Babu wa Kambo
JF-Expert Member
- May 2, 2016
- 559
- 808
Kufuatia kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi wa Oktoba 25 mwaka jana, maisha Kisiwani Pemba yamekuwa magumu na kurejesha wakazi wake kwenye mateso waliyokumbana nayo kati ya mwaka 1995.Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (Zec), Jecha Salim Jecha alifuta matokeo hayo siku ambayo alitakiwa atangaze mshindi wa urais, huku matokeo ya majimbo 31 yakiwa tayari yametangazwa na matokeo ya majimbo mengine tisa yakiwa yamehakikiwa na washindi kupewa vyeti vyao.
Jecha alitangaza uchaguzi mpya Machi 20, uliosusiwa na CUF ambayo ilitangaza kutoutambua
ambao umesababisha wananchi kubaguana katika misiba, sherehe, vyombo vya usafiri na
biashara, jambo ambalo limethibitishwa na polisi, viongozi wa mikoa ya Kusini na Kaskazini Pemba na wa vyama hivyo viwili.
Katibu wa CUF Wilaya ya Micheweni, Khatib Hamad Sheikh na katibu wa chama hicho Wilaya
ya Wete, Riziki Omar Juma wanasema wafuasi wao wataendelea kutoshirikiana na CCM kwa
sababu Serikali imewabagua muda mrefu.
Katibu wa CCM wa Wilaya ya Kaskazini Pemba, Hadija Nassor Abdi anasema uhasama baina ya
wanachama wa CUF na CCM ni mkubwa kiasi cha kutoshirikiana katika shughuli za jamii.
Chanzo: MWANANCHI