Matumizi ya dawa bila kuzingatia ushauri.

Feb 18, 2017
53
56
MATUMIZI YA DAWA BILA USHAURI.

Tabia ya kujinunulia dawa bila ushauri wa daktari, (self medication) kwa mtu asiye mtaalamu wa afya inazidi kuongezeka.
Wapo watu wanajinunulia dawa kwa sababu ya uzoefu wa kipindi kilichopita. Mfano mtu aliumwa tumbo, akapewa dawa aina ya Fragyl. Siku nyingine akiumwa tumbo hatafuti ushauri kwa mtaalam wa afya bali anakwenda kununua 'Fragyl' moja kwa moja na kuanza kutumia, au anaweza kumpatia mtoto/ndugu yake.
Wengi wanafanya hivyo, wasomi na wasio wasomi.
Lakini je! Unajua mtaalamu anatazama vitu gani kabla ya kuandika dawa? Je! Anatazama dalili tu?

Hapana, kuna mambo mengi ya kutazama; Moja ni umri. Zipo dawa hazipaswi kutumiwa na watoto wadogo. Dawa nyingine zina madhara makubwa kwa watoto. Baadhi hazipaswi kutumiwa kwa watoto chini ya miaka 14, nyingine chini ya miaka 12, nyingine chini ya miaka 5, nyingine chini ya mwaka mmoja na nyingine chini ya mwezi mmoja.
Je! Watu wasio na taaluma ya afya wanazingatia hayo pale wanapoamua wenyewe kutumia au kuwapa watoto dawa bila ushauri wa kitaalamu?

Pili, ujauzito. Zipo dawa hazipaswi kutumiwa na wanawake wajawazito. Dawa zingine hazipaswi kutumiwa wakati wote wa ujauzito, nyingine hazipaswi kutumiwa kwa ujauzito chini ya miezi mitatu na zingine hazifai kwa ujauzito wa zaidi ya miezi mitatu. Inaweza kuwa kwa faida ya mama na/au mtoto. Je! Mtu anapoamua kutumia dawa au kumpatia mtu mwingine dawa bila ushauri wa mtaalam, anazingatia hilo.

Tatu, maradhi mengine. Zipo dawa zinazotibu maradhi fulani lakini hazipaswi kutumiwa kwa watu wenye maradhi mengine. Zipo dawa zinazotibu maradhi kama ya mgandamizo wa damu (Presha/Hypertension) lakini hazipaswi kutumiwa kwa watu wenye maradhi ya pumu/Asthma. Zipo dawa hazipaswi kutumiwa kwa watu wenye kisukari. Zipo dawa hazipaswi kutumiwa na watu wenye maradhi ya moyo. Zipo dawa hazipaswi kutumiwa kwa watu wenye maradhi ya damu. Je! Mtu anapoamua kutumia dawa au kumpatia mwingine dawa bila ushauri wa kitaalamu anazingatia hayo.

Nne, zipo dawa zinafanya kazi vizuri kabla ya kula, na zipo dawa zinafanya kazi vizuri baada ya kula.
Tano. Zipo dawa zinapaswa kutumiwa usiku tu, ili ziweze kuleta matokeo mazuri zaidi, au kudhibiti maudhi yasiotarajiwa.
Je! Mtu anayetumia dawa, au kumpatia ndugu/mtoto dawa bila ushauri wa kitaalam anazingatia hayo.

Sita, zipo dawa hazipaswi kutumiwa andapo tayari mtu amekwisha kutumia dawa nyingine. Pengine kazi za dawa hizo zinafanana, au zinakinzana, au pengine iliyokwisha tumiwa ina nguvu kuliko hii nyingine. Je! Hilo linazingatiwa?

Vipi kuhusu kutengeneza usugu? Matumizi ya dawa zinazodhibiti vimelea vya maradhi, mfano 'antibiotics' yanapaswa kuwa na utaratibu maalum. Matumizi yasio na utaratibu yanaweza kufanya vimelea hivyo kujitengenezea kinga, kuwa usugu dhidi ya dawa husika. Matokeo yake ni dawa hiyo kushindwa kufanya kazi.
Je! Wanaoamua kutumia dawa, au kuwapatia ndugu/watoto wao bila ushauri wa kitaalamu wanazingatia hayo?

- Dr. Christopher Cyril
 
Ushauri mzuri
 
asante mkuu,

watu tukielewa hili hata maswala ya 'treatment failures' yatapungua 'drug resistant germs' hawataongezeka ,
na hatutawapa shida madaktari katika ku'decide the right medication
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom