The Chief Economist
Member
- Jan 18, 2013
- 51
- 47
Habari zenu wadau wa JF.
Imeonekana kwa muda mrefu sasa kuwa mambo mengi yenye matokeo hasi ambayo hayawezekani sehemu nyingi duniani, yanawezekana sana kufanyika nchini Tanzania.
Jamii ya kitanzania tunashuhudia uendelevu wa anguko la sekta elimu nchini ulioanzia mwaka 2006 ambapo ufaulu (pass rates) wa wanafunzi ambao as a best practice unatumika kama kipimo (indicator) ya ukuaji na kuboreshwa kwa elimu duniani.Kwa upande wetu Tanzania, anguko hili ni kwa matokeo ya mitihani ya Form II, Form IV na Form VI. Ninaamini kabisa (kwa kuwa nimeshawahi kuwa part-time lecturer) kuwa uduni huu wa ufaulu ni hadi elimu ya juu. Katika elimu ya juu siku hizi tunashuhudia wanafunzi wa Master programmes wana-SUP au ku-DISCO (discontinued) hali ambayo enzi zetu hukuwahi kuidhania. Inaonekana anguko la shule za sekondari ndio huzaa input (enrolled students) za vyuo vikuu.
Ningependa kujadili baadhi ya sababu zinazoweza kuwa ndio zimechangia kwa kiasi kikubwa kupelekea sekta nzima ya elimu kuanguka kiasi hiki na hivyo kuhatarisha viwango vya utaalamu unaotegemewa na taifa kuliendeleza. Utaalamu ni kwenye nyanja zote ambapo itapelekea kuwa na wachumi, wahasibu, madaktari, wanasheria, wahandisi, wataalama wa mazingira n.k wa karatasi tu. Na km Katiba haitarekebisha, tatizo zaidi litatupata kwenye kupata wanasiasa mahiri na wenye vision na sio drop-outs wa life struggle km wanavyoonekana sasa. Baadhi ya sababu ni kama ifuatavyo:
1. Kukosekana na mfumo halali na sahihi wa uendeshaji wa sekta ya elimu nchini ambapo kila kiongozi/waziri analetwa wake;
2. Kukosekana kwa mitaala iliyoboreshwa yenye kuzingatia hali halisi ya raslimali zetu na mahitaji ya soko na dunia kwa ujumla;
3. Uamuzi wa "ajabu" wa Mh. Rais wa kufuta mitihani ya darasa la Nne na Form II alioutoa wakati akiwa mgeni rasmi siku ya mkutano wa Baraza la Afya nchini kwenye ukumbi wa AICC, Arusha mwaka 2006. Katika hotuba yake, alishangaa kwa nini Mh. Mkapa kuweka msisitizo wa kusoma miongoni mwa wafanyakazi wa Serikali ambapo chini ya Katibu Mkuu wa Utumishi wakati huo Ndg. Rugumyamheto, wafanyakazi wote wa Serikali na ofisi za Umma walitakiwa kujiendeleza hadi angalau ngazi ya From IV kwa kipindi cha miaka kumi (1997 - 2007). Na ambaye asingepata cheti ajira yake ingesitishwa ambapo ilipelekea waalimu wa UPE, madereva, manesi, wahudumu wa ofisi (akiwemo mama yangu mdogo) na hata mawaziri akina Rais A.Karume, Mdhihir, nk kujiandikisha kusoma. Hii ilileta changamoto kubwa na taifa lilisisimka kwa kila mtu wakiwemo wafanyabiashara wengi kuanza kujisomesha. Kwenye hotuba yake, JK alishangaa kwa nini muugusi (nurse) ambaye kazi yake ni kuchoma sindano alazimishwe kusoma hadi Form IV. Aliuliza "...hivi kweli kuchoma sindano kunahitaji elimu ya Form IV"? Hii ni katika kujibu risala juu ya uhaba wa wauguzi na watumishi wengine kwenye sekta hiyo. Hivyo akaagiza huo utaratibu wa kulazimisha watu wajiendeleze ufutwe;
4. Agizo la Mh. Rais JK la mwaka 2007 la kufuta mitihani ya Darasa la IV na Form II nchini eti kwa kuwa inapunguza "completion rate" ikilinganishwa na watoto walioingia darasa la kwanza. Maana yake wasikariri darasa ili nchi ionekane wanafunzi wanaomaliza ni over 90% ya walioanza darasa la kwanza na hivyo kuonesha least drop outs (pitia Basic Education Statistics for Tanzania - BEST) vya Wizara ya Elimu vinatoa hizi ratios. Matokeo yake yalianza kuonekana kwenye matokeo ya 2010;
5. Mgomo baridi wa Waalimu uliotokana na ubabe wa Serikali kupitia Commercial Court wa kuzuia mgomo na kuwashtaki viongozi wa CWT ambapo waalimu wameendelea kulalamika chini chini;
6. Mazingira mabovu ya ufundishaji hasa kwenye shule zilizo nje ya miji mikubwa;
7. Mishahara duni na isiyo ya uhakika ambayo haiko kwenye mfumo wa compensation;
8. Kukosekana kwa mafunzo ya mara kwa mara ya waalimu katika Clusters zao;
9. Ufuatiliaji mdogo wa maandalizi na mafunzo yatolewayo mashuleni kupitia kwa wakaguzi wa shule ambao wengi hawana budget ya kufanyia shughuli zao; na
10. Mmonyoko mkubwa wa maadili ambao "utandawazi" umebarikiwa na hivyo kuisababishia jamii yetu kulea watoto kwenye mazingira yasiyo-support makuzi ya mtoto mwenye maadili, mwenye kuzingatia maelekezo ya wazazi na waalimu lakini pia mwenye kumwogopa Mungu na uthubutu wa kulitumikia taifa lake ipasavyo.
Najua wadau mnaweza kunirekebisha, kuboresha na kuongeza sababu zingine ili ikiwezekana JF i-compile some substantive contributions na kuzi-forward serikalini for Action.
Tiba yake:
1. Katiba mpya itoe mamlaka makubwa kwa wananchi ili kuifanya serikali iwe accountable na servant wetu;
2. Kuandaliwe mjadala wa kitaifa wenye lengo la kuibua mfumo mpya, sera mpya, mtaala mpya na mtizamo mpya juu ya umuhimu wa sekta ya elimu na R&D kwenye bajeti zetu zijazo ka maendeleo endelevu ya nchi yetu;
3. Kuboresha vifaa na stahili za utumishi wa sekta zote kuu za huduma na maendeleo;
4. Kusimamia maadili ya taifa kwa viongozi wakuu (wasile rushwa na kutumia madaraka vibaya) hadi kwa vijana na watoto ili kujenga nidhamu; na
5. Kupitia na kuangalia mfumo wa uendeshaji wa elimu kwenye shule za Kikristo hasa shule za Kanisa Katoliki (hapa simaanishi UDINI wowote) ambao wamefanikiwa sana kwenye kusimamia nidhamu, maadili na uwezo mkubwa kwenye kutawala akili za watoto hadi wanabaki wakijikita kwenye elimu zaidi na kutopata nafasi ya kujifunza zaidi ujinga.
Ni mchango wangu. Matokeo haya yameniuma sana kwa kuwa Investment in Human Capital ni chachu ya kuboresha productivity ya one of the factors of production (Labour) na hivyo kuongeza GDP na kuboresha welfare ya wananchi.