Kagondo
JF-Expert Member
- Jun 6, 2016
- 296
- 79
Fikra Pevu katika mijadala yake mingi, imebainisha kuwepo kwa matumizi ya madawa ya kulevya hapa nchini, licha ya serikali kuchukua hatua mbalimbali katika kudhibiti suala hili, huku wengi wakiathiriwa na madawa na wengine wakikamatwa lakini inashindikana kuwa funzo kwa wengine.
Utegemezi wa dawa za kulevya ni ugonjwa sugu lakini unaotibika, matibabu yake hupatikana baada ya kuleta madhara au kabla ya madhara ambapo muhusika hujiwahi na kuacha mwenyewe.
Kwa watu wengi, matumizi ya dawa za kulevya hugeuka sugu, na kurejea matumizi huwezekana hata baada ya muda mrefu wa kuacha. Kama ugonjwa sugu, unaorejearejea, kulevya kunaweza kuhitaji matibabu endelevu ili kuondoa kabisa athari za madhara.
Fikra Pevu inazidi kuwamulika Watanzania wengi ndani na nje ya nchi walioathirika kwa matumizi ya madawa ya kulevya, huku mtandao wa uuzwaji wa madwa hayo pia ukishika kasi, cha kushangaza ni wahusika wa matukio haya ni watu walioaminika na kuonekana kuwa kiio cha jamii.
Umoja wa Mataifa wasema ulitoa takwimu na kubainisha kuwa, Afrika Mashariki imekuwa kinara wa kupokea na kusafirisha madawa kwenda nchi za nje, pengine na vigogo wakihusika.
Ripoti hiyo, imesema jumla ya tani 64 za dawa za kulevya aina ya Heroine, zilisafirishwa bila kukamatwa kwenda au kupitia Afrika Mashariki, ikiwamo Tanzania kati ya mwaka 2010 na 2013.
Ripoti hiyo, imesema nchini Tanzania hasa mji wa Tanga, ndio kinara na njia kuu ya kusafirishia dawa hizo kwani tangu mwaka 2010, ukamataji uliongezeka kutoka kilo 145 hadi kilo 813 mwaka huu.
Takwimu hizo za kushtusha, zinatoa picha kwamba sehemu kubwa ya shehena za dawa za kulevya hupitishwa bila kugundulika au kukamatwa na vyombo vya dola.
Eneo la Afrika Mashariki, linaonekana kuwa kimbilio la wasafirishaji kutoka Asia hususani wa Afghanistan, Iran na Pakistan.
Wasanii wengi wameonekana kukumbwa na janga hili kwa wingi, wengi wakidai kuwa hujiingiza na suala hili kutokana na ugumu wa maisha na kudai hii hutumika kuondoa msongo wa mawazo kutokana na ugumu huo.
Mwanadada aliyewahi kung’ara kwenye tasnia ya muziki wa bongo fleva nchini na Afrika Mashariki, Rehema Chalamila ‘Ray C’, ameathirika kutokana na utumiaji wa madawa ya kulevya na kumletea madhara makubwa ya kiafya na kiakili pia.
Pia msanii Chid Benz ambaye jina lake halisi ni Rashidi Abdallah Makwiro, naye ameathirika sana na matumizi ya madawa, japo naye ameingia katika kundi la watu wanaopatiwa matibabu ya kuondoa madhara ya sumu ya madawa mwilini.
Taharifa kutoka vyombo mbalimbali vya habari, zikiwemo mitandao ya kijamii, inabainisha kuwepo kwa wasanii wengi Zaidi ya hawa wawili wanaojihusisha na matumizi ya madawa.
Hii upelekea kazi kudhoofika katika uingizaji wa kipato, pia hii hutoa picha mbaya na kupoteza matumaini kwa wale waliowachukulia watu hawa kama kioo kwao.
MATIBABU
Matibabu ya utegemeaji wa dawa za kulevya hutofautiana sana kulingana na aina ya dawa husika, kiasi cha dawa kilichotumika, muda wa utegemeaji wa dawa ya kulevya, matatizo ya kiafya na mahitaji ya kijamii ya mtu binafsi.
