salimkabora
JF-Expert Member
- Nov 10, 2012
- 2,441
- 654
Wana jf Nimefatilia sana maongezi kati ya waziri mkuu wa zamani wa Kenya na mwandishi Balile aliyekuwa anaongoza kamati ya jukwaa la wahariri kuchunguza matukio ya kijinai zidi ya wanahabari na kugundua maongezi yale yanaibua mzizi mkuu wa ghasia na mauaji katika jamii yetu kuwa ni upendeleo katika kugawa madaraka kwa maana ya kwamba watu wanapewa madaraka si kwa sifa walizonazo bali kiupendeleo aidha wa kidini, kirafiki, kindugu, kishemeji, nk. Kwa mfano Igp hawezi kuwa na sababu ya kujipendekeza kwa Rais au wanasiasa wengine kama anajua wazi yeye ndiye bora kuliko yoyote mwingine ndani ya Jeshi husika na kama inaaminika kigezo hicho ndicho kinachotumika kuteua igp. Ingekuwa hivyohivyo kwa nafasi zingine serikalini kama vigezo vinavyotumika viko wazi na wahusika wanalazimishwa na sheria kuvifata; hakutakuwa na sababu mtu serikalini kutoa siri na kuipeleka upinzani ili wakiingia madarakani apewe uwaziri ambao hana sifa nao; wala polisi hatauwa watu ovyo kujipendekeza kwa wakubwa apewe cheo. Kwenye idara yoyote watu wanajijua nani anastahili kupanda kabla ya wengine na kama vigezo vinafatwa matatizo yetu ya kuuwana na kuchimbana yasingekuwepo. Hebu wana jf tujadili hapa njia bora na sahihi pamoja na vigezo muafaka vya kuwezesha watu kuteuliwa katika ngazi mbalimbali na ikiwezekana tuingize kwenye katiba mpya.