Maumivu makali ukeni

CTX

JF-Expert Member
Jan 3, 2015
1,273
984
habari zenu wadau/wakuu....

Ni hivi nina dada yangu ambaye anasumbuliwa na maumivu makali sehemu yake ya uzazi.
Kwa mujibu wa maelezo yake,anasema anapata maumivu makali sana kama ya jipu hasa kwenye mlango wa kizazi ambao anasema unakua unapwita kama jipu. Hadi maeneo ya kiunoni na mapajani huwa anasema anahisi maumivu.amejaribu kwenda hospitali akaandikiwa sindano lakini hazikusaidia.walimchukua vipimo vya ultra sound lakini ilionyesha hamna tatizo lolote.
mwanzoni tulizani ni mchango akatumia dawa za kienyeji lakini hakuna mafanikio.
hivi ninavyoongea yupo kwenye dozi ya tatu ya sindano ambazo aliandikiwa hospitalini za siku 5 lakini hakuna maendeleo mazuri.
Sasa wadau bado tunaendelea kufikiria ni shida tatizo gani hili huku tukijipanga kwenda kwa maspecialist wa masuala ya wanawake sababu hata hospitalini wameshauri hivyo.
Nimeona ni vyema nikalileta huku ili tushee wote kwa anayefahamu ni shida gani na matibabu yake tuweze kusaidiana. Kwani matatizo yapo kwetu sisi binadamu hivyo kusaidiana ni sehemu ya maisha.

MAELEZO YA ZIADA: dada yangu yupo kwenye ndoa na ana watoto 3 wadogo.wawili wamefatana kiumri mmoja wa kike ana miaka 8 mwingine 7 wa kiume.wa mwisho ana miaka 2 sasa.

tiririkeni wadau....
 
peleka hospital mkuu hapa huwezi pata majibu sahihi nendeni mkampime kwenye vipimo vikubwa ili mjue tatzo ni nini
 
  • Thanks
Reactions: CTX
akajaribu kucheki kansa ya shingo ya kizazi... nahisi kwa maelezo yako anahitaji uanagalizi wa kitabibu zaidi kuliko hiyo mitishamba!!
 
Back
Top Bottom