Matokeo ya utafiti | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Matokeo ya utafiti

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kijakazi, Aug 10, 2012.

 1. Kijakazi

  Kijakazi JF-Expert Member

  #1
  Aug 10, 2012
  Joined: Jun 26, 2007
  Messages: 3,546
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 135
  Moja kati ya vitu nilivyogundua katika Utafiti wangu ambao ulinichukua katika nchi mbalimbali za kiafrika zilizo chini ya jangwa la sahara (Project) ni kwamba katika nchi zote hizo nimegundua kwamba Tanzania ndio nchi pekee ambayo ina nafasi kubwa sana ya kupiga hatua kubwa mbele ya kimaendeleo ukifananisha na nchi nyingi kama sio zote, nitaelezea kwa nini na mimi nilijikita sana ktk maswala ya mawasiliano.

  Tulipokuwa Nigeria tulisafiri sehemu kubwa ya nchi na tumegundua kwamba, Lugha ya mawasiliano ktk nchi hiyo ni kiingereza lakini ni chini ya asilimia 20 ya watu wa nchi hiyo wanaweza kuitumia hiyo lugha na kati hao wengi wanatumia kitu wanaita "Pidgin English" kwa hiyo kama ukija kwenye English proper namba inashuka zaidi chini ya hapo.
  Nikaenda Ghana nako stori ni hiyo hiyo, Uganda nako nikapata kama asilimia 8, Kenya nako ni chini ya asilimia 10.

  Sasa nataka kusema nini, ni kwamba hizi nchi zote ikumbukwe kwamba lugha ya Taifa ni kiingereza kwa maana kama hujui hiyo lugha "you are cut off" kabisa kwenye real economy au shughuli za kiuchumi, ina maana huwezi kufungua akaunti benki kwa maana fomu ni kiingereza, HUWEZI ELEWA MBUNGE WAKO ANAONGEA NINI BUNGENI kwa maana anatumia kiingereza bungeni, huwezi kosoma Gazeti na kujua nini kinaendelea, kwa kifupi hali ya maisha kwa mtu wa kawaida ni mbaya sana na nimegundua kwamba mtu wa kawaida hata hajui nini kinaendelea nchini mwake kwa sababu hawezi kupata habari (access of information).

  Mfano mdogo Uganda tulifika mji unaitwa Mbarara, tukiwa pamoja na Mganda tuliyetoka naye Kampala (mji mkuu) lakini cha ajabu ili tuweze kuwasiliana na kufanikisha kazi ilibidi tutafute mtu ktka Mbarara anayejua Kiingereza na lugha ya hapo ili aweze kutafsiri yaani huyu Mganda mwenzetu hakuweza kuwasiliana na waganda wengine ambao hawajui kiingereza, na hali hapa Tanzania ni tofauti kabisa utafiti ulikwenda vizuri tumefika mpaka vijijini watu wengi sana na ilinishangaza wanauelewa mkubwa sana kuhusu nini kinaendelea (kulinganisha na nchi zingine) wanasikiliza Bunge wanaelewa mbunge wao anaongea nini, anaweza akajaza fomu ya benki, anaweza kuandika Barua na kuendelea, kwa kifupi hata mafanikio ambayo CHADEMA inayapata leo yasingewezekana katika nchi ambazo tumepita kwani ni ngumu sana kufikisha ujumbe na hivyo watu kubakia tu kushabikia kikabila badala ya sera hayo ndio moja ya matokeo ya Project yangu
   
 2. Ruge Opinion

  Ruge Opinion JF-Expert Member

  #2
  Aug 13, 2012
  Joined: Mar 22, 2006
  Messages: 1,696
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  Hakuna utafiti wowote uliofanya ni ngonjera tu. Mimi nimeishakaa Ghana kwa muda wa kutosha. Literacy rate yao ni kubwa kushinda ya TZ. Kiingereza wanakimudu sana kwa sababu kinafundishwa vizuri toka shule ya msingi. Kwa hiyo mtoto wa shule ya msingi wa Ghana anaweza kuongea Kiingereza kumshinda msomi wa Chuo Kikuu wa TZ. Kwa Uganda ukweli ni kwamba lugha ya mawasiliano inayowaunganisha si Kiingreza bali Luganda (lugha ya kabila la Baganda). Makabila mengine yanelewa na kuongea Luganda kwa kiasi kikubwa. Hata Uganda mtu yeyote aliyepitia shule kidogo anaelewa na kuongea Kiingereza cha kuridhisha. Si ajabu kuingia vijijini na kukuta bibi kikongwe anaongea Kiingreza tena kwa kujiamini. Sasa hoja yako kuwa TZ ndiyo ina nafasi kubwa ya kupiga hatua kuliko wengine haina mashiko. Kama umeingia duka la vitabu lolote siku za karibuni utagundua kuwa kuna vitabu vichache sana vya maarifa mbali mbali vilivyoandikwa kwa Kiswahili. Hiyo elimu na maarifa yanahamishwaje kama haviko kwenye maandishi/vitabu. Na hapo sijaongelea uvivu wa waTZ wa kusoma. Ni ajabu hata "wasomi" wa chuo kikuu wana allergy na vitabu.
   
 3. mvingira

  mvingira Member

  #3
  Aug 13, 2012
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Huu ndio ukweli Watoto wa Nyerere hatutaki, tuache propaganda
  Nashukuru sana kwa kusema ukweli.
   
Loading...