Mauaji yanayoendelea nchini Burundi

Eastern DRC zaidi ya watu milioni 2 wamekufa..
Sanasana wazungu wanajadili namna ya kuwaokoa sokwe wa Eastern DRC...
hawana shida binaadamu akifa

Hahahahaa The Boss hii ni dhihaka kubwa sana. Kweli ulimwengu wa leo wanyama wanathamani kuliko binadamu..... daah Mungu na atusaidie.
 

Ok asante, japo kama una hizo taarifa haidhuru ukiziweka hapa kwa faida si yangu tuu hata wengine ambao tuko na uelewa mdogo wa mambo ya siasa.
 
Dada kasie, japo wanasema dawa ya moto ni moto, lakini vita ya wenyewe kwa wenyewe haijawahi kuzimwa na vita. Angalia Libya Obama anajuta kuingilia kivita.
Dawa ya kudumu ya vita kama hii ni mazungumzo..ona rwanda wametulia.
 
Ni nani anatakiwa kufukunyua hiyo mizizi ya vita na kumaliza mauaji?

Siasa kwakweli mie huwa siielewi kabisa yaani kuna muda unaona mambo hayaendi sababu utaambiwa political reason..... khaaaa.
Warundi hawawezi kufukunyua hiyo mizizi, inawazidi kimo.

Mgogoro wa Burundi ni mentality ya ukabila iliyojikita zaidi ya miaka 200 kweye minds za watu, sio kitu cha kuvunja siku moja wala kwa miaka 10. Na tatizo kubwa la Burundi ni either wewe ni Mhutu au wewe ni Mtusi sasa hapo ni pagumu sana.

Huku kwetu kulikuwa na matatizo kama hayo, Nyerere akasoma mchezo akaja na stategy ya kutokuyapa makabila makubwa uongozi mkuu wa nchi na tukaishi kwa strategy hiyo kwa miaka 50 mpaka tukakomaa.

Leo tuko huru, mentality ya ukabila hata kama ipo lakini haina mizizi sana, hata hayo makabila makubwa yakipewa madaraka kwa sasa ni vigumu mno kurudi kwenye ukabila.

Burundi hii haiwezekani, nchi yenye makabila makubwa mawili hasimu ambayo ni almost 99% ya total population hayawezi kuchangamana kirahisi hata kwa miaka 50 kama hakuna juhudi za makusudi za kuyachanganya
 
Jambo la kujiuliza ni chanzo cha mauaji ni nini? jibu rahisi kabisa ni tamaa ya madaraka. Ukishagundua tatizo kabla ya kuwalaumu wengine unajiangalia ww je uko protected? unagundua hapana kuna case kama hiyo visiwani, sema wananchi either wameamua kuipotezea au wanavutia kasi. Kwa hiyo una conclude kwamba muda wowote tatizo linaweza kutokea hata hapa, so ni kuomba Mungu tu.
 
Nawapenda na ninawaonea huruma watu hawa,, wanakufa kwa 7bu ya mtu m1 anayeng'ang'ania nchi kwa interest zake mwenyewe,,
 
Halafu eti rais wao kaokoka. Hata hanijii kichwani mtu anaina watu wanachinjana halafu anakaa kimya. Wokovu gani huo. Uwongo mtupu
 
Leo hii busara umeipata wapi, nikajua umelalia msalibokoo..!
 
Trump alishatoa msimamo wa namna atakavyofanya kuleta amani kwenye nchi za namna hii duniani. Ni kutawalia chini ya mandate ya UN. Tumwombee urais wa dunia anaogombea.
 
Mkuu asigwa, at least unafahamu baadhi ya mambo kwa usahihi wake. Ukiangalia baadhi ya comment za wachangiaji wengi, wanachangia ama kwa mihemko au kwa hearsays! Jamani, hebu jaribuni kuchimbua tawala za Congo, Rwanda na Burundi muone tatizo ni nini. Nkurunziza sio tatizo hata kidogo, tatizo la Rwanda na Burundi ni ukabila tu. Kuna kabila moja halitaki kabila lingine litoe kiongozi wa nchi. Wanataka wao tu ndio wawe viongozi na hata wakiwa viongozi huishia kuua au kuwaua kabila lingine.
 

Kungekuwepo gesi au visima vya mafuta burundi, ungeona mataifa makubwa yanavyojifanya yanajua kuamua kesi
 
Ni kweli mkuu.

Juhudi kubwa zinatakiwa kuelekezwa katika kupunguza huu uhasama baina ya makabila haya hasimu, kama ingewezekana programu ingeanza kwa vijana ambao wengi hawapendi mambo ya kihafidhina, wanapenda kwenda na wakati.

Ingewezekana kutengeneza kizazi kipya cha warundi kilicho na mchanganyiko wa damu hizi mbili wangefanikiwa sana.

Hakuna mtu anayeweza kumuua mjomba wake kisa si wa kabila lake, au shangazi kwa sababu ni mtusi au muhutu.
 
Mkuu Nyerere aliwabeba sana Watutsi (kwa sababu anazozijua yeye mwenyewe) hadi wakati ule wa Arusha peace negotiation alipowageuka. Nyerere hakutaka kuonekana mpuuzi mbele ya jamii ya kimataifa kwa kuwakumbatia Watutsi kwenye ujinga wao. Aliona kwamba alishawabeba kwa muda mrefu sasa iliwapasa wabadilike waukubali ukweli kwamba hawatatawala milele Burundi. Watutsi walipoona Nyerere amewageuka walimtukana eti ni k'kojoz!
Tangu uhuru Nyerere aliwabeba sana Watutsi.
Mwaka 1965 aliuawa waziri mkuu wa Burundi Pierre Ngendandumwe, Nyerere aka mute!
Mwaka 1972 mauaji ya kimbari yakafanyika dhidi ya Wahutu (wahutu laki 3 wengi wao wasomi waliuawa), UN ikataka kupeleka jeshi Burundi Nyerere akasema Warundi wasiingiliwe masuala yao ya ndani ya nchi.
Mwaka 1994 walipouawa maraisi Ntaryamira na Habyalimana kwa kutunguliwa ndege yao, kuna Watutsi kule Mwanza walifanya sherehe kushangilia. RPC alipowatia ndani Nyerere akamtaka awaweke huru akasema 'adui yako akifa huwezi kufurahi'?
Upo mkono wa Nyerere uliojificha nyuma ya nguvu za kiutawala za Watutsi kuanzia Uganda, Rwanda, Burundi na DRC.
 
Mkuu unaijua historia ya Mwl. Nyerere vizuri ? Unajua historia ya wazazi wa Mwl. Nyerere ? Walitoka wapi ( i mean their origin) ? Kama huijui nitakuambieni siku moja then mtaconnect dots ni kwa nini alizipenda sana na kuzitetea mno tawala za kitusi na ni kwa nini alimuunga mkono yoweri museveni kuivamia Uganda.
 
Halafu eti rais wao kaokoka. Hata hanijii kichwani mtu anaina watu wanachinjana halafu anakaa kimya. Wokovu gani huo. Uwongo mtupu

Hivi una uhakika kwamba nkuruzinza anafurahia hali hiyo na hakuna hatua zozote kukomesha machafuko au ni jazba yako tu?
 

Andrew Nyerere
 
Ukabila, Udini, ni kitu kibaya sana.

Siku zote huwa nazungumzia hili suala
 
Sisi ni wanyama mzee hatuna tofauti yoyote na mafisi au mbwa,so sheria zisipo fuatwa na kusimamiwa definitely tunaludi kwenye unyama wetu ufisi na u mbwa we are animals
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…