauzito hupata maambukizi kwenye njia ya mkonjo mara kwa mara. Hii ni kutokana na mabadiliko yanayojitokeza wakati huu wa mimba.

Sababu nyingine ya maumivu husababishwa na ROUND LIGAMENT. Ligament hii ndio inayoshikilia mfuko wa uzazi tumbo. Mfuko wa uzazi unavyozidi kukua, ligament hii huvutika na kusababaisha maumivu.
Dawa za maumivu husaidia kwa tatizo hili.

Ultrasound hutumika katika uchunguzi wa maumivu ya tumbo wakati wa ujauzito. Kongosho, mfuko wa nyongo na kidole tumbo vyote huonekana kwa mama mjamzito. Vipimo vinavyotumia
mionzi viyumike tu pale inapohitajika kwa mama mjamzito.

abdominal-pain-during-pregnancy.jpg
dfs.png
maumivu ya tumbo.jpg
 
Dah, asante sana Mzizimkavu, maana jana nilikuwa naingia siku ya kuminambili tangu nitoke danger days, nikashangaa ghafla tumbo linaniuma ingawa si sana, hasa nikiinama, harafu nikashangaa damu nyepesi, zenye rangi kama ya kahawa hivi, inayoelekea kwenye weusi zinatoka Zinatulia, zinatoka zinatulia.

Ila swali langu ni hili mzizi mkavu inakuwaje mpaka kufika mda huu sioni dalili ya maziwa kuvimba,nawakati huwa nasikia yakuwa maziwa huwa yanavimbaga nyakati za mwanzo? Na je nikienda kununua kile kipimo ntaiona? Au kina mda wake?
 
Asante Mzizimkavu kwa elimu nzuri.

Naomba kuuliza, mimi ni mjamzito niko mwishoni mwa second tremister. hii ni mimba yangu ya 3, na zote mbili nimezaa kwa oparesheni. sasa ninasikia maumivu ya tumbo chini kidogo ya kitovu upande wa kulia na kushoto.

Nikikaa kwa muda mrefu nikisimama nasikia kitu kinanichoma na nasikia maumivu makali sana mpk nashindwa kutambea, nainama huku nashikilia tumbo,pia wkt mwingine nikipiga chafya inanitokea. na maumivu haya mara nyingi yanatokea upande mmoja. pia nikitembea sana.

Nimepiga ultrasound hamna kitu, ila dr. kanipa dawa za kutuliza maumivu. naomba unisaidie tatizo nini? naogopa sbb nategemea kufanyiwa tena opareheni ya tatu, sasa naogopa hata kutembea sana.
 
Na swali lingine nikwamba, mbona mpaka sasa sijaanza kuchagua vyakula,wala kuchukia harufu fulani fulani, ila nimeanza kujisikia kizunguzungu tu, na hiyo hali niliyokuuliza hapo juu,,,na huwa naingia period tarehe 14 na ninaenda kwa siku nne.
 
Kuumwa tumbo wakati wa mimba changa hutokea, japo hata kama ni kawaida ni vizuri kujiridhisha kwa Daktari.
 
Titia,
Pole sana laiti ningelikuwepo huko nyumbani ningekufanyia dawa ya kienyeji ungeweza kuzaa pasipo na kufanyiwa Operesheni laikini nipo mbali na huko nyumbani hilo ndilo tatizo. Na kuhusu kusikia kitu kukuchoma kama kwenye

(ultrasound) hujakiona hicho kitu kinaambatana na mambo ya kienyeji siwezi kukwambia sana nisije kukutisha fanya hivi jaribu kila unaposikia maumivu ramba kijiko kimoja cha Asali maumivu yako yatatulia inshallah. Ukiwa na Matatizo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom