Matokeo ya uchaguzi yawekwe hapa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Matokeo ya uchaguzi yawekwe hapa

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Nikupateje, Oct 29, 2010.

 1. N

  Nikupateje JF-Expert Member

  #1
  Oct 29, 2010
  Joined: Dec 22, 2009
  Messages: 1,314
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Waheshimiwa na ndugu zangu JF, salamuni popote mlipo,

  Mnivumilie kwa maelezo marefu kani naamini mtakapomaliza kuyasoma wengi mtafurahi na kuboresha nilicholeta..

  Kilio chetu siku zote kimekuwa ni tupate matokeo ya uchaguzi ikibidi dakika chache kura zinapomalizika kuhesabiwa kituoni. Vituo ni vingi, zaidi ya 50,000. Kweli tunahitaji kuchemsha bongo.amiria.

  Pokeeni spreadsheet hii ya microsoft excel niliyotengeneza ambayo unaweka matokeo ya kituo fulani kwenye mstari mmoja (row) na spreadsheet inajumlisha yenyewe, wewe huumizi kichwa.

  Kazi yetu sasa itakuwa ni kuingiza matokeo ya kura tu sanasana zilizopigwa na zilizoharibika labda na idadi ya waliotegemewa kupiga kura kituoni kama tutaipata ili nasi tungÂ’amue mapema wangapi hawakupiga kura.

  Nimeifanya iweze kuonyesha rangi ya kijani kwenye idadi iliyoongoza kituo, hivyo kukupunguzia muda wa kuanza kupepesa yupi ni mshindi kituoni. Simply ingiza matokeo chini ya kila chama halafu rangi ya kijani itajimulika pale kwenye kura nyingi kuliko zote kituoni.

  Spreadsheet ina worksheets tatu, nilizozipa majina ya URAIS, UBUNGE, UDIWANI. Najua tunajua microsoft excel lakini ninasisitiza kwa wale waenzetu wanaoweza kusaahu na kuishia kusoma worksheet ya kwanza tu ambayo ndiyo inafunguka ukishafungua document.

  Nimekumbwa na changamoto wakati naiandaa. Moja ni kwamba sikusumbuka kwenye worksheet ya URAIS kwani wagombea urais ni saba tu, hivyo column za matokeo ya vyama ni saba pia.

  Kwenye worksheet za UBUNGE na UDIWANI haikuwa rahisi kwani si vyama vyote vilivyosimamisha mgombea kila consituency. Hivyo nimekusanya nilivyoweza na hatimaye kupata vyama 18 na na sina hakika kama vyote vimo uchaguzini hivyo wataalamu mtarekebisha.

  Hivyo kwa UBUNGE/UDIWANI kutakuwa na column 18 na ni wazi pale chama kisipokuwa na magombea utaacha wazi bila kuandika kitu, usijihangaishe kuweka 0 kwani unaweza kujisahau na kuweka herufi O halafu formula za hesabu zikasumbua.

  Vilevile kwenye UBUNGE/UDIWANI inawezekana mkagundua chama/vyama nimevisahau. Iikiwa hivyo basi unaweza kuongeza column. Ila ukiongeza column hakikisha unakopi column nzima ya jirani na kui-paste hapa papya. Haina tofauti sana kama jimbo lina vituo zaidi na ikabidi uongeze rows ambako sasa nakopi row nzima ya jirani pale papya. Ukifanikiwa kukopi hivi formula zinazopiga mahesabu ya matokea zinabaki vilevile.

  Sifahamu zoezi la kuhesabu kura kama huanza kwanza kwa kutenganisha kura za kila mgombea, au huhesabiwa kwanza zinahesabiwa jumla yake. Nime-assume zoezi huanza kwa kutenganishwa moja kwa moja toka masandukuni, yaani inaokotwa kura, inahakikishwa na kila mmoja kuwa ni ya nani kisha inawekwa kwenye fungu la kura za chama kile.
  Kama ni hivyo basi kumbe hii spreadsheet inaweza kuwasaida hata mawakala ndani ya chumba cha kura kama ameamua kuwa laptop/computer ni kifaa chake kumsaidia kuhesabu kura kama wengine wanavyotumia calculator. Lakini pia kwa sababu spreadsheet hii itasmbaa na wengi wakajua hivyo basi wakala anaweza hata kutuma message kwa anayemuamini au aliyeko kwenye tally centre ambaye spreadsheet kama hii akiitumia hatakuwa na kazi zaidi ya kuingiza data na kuona matokeo.

  Akiweza atume kwa wengi maana kuna hatari nyingi kwa centre ya kujumlisha ikiwa sehemu moja tu bila kuwa na bakcup kwingine. Ikibidi humu humu JF tunusenuse tuzidake data hizo.

  Tulishauriwa kampenini kuwa hata kama jina halionekani kituoni nenda tu na kitambulisho chako kwani ndani ya dafatari kutakuwa na kila kitu kisichoweza kubadilishwa, hasa lile daftari liliandikwa jina lako kwa wino.

  Kama ni hivyo basi haijulikani ni wangapi watapiga kura na hivyo idadi ya waliopiga kura itabidi itokane na kura zenyewe zilizopigwa, tofauti na nilivyoweka humu na kama itabidi turekebishe hapo na formula iliyotumika na weni nikiwemo mimi tutajitolea kusaidia marekebisho.

  Mnaojua simu na email za wanaoonggoza vyama na kampeni muhimi zaidi watakaohesabu kura vituoni na za majumuisho basi ni vizuri kuwajulisha kuhusu hii document mara moja ikiwezekana waikague na waitumie. Na kazi ya kuikagua tuifanye wote kama experiment. Yaani ingiza majina kadhaa ya vituo hata ya kutunga na idadi yoyote ya wapiga kura hakikisha kama inakuletea usahihi.

  Ombi langu kwa MODERATORs wa JF ni kwamba wafikirie uwezekano wa non-members ku-download hii document tupate mawazo yao. Muda umetukimbia tunahitaji maoni haraka kutoka kwa yeyote.

  Jina la spreadsheet nimeiita DAR-ES-SALAAM kwa maana ya kwamba hii ni kwa mkoa wa DAR-ES-SALAAM tu. Kupata spreadshit za mikoa mingine ni kiasi cha kuibadili tu hii jina kwa kui-save hii kwa jina la mkoa ule unaotaka. Hivyo tutakuwa na spreadsheet zaidi ya 25 kila mkoa ukiwa na spreadsheet yake. Mfano spreadsheet ya Arusha iitwe ARUSHA.

  Spredsheet hii nilikuwa nimeweka nafasi ya vituo 100 kwa kila jimbo lakini nimepata tatizo kui-upload kwani ilikula 3megabytes na ZIP yangu si affective that much. Hivyo nimepunguza na sasa nimeweka vituo 50 lakini kila mmoja anaweza kuongeza rows kwa command ya insert rows kisha una-copy na kupaste kama tulivyoelekezna hapo juu. Ikitatiza naamini JF imesheheni wataalamu utasaidiwa.

  Tukiweza kupata idadi halisi ya vituo na majina kwa kila jimbo basi kwa matokeo ya urais tutaweza kutengeneza spreadsheet ya jumla inayo-link zote hizi za mikoa na kujumlisha kiurahisi.

  Idumu internet, Idumu JF na wadumu wana JF.
   

  Attached Files:

 2. Somoe

  Somoe JF-Expert Member

  #2
  Oct 29, 2010
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 757
  Likes Received: 147
  Trophy Points: 60
  kazi ipo:nono:
   
 3. M

  MC JF-Expert Member

  #3
  Oct 29, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 751
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Kazi nzuri mkuu.
   
 4. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #4
  Oct 29, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Swali langu je nikii-update kwenye mashine yangu itawezaje ku-update kwenye JF?
   
 5. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #5
  Oct 29, 2010
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Kazi nzuri kwa kweli. Hii ni changamoto kwa Mods wetu waweze kuweka link ambayo kila anayeingia pale ataupdate accordingly.Pia nashauri kuwa ingekuwa kwenye mtiririko wa kimkoa then wilaya. Kwa kufanya hivi wanaJF wangeweza kuweka ward zao kutegemea na mikoa waliko. Hii itasaidi wakati mtu anatafuta mathalani mkoa fulani aanjua uliko. Ila kwa kuanzia ni safi. Twende sasa tukaboreshe na kurahisisha.
  Ni mawazo yangu tu.
   
 6. N

  Nikupateje JF-Expert Member

  #6
  Oct 29, 2010
  Joined: Dec 22, 2009
  Messages: 1,314
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Ni lazima awepo dedicated person kwenye JF awe na kazi ya ku-update tu na apelekewe live update kila dakika zinapomalikizika kura kuhesabiwa.

  Ila unaweza kutuma hapa JF kwenye text kama hivi na wenye access ya ku-modify hii iliyoko humu wanweza kuingiza kiurahisi nikiwemo mimi niliyeleta document hii.

  Lakini tukumbuke tunatakiwa kuwa nazo zaidi ya 25 kwa mikoa mingine sasa sijui quota yangu ya ktumua ninapewa ngapi na kuna wachangiaji walisha-quotion kuhusu capacity ya JF na tuaimini kuwa hilo halina tatizo.

  Thread hii imekuja mchana na ndiyo kwanza inasomwa. Kufikia usiku leo lazima tutakuwa tumepata sounding contribution tufanyeje hata nisiyoweza kujibu peke yangu.
   
 7. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #7
  Oct 29, 2010
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,367
  Likes Received: 7,008
  Trophy Points: 280
  naungana na wewe Mkuu, hapo ni lazima hawepo mtu wa kuingiza hizo update, na huyo mtu atakuwa yupo tayari kuconfirm kwa watu zaidi ya mmoja ili matokeo yasiwekwe yale ya uongo
   
 8. N

  Nikupateje JF-Expert Member

  #8
  Oct 29, 2010
  Joined: Dec 22, 2009
  Messages: 1,314
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Mkuu,
  Nilijaribu unavyosema lakini imeshindikana kutokana na upload capacity kuwa exceeded. Kwanza nilidhani sintafanikiwa kabisa na ndipo ikabidi nipunguze si maneno tu bali hata mistari kama nilivyosema mwanzoni.

  Na hata ukiingalia hii haijaandikwa sana lakini tayari ina 120kb na hii ni kutokana na wingi wa formulas zilizomo.

  Ninachofurahi ni kwamba imekuwa uploded na sasa inaweza kuwa update hukohuko kweny server na si kwenye machine yangu tu au yako.

  Kuhusu mikoa na wilaya adnahi nilishasema hii ni mano wa D'Salaam tu na tunahitaji document zingine similar kwa mikoa mingine.

  Hii ya Dar unachofanya ni kuingiza jimbo na kituo tu maana ndizo constituency zenyewe.
  Tuendelee kuboresha.
   
 9. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #9
  Oct 29, 2010
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,793
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Jee kama wana jf watakua hawajapata matokeo yote na nec ikamtangaza jk mshindi wa urais kama alivyofanya kibaki kenya itakuaje?
   
 10. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #10
  Oct 29, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Shukurani, jaribu ku freeze na ku hide formula ili hata kama mtu atakosea kuandika sehemu hizo aki detete asiweze kuharibu formula, otherwise kazi nzuri.
   
 11. N

  Nikupateje JF-Expert Member

  #11
  Oct 29, 2010
  Joined: Dec 22, 2009
  Messages: 1,314
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Mkuu,

  Umenikumbusha. Unajua nimeitayarish harakaharaka asubuhi ya leo wazo la kufreeze lilikuwa halipo na badala yake nikawa nahangaika na hide ya protection na badala yake nkajikuta na-protect worksheet nzima.

  Na kwa vile leo ni Ijumaa ningekosa mchana huu kuituma isingepata response kubwa.

  Ninalifanyia kazi wazo lako la kufreeze formulas. Nipe dakika 20.
   
Loading...