Mauaji ya Nyamongo: CCM wawaunga mkono CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mauaji ya Nyamongo: CCM wawaunga mkono CHADEMA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by sweke34, Jun 5, 2011.

 1. s

  sweke34 JF-Expert Member

  #1
  Jun 5, 2011
  Joined: Sep 28, 2010
  Messages: 2,533
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Wenyeviti wa vijiji vitatu vilivyopo Kata ya Nyamongo, wilayani Tarime wametua jijini Dar es Salaam na kueleza wanaunga mkono viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kutetea haki za wananchi wa eneo hilo.
  Wakizungumza katika kikao cha pamoja na wananchi wa Nyamongo wanaoishi jijini Dar es Salaam juzi, Wenyeviti hao Elisha Marwa wa kijiji cha Nyangoto (CCM), Tanzania Omtima wa Kewenja (Chadema) na Otembe Nyamhanga (CCM), walisema kudai haki hakuna itikadi ya vyama, hivyo wanaungana na Chadema katika kusimamia katika kufungua kesi dhidi ya Jeshi la polisi kwa kufanya mauaji ya watu wanne.
  Hivi karibuni watu wanne walikufa kwa kupigwa risasi na Polisi kwa kile kinachodaiwa kuvamia Mgodi wa North Mara Gold Mining unaomilikiwa na Kampuni ya African Barick Gold kwa nia ya kutaka kuiba mchanga wenye dhahabu.
  Katika Kikao hicho kilichowakutanisha na wanachama wa Wananchi wa Nyamongo wanaoishi jijini hapo (Nyada), Mwenyekiti wa kikao hicho Elisha Marwa, alisema kimsingi chanzo cha mauaji ya watu hayo hayakutokana na uchochezi wa kisiasa bali ni kutokana na wananchi kuchoshwa na hali ngumu ya maisha.
  Marwa alisema chimbuko la mgogoro ni wamiliki wa Mgodi kukiuka mkataba waliowekeana baina yao na vijiji hivyo, ambapo ulielezea mgodi huo utawajibika kurudisha asilimia moja ya mapato kwa kupitia mfuko wa dhamana kwa kila kijiji kwa ajili ya maendeleo.
  Alisema mkataba huo pia uliweka wazi kwamba mgodi pia ungewajibika kusaidia wachimbaji wadogowadogo kwa kuwatengea eneo pamoja na kuwasaidia nyezo bora za uchimbaji.
  Hata hivyo, mgodi huo baada ya kuanza kazi hawakutekeleza mkataba huo na badala yake wananchi wa vijiji vitano vinavyozunguka mgodi huo, Kewanja, Nyamwaga, Kerende, Ngekuru na Nyagoto wamezidi kuwa na hali ngumu baada ya kuzuiwa kufanya shughuli mbalimbali ikiwemo biashara na uchimbaji mdogomdogo.
  Marwa alisema wao kama viongozi wa vijiji walijaribu kufuatilia utekelezaji wa mradi lakini walikatishwa tamaa baada ya kutakiwa kuchukua dola za Marekani 100,000 kwa masharti ya kufutwa kwa mkataba wa awali.
  Mwenyekiti wa Kewanja, Tanzania Ontima, alisema vurugu zilizotokea baada ya mauaji hayo, zilisababishwa na Mkuu wa Wilaya ya Tarime, John Henjewele kukataa kuwasikiliza na kuwafukuza ofisini kwake walipoenda kumtaarifu juu ya mauaji hayo.
  Alisema kimsingi kama Tarime inatakia kuwa tulivu lazima Rais afikirie upya juu ya Mkuu huyo wa Wilaya akieleza anafanya kazi kwa ubabe bila kuwasikiliza wananchi.
  Naye Otembe Nyamhanga (CCM), alisema kuja kwao kuonana na wananchi hao ni kutafuta namna ya kusaidia familia zilizoathirika kwa kufiwa na ndugu zao pamoja na kudai haki za Wananyamongo.
  CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
   
 2. kidi kudi

  kidi kudi JF-Expert Member

  #2
  Jun 5, 2011
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 628
  Likes Received: 157
  Trophy Points: 60
  kweli hata hayo makubaliano yapo sawa? yaani katika faida yoooote wanayopata hao Barrick katika madini hayo walikubaliana watoe asilimia 1 Tu!!!??!! Nashindwa kushangaa sijui kama kweli uwekezaji wa namna hii unalinufaisha taifa au kufukarisha wananchi! kama kweli idea ya serikali ya ubinafsishaji ilikua ndio hiyo ya kuwageuza wananchi wake watumwa ndani ya nchi yao, basi ni bora tukawekwa wazi kuwa hatuna wawekezaji bali wakoloni!!! imefikia hatua sasa tufanye maamuzi magumu ambayo Baba wa Taifa aliweza kuyafanya; kuna haja gani ya kuharakisha kuwaleta wawekezaji (WAKOLONI) ilhali hawana faida yoyote kwa maslahi ya nchi yetu.

  SASA NIMEJUA WAZALENDO NCHI HII NI WA KUHESABU NA HAWAPEWI NAFASI YA KUONYESHA UZALENDO WAO KWA VITENDO, BALI WALIOPO KWENYE UONGOZI ASILIMIA KUBWA (kama sio yote)NI WADHALIMU, WASIO NA CHEMBE HATA NUSU YA UZALENDO​
   
 3. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #3
  Jun 5, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,232
  Likes Received: 3,782
  Trophy Points: 280
  Wamesema kilicho moyoni mwao lakini ccm taifa wanayo yakwao na kikwete anayo yake na Rashid Othimani anayo yake na Zoka anayo yake mwisho wasiku wate tutaungana kulikomboa taifa na kuiacha ccm na kikwete wake
   
 4. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #4
  Jun 5, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  Taratibu nawaona wakiupoteza uanachama kwa kosa la kuwa wakweli!
   
 5. M

  Murrah Senior Member

  #5
  Jun 5, 2011
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 191
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tatizo Nyamongo Hakuna ushiriakiano wa dhati miongoni mwa viongozi toka katika vijiji vinavyozunguka mgodi. Wakuunagana kwa dhati wanaweza kushinda makaburu
   
Loading...