Matumizi sahihi ya jiko la gesi

Matumizi sahihi ya jiko la gesi

Nyongeza:
11- haya maelekezo hayawahusu wenye Geto ambalo ni single
 
Mbona namba 5 inakinzana na ile mitungi midogo? Au ile gesi sio sawa na mtungi mkubwa?
Maana hiyo mitungi midogo unapikia juu yake.
MATUMIZI SAHIHI YA JIKO LA GESI

No. 1
Gesi ya kupikia yaweza kuwa ya asili (natural gas), mitungi ya gesi (liquified petroleum gas) na gesi inayotokana na kinyesi (biogas)

No. 2
Gesi hizo ni zile ambazo zina tabia ya kuwaka kama vile butane, propane na methane.

No. 3
Gesi ni nishati nzuri na rahisi kuitumia ila ni hatari kama hautozingatia usalama

No. 4
Unapopika kwa kutumia jiko la gesi hakikisha kuna hewa ya kutosha ili endapo kutakuwa na uvujaji wa gesi yasitokee madhara.

No. 5
Hakikisha mtungi wa gesi haukai Karibu na jiko (cooking place) ikiwezekana mtungi wa gesi ya kupikia uwe nje ya jiko na mpira wa gesi utoke nje kuingia ndani

No. 6
Hakikisha unaweka mtungi wa kupikia ukiwa umesimama (upright) na hakikisha hauwezi kupata misukosuko yeyote ambayo inaweza kuuharibu mtungi huo.

No. 7
Hakikisha unaangalia valve, regulator na pipe kama viko sawa kabla haujaanza kutumia gesi ya kupikia.

No. 8
Unapotumia jiko la gesi usiache kitu Jikoni na wewe ukaondoka vinaweza kuungua na kusababisha moto au tatizo likatokea bila wewe kuona.

No. 9
Hakikisha unakagua mpira unaopitisha gesi mara kwa mara kwa kupaka povu la sabuni ili kuona kama kuna sehemu inavuja. Pia hakikisha unabadilisha mpira kila baada ya miaka miwili na valve baada ya miaka 3-5

No. 10
Ukitaka kujua mtungi wa gesi upo kiasi gani usiutingishe. Chukua kitambaa weka maji kisha paka kwenye huo mtungi kuzungushia kwa pembeni na utaona kiasi kilichobaki, Ni hatari kutingisha mtungi wa gesi ya kupikia.

No. 11
Mambo ya kuzingatia endapo utahisi harufu ya gesi ya kupikia jikoni;
-Hakikisha unafungua milango na madirisha hewa iingie na kutoka.
-hauwashi moto wa aina yeyote.
-hakikisha kama taa zimezimwa usiwashe na kama zimewashwa usizizime. -hakikisha hauwashi tochi au simu.
-Usipige picha kwa simu au camera.
-Toa mtungi nje ya jiko na ukague wapi unavuja.
 
Chukua kitambaa weka maji kisha paka kwenye huo mtungi kuzungushia kwa pembeni na utaona kiasi kilichobaki, Ni hatari kutingisha mtungi wa gesi ya kupikia.

Hakikisha mtungi wa gesi haukai Karibu na jiko (cooking place) ikiwezekana mtungi wa gesi ya kupikia uwe nje ya jiko na mpira wa gesi utoke nje kuingia ndani

Pia hakikisha unabadilisha mpira kila baada ya miaka miwili na valve baada ya miaka 3-5
  1. Ukishachukua kitambaa ukatia maji na kuupaka mtungi utaona nini mpaka ujue hicho kiasi cha gas kilichomo
  2. Kuna majiko yana gas cylinder compartment unayazungumziaje haya
  3. Maximum length ya mpira ni kiasi gani, na je hakuna teknolojia ya kutumia metal au copper pipes kwa usalama zaidi kuliko mipira
 
Inashauliwa urefu 1.5M hadi 2M kwa sababu za Kiusalama, lakini Pia ukizidisha kuweka Pipe ndefu zaidi Flow ya Gas Pressure yake inakuwa ndogo kidogo... Unaweza kuweka Pipe ndefu zaidi ya hiyo 2M ila zingatia sana Usalama
ukizidisha kuweka Pipe ndefu zaidi Flow ya Gas Pressure yake inakuwa ndogo kidogo

Kumbee! Me ndo maana niliongeza tundu pale kwenye valve maana pressure ilikuwa ndogo ikasababisha Moto kuwa mdogo pia!
 
Namba 12 kama unaishi stoo tumia mtungi mdogo!
Mtungi mdogo ni rahisi kuu'maintain' koki yake ni sh.10,000 tu.
Ni rahisi kuzima moto wa mtungi mdogo kuliko wa mtungi mkubwa.
Ni rahisi kujaza mtungi mdogo kuliko mtungi mkubwa.
Kama mifumo ya usalama kwenye nyumba yako ni mizuri na nyumba yako ni kubwa unaweza kutumia mtungi mkubwa.
NB: Natumia mtungi mdogo.
 
vijana wetu wasomi wa engineering ni wakati wa kupiga hela kwa kubuni technolojia rahisi itakayowasaidia watanzania juu ya hizi gas...

Either kubuni kaelectronic circuit ambako incase of gas leakage jiko lisiwake...
wabuni leak detector ambayo gas ikivuja yenyewe inapiga alarm kwa nguvu kiasi kwamba watu watajua mapema kabla jiko halijawashwa....
wabuni majiko yenye pressure gauge na gate valve before jiko, ukinunua jiko unapewa na pressure ya gas say 2psi, kabla ya kufungua valve hakikisha gauge inasoma 2psi ikiwa chini ya hapi usiwashe gas and cheki for the possible leak...

Wenzetu hutumia matatizo ya binadamu na kutengeneza solution ili wapate hela na kutengeneza ajira..
 
Back
Top Bottom