Matukio ya ujambazi ni matokeo ya serikali kuwapuuza vijana.

Molembe

JF-Expert Member
Dec 25, 2012
9,821
11,527
Kumekuwepo na ongezeko la matukio ya ujambazi hasa ule wa kutumia silaha hapa nchini, hali inayopelekea watu kuwa na wasiwasi na mali zao.
Hii yote inatokana na serikali kuwapuuza vijana na kutowapa muongozo wa nini cha kufanya mathalani kuna vijana wengi sana wanaohitimu elimu ya msingi na hawaendelei na masomo vijana hawa humezwa na jamii huku wengi wakijihusisha kwenye matukio ya uhalifu.
Kuna kundi lingine kubwa la vijana wanaohitimu elimu ya sekondari ambao hufeli nao hubaki mtaani bila mwelekeo mwisho wa siku hushawishika kuingia kwenye makundi ya kiuhalifu
Kuna kundi la tatu ni vijana wanaohitimu vyuo mbalimbali wakiwa na maono tele lakini hawa vijana nao hurudi mtaani bila kuwa na shughuli maalumu ya kufanya mwishowe hushawishika kuingia kwenye uhalifu.
Wito wangu kwa serikali iandae sera na miongozo mizuri ya kuwaendeleza vijana ili angalau tupunguze uhalifu maana kwa sasa wahalifu wanatishia usalama wa raia vijana wasiwe wanatumika tu wakati wa kampeni kuwaweka wanasiasa madarakani, nchi zilizowapuuza vijana wake ndio tunayaona ya Al shabab, Boko haram na uhalifu mwingine.
 
Back
Top Bottom