Uamuzi wa aina bora zaidi ya mpango wa matibabu kwa mtu anayetegemea dawa za kulevya hutegemea vigezo kadhaa kama vile: tabia, dawa za kulevya anazopendelea mtumiaji, dhana za kiimani au kidini, ugonjwa wa akili au kimwili, na upatikanaji na gharama zake.
Kumekuwepo na mtazamo kwa baadhi ya watu kuhusu utoaji wa matibabu haya.
Matumizi ya dawa ya kuondoa madhara ya madawa ya kulevya aina ya Methadone kwa waathirika inaonekana kama kuwatia kiburi cha wao kuendelea kutumia madawa Zaidi.
Hali halisi inaonesha kuwa, mpango wa utoaji wa matibabu utaongeza maradufu utumiaji wa dawa za kulevya, kwani watu hutegemea kupona pindi wakiathirika, hivyo hutumia bila woga.
Rais wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete, alimsaidia sana Ray C katika kufanikisha kupata matibabu, lakini jitihada zake hazikuleta mafanikio ya muda mrefu, kwani dada huyo amerudia tena utumiaji wa madawa na hali yake kuendelea kuathirika Zaidi.
Baadhi wengine wanaunga mkono suala la matibabu.
Wengine wanadai kuwa, hili ni janga kama majanga mengine ya kitaifa, hivyo watu wapewe matibabu ili warudie hali yao ya awali, na kuwaa hakuna haja ya kuwanyanyapaa.
Wanaona uwepo wa mahali pa kupatia matibabu ni lazima ili waathirika wapewe dawa.
Serikali na jamii kwa ujumla inapaswa kufanya yafuatayo kutokomeza suala hili.
Kupunguza upatikanaji wa dawa za kulevya kwa kuimarisha operesheni za ukamataji wa dawa za kulevya mitaani.
Kuteketeza mashamba ya bangi, Kuongeza utoaji elimu juu ya athari za dawa za kulevya kupitia vyombo vya habari, mikutano, semina, matamasha, sanaa na michezo, kuwa na sera na sheria madhubuti za kupambana na tatizo la dawa za kulevya.
Aidha, mapendekezo ya watanzania wengi yamebainisha kuwa, kuwepo kwa matibabu hakuna tija kwani huongeza kwa kasi watumiaji kuendelea kutumia madawa kwa kujipa moyo kuwa watatibiwa.
Serikali imejipangaje.
Rais wa awamu ya tano, Mweshimiwa John Magufuli, ametoa tamko la kuvunja mtantandao kuhusu wavurugaji wa Amani katika utumizi wa madawa ya kulevya.
Rais Magufuli alitoa maelekezo mahsusi kupitia kwa aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Charles Kitwanga akielekeza kuwa anataka kuiona Tanzania isiyokuwa na wauzaji wala watumiaji ‘unga’.
Rais aalinukuliwa akisema haiwezekani wauza unga wakawa na nguvu kuliko Serikali, na hivyo kuahidi kupambana nao.
Pengine kwanini juhudi za kukomesha janga hili linakwama.
Inaonesha wahusika wengine katika mtandao huu ni wale wenye dhamana ya kukataza matumizi ya madawa, kama vile, viongozi waliopo madarakani na polisi wenye dhamana ya kuwakamata waalifu.
Serikali ya Awamu ya Nne, iliamua kupambana na dawa za kulevya kwa kubadili sheria na ikaelekeza kuanzishwa kwa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya, lakini hadi sasa mpango huu unaonekana kusuasua na kuingiliwa upya na rais wa sasa mweshimiwa Magufuli.
Matumaini makubwa ya Watanzania sasa yapo mikononi mwa Rais Magufuli, kwani inaelezwa kuwa yeye hana ushirika, huruma wala hofu na wafanyabiashara ambao baadhi yao wanafanya biashara ya dawa za kulevya.
Ni wajibu wakila mwanajamii kukataa janga hili la madawa ya kulevya, kwani limekuwa tatizo linalowapelekea wapendwa wetu kupata matatizo na madhara makubwa kiafya ikiwemo akili kuvurugika.