kindikwili
JF-Expert Member
- Oct 5, 2016
- 1,862
- 2,872
Habari wana bodi!
Kama kichwa cha habari kinavyojieleza, nimefanya uchunguzi mdogo sana hapa jijini (Dsm) nikiwa kwenye daladala, maeneo ya starehe na hata ninapokuwa na marafiki zangu wenye hizi smartphone nimegundua kwamba 80% ya matumizi ya hizi simu ni ya hovyo sana. Nitaeleza kwa uchache kama ifuatavyo.
UMBEA
Hizi simu zimeongeza umbea sana hadi wanaume wamekuwa wambea wakubwa sana baada ya kuja kwa hizi simu. Kwenye magroup mengi watu wanajadili mambo ya hovyo sana, wanakuwa wepesi wa kutuma picha za matukio ambayo kimsingi hayana ulazima. Hapa hakuna cha wanaume wala wanawake wote wamekuwa na umbea wa hali ya juu sana.
PICHA
Mimi sikuwahi kutegemea kama kuna wanaume wanapenda kupiga picha kama ninavyoshuhudia sasa, kwakweli mimi si mpenzi wa picha maana nakumbuka nikiwa primary nilipiga picha moja siku ya kumaliza shule, sekondary nina picha kama 5, advance ziko 2 na chuo kama 3 toka 2013 hadi leo nina picha moja. Hata kama sina interest na picha ila kuna watu wamezidi yaani asione gari, nyumba nzuri, bustani nk atapiga picha tu. Picha zenyewe mara kabinua makalio, mara kavuta mdogo kwenda mbele, mara kavuta uso, mara kama anakonyeza, mara analamba mdomo na vituko vingine kama hivyo. Wakaka nao wameanza kuiga haya mambo ya kijinga yasiyo na tija ambayo kimsingi yanapaswa kufanywa na wadada wasiojielewa.
KUPUNGUA KWA HESHIMA NA UTU
Kwasasa kwenye daladala ni shida tupu, unakuta baba au mama wa miaka 60+ amesimama kwenye gari huku mdada au kaka wa chini ya miaka 30 amekaa kwenye sita macho yote kwenye simu yake anachat na kutabasamu bila shida. Wengine anaingia kwa gari anakukuta umekaa kwenye siti moja anakuja kukaa kiti cha pili hata kusema hi! hakuna. Anafika anakaa kwa siti na kutoa simu kama hajakaa na binadamu kabisa.
KWA WANANDOA
Juzi nimepanda gari ya jamaa yangu akiwa na mkewe yaani toka tunatoka home Tabata hadi Sayansi hakuna aliyeongea na mwenzake. Mimi nikiwa na gazeti langu la mwanchi nasoma huku yule jamaa yangu anaendesha gari mke akawa anachat. Tukifika kwa foleni jamaa naye anatoa simu yake anachat yaani hakuna wa kuongea na mwingine. Hali kama hii nimeiona kwa watu wengi sana wenye magari wakiwa na wake au ndg zao yaani wanakuwa busy sana kuchat.
USHAURI WANGU
Kwanza nakiri kwamba kila mtu ana interest na hobby yake na ana haki kutumia mali zake atakavyo ila tuwe na kiasi jamani. Halafu hizi simu ni mtaji mkubwa sana ukiwa nazo, nadhani waliozileta walijua manufaa ya hizi simu kibiashara zaidi kuliko kazi ya kupiga picha na kushare umbea. Tubadilike kwa wale ambao wanadhani kuwa nazo ni sifa na kwamba kupiga picha za ajabu ajabu ndiyo matumizi sahihi wafikiri upya kwakweli.
SHUKRANI
Nawapongeza wale wote wanaotumia hizi simu kutangaza biashara zao na kuzikuza, kueneza neno la Mungu na matumizi mengine yenye matokeo chanya kwao.