mauaji ya wanaodaiwa kuwa wachawi yalaaniwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

mauaji ya wanaodaiwa kuwa wachawi yalaaniwa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mgoyangi, Feb 23, 2011.

 1. Mgoyangi

  Mgoyangi Senior Member

  #1
  Feb 23, 2011
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 184
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35

  Naona jamii hawa wamejitokeza kulaani mauaji ya wanasongea.
  -------------------------------------------
  TAARIFA KWENDA VYOMBO VYA HABARI
  Hii ni taarifa kwenye vyombo vya habari kulaani mauji ya wazee wawili wa kike Magreth Makunga (76)na Raphaela Komba(76) yalitokea tarehe 19/02/2011 mchana za saa saba na kuzikwa tarehe 21/02/2011 taarifa za mauji hayo ziliyotolewa jana tarehe 22/02/2011 na Television ya taifa TBC 1 kwamba wazee hao wawili toka kijiji cha Magagula kata ya Magagula wilaya ya songea vijijini waliuwawa kwa kuchomwa moto kwa imani za kishirikina na watu wenye hasira kari baaada ya mkazi mmoja wa kijijini hapo kufariki baada ya kuwa mgonjwa wa muda mrefu.

  Wazee hao wa kike waliuwawa kwa kuchomwa na moto na mazishi yao yakasusiwa na wakazi wa eneo hilo isipokuwa ndugu wa karibu, wanaharakati wa maswala ya haki za wazee mkoani Ruvuma na wandishi wa habari.Sisi NABROHO taasisi inayojishughulisha na maswala ya haki za wazee hapa Tanzania tunaungana kabisa na wanaharakati wengine kukilaani kitendo hicho cha kikatili waliofanyiwa wakinamama hao wazee na wananchi wa eneo hilo kwa imani zilizopitwa na wakati tunaamini kwamba vyombo vya usalama vitafanya kila liwezekanalo kuwatia nguvuni wote waliofanya tendo hilo na kuwafikisha mahakani mara moja ili kuepusha mauaji yanamna hiyo yasitokee tena na huu ni ushahidi mwingine unaoonyesha ukiuakaji wa haki za wazee haki za wazee hapa nchini unaofanywa na watu wachache kwa masilahi yao binafsi, pengine tukio hilo litakuwa chachu kwa vyombo vetu vya usalama na serikali za vijiji kuwa na mipango madhubuti ya kulinda maisha na uhai wa wazee wote kama kundi maalumu.

  Ni masikitiko yetu makubwa kwamba tukio hili limekuja huku serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania na taasisi zingine zinazo shughurikia maswala ya haki za binadamu wakiwa katika harakati za kukomesha na kutokomeza kabisa mauji ya wazee kwa imani za kishirikina hapa Tanzania ,sambamba na hilo tunalani pia kitendo cha kiongozi wa dini aliyekataa kuendesha misa ya mazishi ya wazee hao licha ya kwamba walikuwa waumini wa dhehebu lake kwa kisingizio eti musiba ulikuwa umegubikwa na harufu za imani za kishirikina,yeye kama kiongozi wa dini hakupaswa kujichanganya katika hisia hizo ambazo zinapingana na misingi ya dini,tulitegemea kiongozi wa dini kama yeye alipaswa awe msitari wa mbele kukemea maovu hayo na kuwatia moyo ndugu na jamaa waliowapoteza wapendwa bibi zao.tunakilani kitendo hicho kwa kuwa kiliwanyima marehemu wazee hao haki yao ya kidini ya kusaliwa kabla ya mazishi kwa imani za dini yao.

  Tunapenda pia kumupongeza mwandishi wa habari wa kituo cha TBC 1 Ruvuma aliyetoa taarifa ya tukio hilo na wanaharakati wote toka mashirika ya PAD na WLAC mkoani Ruvuma walioshiriki kikamirifu katika mazishi ya wazee hao licha ya kwamba wakazi wengine wahakujitokeza kwa wingi katika mazishi hayo,tunawaomba watu wote wanaopenda amani Tanzania wajitokeze kuraani kitendo hicho na kisijitokeze kamwe.
  NABROHO SOCIETY FOR THE AGED ni taasisi inayojishughurisaha na maswala ya haki za wazee hapa Tanzania ikiwa na Makao yake makuu mkoani Mwanza wilaya ya Magu,PO.BOX 299,MAGU
  Taarifa hii imeandaliwa leo Tarehe 23/02/2011 na kuletwa kwenu
  na kupitia barua Pepe

  KUBINI NKONDO KUBINI
  ,0754937107,0782090980
  Meneja Miradi ya haki za wazee Nabroho Society For The Aged
  Leo Tarehe 23/02/2011

  HAKI ZA BINADAMU NI HAKI ZA WAZEE PIA
   
Loading...