Matukio makubwa kwa mwaka 2015

Matukio makubwa kwa mwaka 2015

Mapengo 17

R I P
Joined
Mar 28, 2014
Posts
1,228
Reaction score
618
Katika kipindi cha mwaka huu kuna matukio makubwa yanayotarajiwa kufanyika, mojawapo ni kura ya maoni ya Katiba inayopendekezwa, ambayo inatarajiwa kufanyika Aprili 30. Tukio lingine kubwa la aina yake ni kufanyika kwa uchaguzi mkuu wa madiwani, wabunge, wajumbe wa Baraza la Wawakilishi, Rais wa Zanzibar na Rais wa Jamhuri ya Muungano.

Naunga mkono kauli ya Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein aliyotoa jana Januari 12, 2014 wakati wa sherehe za miaka 51 ya Mapinduzi ya Zanzibar ya kuwataka Wazanzibari na Watanzania kwa ujumla, kuwa makini na matukio hayo, ambayo ni sehemu ya kielelezo cha kukua kwa demokrasia nchini.



MWAKA huu ni wa matukio makubwa ya kihistoria.

Tunahimiza Watanzania wote, kuimarisha amani na utulivu na tunasisitiza kuwa matukio hayo mawili na mengineyo, yasitumike kuvuruga amani na utulivu wa nchi, ambayo ni hazina kubwa tuliyoachiwa waasisi wa Taifa letu, hayati Mwalimu Julius Nyerere na hayati Abeid Amaan Karume. Tunatakiwa kuimarisha amani na utulivu katika kipindi chote.

Ukiacha mambo hayo mawili, kuna jambo lingine linaloendelea huko Zanzibar; nalo ni mchakato wa kupokea maoni juu ya ugawaji wa majimbo. Kazi hiyo inafanywa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC).

Kwa mujibu wa Ofisa Uhusiano wa Tume hiyo, Idrissa Jecha, kwa sasa ZEC inaendelea na mchakato wa kupokea maoni na kuyachambua kuhusu ugawaji wa majimbo ya uchaguzi ya Zanzibar, kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu baadaye mwaka huu.

Ofisa huyo wa Tume anasisitiza kuwa hadi sasa hakuna uamuzi wowote, uliotolewa katika suala la ugawaji wa majimbo hayo, tofauti na baadhi ya watu wanavyovumisha mitaani. Kinachotakiwa ni tuache kuamini uvumi mitaani. Tuwasikilize wataalamu na watendaji wa serikali, wanavyotuambia.

Mathalani, katika suala la ugawaji wa majimbo Zanzibar, wanaopaswa kusikilizwa ni watendaji wa ZEC, ambao wanasisitiza kuwa Tume haijatoa uamuzi wa kugawa majimbo ya uchaguzi, bali ilitoa tangazo la kuwakaribisha wadau, kutoa maoni yao na kwa sasa Tume inayachambua maoni hayo kwa ajili ya kuyafanyia kazi.

Miongoni mwa wadau walioitwa na kutoa maoni yao kuhusu ugawaji wa majimbo ya uchaguzi na mipaka yake ni wananchi, wajumbe wa Baraza la Wawakilishi, wabunge, madiwani na viongozi wa vyama vya siasa.

Kwa mujibu wa Jecha, jumla ya viongozi 18 wa vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu, waliitikia mwito huo na kutoa maoni yao kwa njia ya maandishi. Kwa sasa tume hiyo inafanya uchambuzi wa kina na kuangalia maeneo hayo kikatiba na kisheria.

Lakini, suala hilo litarudishwa tena kwa wadau Februari kwa ajili ya kujadiliwa tena na kupokea maoni zaidi. Suala hilo linatarajiwa kutolewa uamuzi wake mwezi Machi. Hivyo, kama alivyoagiza Dk Shein Watanzania tunatakiwa tuwe makini mno mwaka huu, kwa sababu ni mwaka wa matukio makubwa.

Chanzo:Habarileo

 
Back
Top Bottom