Maumivu ya tumbo chini ya kitovu kwa mama mjamzito: Fahamu visababishi, ushauri na tiba

Habari Mkuu mzizi mkavu,

Mimi ni mjamzito wa miezi tisa hadi kufikia jumamosi kesho kutwa . Je, dalili zipi zitanifanya nijue kuwa mtoto kashageza kichwa kueleke kwenye njia?

Na kuna ya kufanya mtoto ageuke. Sitaki kuzaa kwa kisu.Pia tumbo linatutumka mno. Na ananipiga Sana maeneo ya mbavu upande wa Julia na juu kuja kwenye matiti.

Pia kwenye nyonga ya kushoto huwa nahisi movement kwa mbali. Ila ninakojoa kila muda. Nisaidie mkuu na Kuna njia ya kufanya nijifungue kwa njia ya kawaida nijulishe.

Natanguliza shukran
 
Habari humu ndani,

Wife anapata maumivu makali sehem za nyonga hasa upande wa kulia, hasa usiku wakat anapotak kulala. Ni mjamzito miez 7.

Baada ya kumpeleka zahanat Ucku alipew amoxilin 2x3, phenobabitone 1x2, na diclofenac, alvotumia Ucku zilimpa nafuu japo nkawaza sana kuhusu dawa hzo, nkawa na hofu Sana ckumpa tena. Tatzo limejirudia Ucku uliofuata. Vp aendelee kunyw hz dawa?

Hofu dawa c nzuri saaana kwa mjamzito hasa diclofenac
 
Usimpe kwani hata mimi mke wangu halikuwa hivyo nakuila tukienda hospital tunapewa dawa kama hizo sio nzuri kwa Mama Mjamzito.
 
Dr Habari, je maumivu huwa ni kawaida during first trimister au? Mathalani kwenye wiki ya sita na saba?
 
Msaada wanabodi,
Mke wangu ana maumivu makali chini
ya kitovu,kiasi cha kwamba inampelekea tabu kutembea. Ujauzito ni wa miezi 6,juzi tulienda clinic ila wakasema itakuwa uchovu tu wa kazi.

Maumiaumivu yake anasema tumbo kama linavuta. Huu ni ujauzito wake wa pili,wa kwanza alijifungua kwa operation.
Natanguliza shukrani.
 
Jaman naombeni ushauri mke wangu anaujauzito wa miez kama miwili ivi but siku tatu zilizopita amekua akipa maumivu ya tumbo ya kuuma na kuachia kwenda chini leo nmetoka kazin nmeambiwa ilo tatizo. ndugu zanguni naombeni ushauri kipi kitakua kinasumbua nakua na hofu sana na pia ni ujauzito wake wa kwanza
 
Dr Habari, je maumivu huwa ni kawaida during first trimister au? Mathalani kwenye wiki ya sita na saba?
Hii first trimester inasumbua sana hasa kwa sisi ambao ndo uzazi wa Kwanza. Wiki ya tisa sasa lkn natapika na maumivu ya tumbo. Kila harufu kwangu ni mbaya.

Nimepewa dawa Folic acid with ferrous lkn zimenishinda nakuwa hoi
 
Jamani naomba wataalam mnisaidie:

Mke wangu anamimba ya mwezi mmoja hivi lakini occassionaly huwa analalamika kwamba anasikia maumivu kwenye eneo la chini ya kitovu chake lakini pia huwa anatapika sana baada ya kupata maumivu hayo! Je hii hali inasababishwa na nini kitaalam? Au itakuwa unique kwa yeye tu?
Ina umri gani sasa hivi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari wana JF,

Mke wangu yupo kwenye mwezi wa pili wa ujauzito wake lakini mara kadhaa amekuwa akilalamika maumivu ya tumbo chini ya kitovu. Hali hii inamkuta muda mwingi usiku, nashindwa kujua nifanyeje. Msaada tafadhali.

Asanteni! 🙏🏾
 
Wakuu nina mjamzito,tumbo linamuuma maeneo ya kitovuni, hutokea mara chache, na pia hutoa maji yenye rangi nyeusi mara chache ukeni, alienda Hospitary akapimwa na kuonekana ana UTI nyingi, ametumia dawa na tatizo kupotea kwa muda na kurudi tena. Hili ni tatizo gani?

NB: amefanya utra sound Dk amemwambia mtoto yupo salama aendelee kutumia dawa tu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom