Ali Nassor Px
JF-Expert Member
- May 6, 2022
- 2,433
- 4,043
UTANGULIZI
Magonjwa ya afya ya akili ni matatizo ya ubongo ambayo humfanya mtu kuwa na hisia, fikra na matendo tofauti na yale yanayotarajiwa na jamii na kushindwa kukabiliana na changamoto za maisha.
Kwa mujibu wa ripoti za SHIRIKA LA AFYA DUNIANI (WHO). Kati ya watu watano basi moja ana magonjwa ya afya ya akili . na ubaya zaidi magonjwa aya umpata mtu yoyote yule wa rika lolote lile.
Waathirika wa magonjwa aya ni wanawake zaidi ya wanaume. hivyo basi shirika la afya duniani (WHO) Mwaka 2019, mpango maalum wa afya ya akili (2019-2023): chanjo ya afya ya kila siku ya afya ya akili ili kuhakikisha upatikanaji wa ubora na huduma za bei nafuu kwa hali ya afya ya akili katika nchi 12 za kipaumbele kwa watu milioni 100 zaidi.https://www.who.int/
Hata hivyo tatizo la limekuwa kubwa sio kwa nchi za jirani tu bali hata ndani ya Tanzania. matukio mengi yanaonesha . matokea ya magonjwa ya afya ya akili UBAKAJI, KUSHAMBULIA WATU , KUUA / KUJIUA.
Katika andiko hili nitaangazia zaidi matukio yanayosababisha na magonjwa ya akili , Sababu za magonjwa ya akili , Dalili na Tiba.
• MATUKIO YALIYOSABABISHWA NA MAGONJWA YA AFYA YA AKILI KATIKA NCHI YA TANZANIA.
Japo kuwa hakuna takwimu rasmi katika nchi ya Tanzania. lakini wastani wa matukio ya mauaji asa ya mapenzi ulipotiwa katika kila kipindi cha miezi miwili. Jeshi la polisi lilitoa takwimu mwezi Julai 2021 zilionyesha katika kipindi ha miezi miwili tu Mei hadi Juni 2021. Mauaji yalikuwa 275 na kati ya ayo chanzo kilikuwa ni wivu wa kimapenzi.
Lakini pia kituo cha sheria na haki za binadamu (LHRC). ilitoa ripoti yake mwezi Mei pekee kimeripoti matukio 35 ya mauaji ambapo waliouwa wanaume walikuwa ni wanne (4) na wanawake walikuwa ni (31). chanzo kikiwa ni wivu wa kimapenzi.
✓ Tukio la siku ya kuamkia Mei 29, 2022 la kuuwa kwa kupigwa risasi 7 Swalha. kwa kupigwa na mumewe kisha mume mtu pia kujiua lililotokea. huko Mwanza liliteka hisia za wengi nchini Tanzania.
CHANZO CHA PICHA, MILLAD AYO TV.
Ukiachana na matukio ya mauaji . lakini pia matukio ya unyanyapaa yanazidi kushamili nchini Tanzania kila siku. sana sana maeneo ya vijijini na waathirika zaidi ni watoto wadogo na wazee. Baadhi ya mikoa hapo zamani kidogo yalitokea matukio ya mengi ya unyanyapaa yaliyopeleka vifo na hata mengine kuacha kumbukumbu mbaya katika jamii.
✓ Tukio la mtoto Nasra ( MTOTO WA BOX) ; tukio la mtoto nasra maarufu kama mtoto wa box lilitokea mwaka 2014. ambapo mtoto mwenye umri wa miaka mitatu na nusu alikutwa mzima ndani ya box ilisemekana alikuwa akiishi humo ndani ya box pasipo kuoenkana na mtu yoyote na akilishwa pumba kwa mda wote.
PICHA YA NASRA, CHANZO CHA PICHA MTANDAONI .
afya ya mtoto huyo ilikuwa sio ya kuliridhisha sana kwani alikuwa ni mlemavu tokea alipozaliwa . aikuchukua siku nyingi baada ya tukio hilo mtoto nasra alifariki dunia. hii ilionesha na inaonesha wazi matukio ya unyanyapaa bado yapo japo yanafanywa kisiri siri.
hata hivyo matokeo ya matukio ayo yanasababishwa na magonjwa ya afya ya akili.
AINA NA SABABU YA MAGONJWA YA AKILI.
1. Kurithi vinasaba, magonjwa ya mda mrefu
2. Matumizi ya madawa ya kulevya
3. Kufiwa na ndugu au mtu tegemezi katika familia
4. Kukosa elimu
5. Kufanya vibaya katika masomo / kufukuzwa masomoni.
Magonjwa ya afya ya akili pia yapo mengi sana kama vile
1. Depression (Huzuni)
2. Anxiety Disorder (Ugonjwa wa wasiwasi).
3. Schizophrenia
4. Eating Disorder ( Matatizo ya kula).
Na magonjwa mengine mengi tu.
DALILI ZA MAGONJWA YA AKILI.
Japo magonjwa aya yanatofuatia dalili zake. miongoni wa dalili za magonjwa ya akili ni:
1. Wivu uliopitiliza
2. Kuhusu maisha hayana thamani kwako.
3. Kukosa furaha / kuwa na furaha kupita kiasi
4. Hasira za haraka na kufikia hatua ya kudhuru watu / vitu.
5. Kuhisi harufu ambayo wengine hawahiisi.
MATIBABU NA USHAURI .
Hata hivyo magonjwa ya akili yanatibika japo kuwa utofautiana
Cha kwanza, Elimu itolewe kwa jamii kuhusiana na magonjwa ya afya ni kitu muhimu sana katika kuzuia au kujirudia
pili ; Tiba ya kisaikolojia (mtu yoyote kujitambua alipo anapotoka na anapoenda ili kumsaidia kufanya mabadiliko ya maisha yake yeye mwenyewe).
Tatu; Kutotumia dawa za kulevya pamoja na vilevi
Nne; Tuanze kufanya mazoezi na tafiti zetu sisi wenyewe na watu wetu wa karibu (hususani kwenye mahusiano sehemu kubwa inayoaathirika zaidi ni kwenye ndoa sasa tukipima kipimo cha UKIMWI / VVU, BLOOD GROUP AGGLUTINATION tusipuuze na AFYA YA AKILI).