Matumizi ya IT katika kuongeza ufanisi kwenye biashara

Ntwa A. Katule

JF-Expert Member
Jan 4, 2017
239
229
15673038_1820518418188972_3418397614340196137_n.png

Katika setup ya biashara ili kila kitu kiende vizuri lazima kuwe na "efficient business processes". "Business process" ni jinsi vitengo mbali mbali ndani ya kampuni vinavyofanya kazi kwa lengo la kuhakikisha mteja anapata huduma stahiki na nzuri. Mfano wake ni labda kwenye idara ya mauzo kazi yao inakuwa ni kupokea oda za wateja na kisha kuanza kuziandaa. Kwenye idara ya usambazaji labda wao kazi yao ni kuchukua oda ambazo zipo tayari kutoka watu wa mauzo na kuzisambaza kwa wateja. Idara nyingine inayoweza kuwepo ni masoko ambao labda wao kazi yao ni kufikisha ujumbe kuhusu bidhaa zipatinazo kwenye kampuni kwenda kwa wateja. Mifumo ya ugawanaji majukumu kama hivi inawezesha kampuni kutoa huduma kwa urahisi kwa wateja. Business process ambazo zimetengenezwa kuendana na mifumo ya IT zina uwezo mkubwa zaidi katika kuiongezea kampuni ufanisi zaidi ya washindani wao wa kibiashara. Mfano wa matumizi ya IT ni pale unapoweza kuitumia katika kutafuta masoko zaidi au katika kutoa huduma kwa wateja. Badala ya wewe tu kutegemea wateja wanaokuja kwenye sehemu yako ya biashara unaweza pia kuwafikia wateja ambao hawana uwezo wa kufika kwenye sehemu yako ya biashara.

Hivi karibuni watu wengi wameanza kutumia mitandao kama Instagram na Whatsapp kuwafikia wateja wao. Lakini mifumo kama hii kwa jinsi wanavyoitumia kuna mapungufu na wengi hawaitumii kwa ufanisi sana na kuna ushindani mkubwa sana kwa maana kila mtu anakuwa anajaribu kuitumia. Je tofauti yako na watu wengine itakuwa ni nini? Je unajua unaweza ukaitumia hii mitandao kwa ufanisi na kuwa bora zaidi katika ushindani kuwazidi washindani wako? Yote haya yanawezekana iwapo utaamua kuzikarabati business process zako ili kuiwezesha IT ndio iongoze ufanyaji kazi wa business processes zako.

Kwaushauri zaidi wa jinsi gani unaweza kutumia IT kuboresha biashara yako, basi usisite kutembelea page hii Mr ICT Guru Tanzania LTD | Facebook. Like page hii ili uendelee kujifunza ya vitu vinavyoendelea kwenye ulimwengu wa biashara na teknolojia.
 
Back
Top Bottom