Matumizi yasiyozingatia bajeti zilizopitishwa na bunge ni tatizo kwa maendeleo ya nchi.

Anold

JF-Expert Member
Jul 15, 2010
1,456
615
Nilivyokuwa najua ni kuwa matumizi ya serikali yote lazima yawe kwa mujibu ya bajeti, utaratibu wa sasa wa kutofuata bajeti iliyoidhinishwa na bunge inafanya kusiwe na maana kwa wabunge kukaa na kujadili kitu ambacho hakitazingatiwa. Taasisi nyingi za serikali kwa muda mrefu hazija pewa hela za maendeleoa au fedha za kuendesha Ofisi, ieleweke kuwa pamoja na nia nzuri ya kufanya miradi ya kimaendeleo bila kufuata vipaumbele ambavyo vimekubaliwa na bunge, itafanya kusiwe na maana wabunge kupoteza muda kujadili mambo ambayo hayatafuatwa.

Kwa siku za hivi karibuni viongozi wengi wamekuwa wakiibua miradi papo kwa papo na kuwaahidi wanachi kuwa watajua hizo pesa watazinyofoa wapi. Nchi hii inachangamoto nyingi tena za muda mrefu viongozi waandamizi lazma wajihadhari na mihemko ya kupenda kuwafurahisha wanachi. Ni vizuri vipaumbele vieleweke ili tufanye mambo yenye tija.

Wabunge lazima wasimamie hili kwa nguvu zao zote vinginevyo bunge halitaeleweka. Pamoja na nia nzuri ya kujenga viwanda, ila hilo lisifanye shughuli nyingi za serikali zisimame. Ni matumaini yangu makubwa kuwa wabunge kwa umoja wao watakemea vitendo vyovyote ambavyo vinakiuka matumizi sahihi ya pesa ya serikali, aidha wabunge wahakikishe kuwa bajeti inafuatwa na pesa zinapelekwa kunakohusika ili kupunguza usumbufu kwa watendaji wa serikali.
 
Back
Top Bottom