Matatizo yetu kama jamii ni zaidi ya Katiba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Matatizo yetu kama jamii ni zaidi ya Katiba

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by garikicah, Jan 27, 2011.

 1. garikicah

  garikicah Member

  #1
  Jan 27, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 68
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 15
  hivi ni kweli kwamba matatizo yetu yote tuliyonayo ni sababu ya katiba? na ni kweli kwamba katiba tuliyo nayo haitoi maelekezo ya nini cha kufanya juu ya rushwa na ufisadi? hivi tukipata katiba mpya haya yote, hatutayasikia kabisa na sasa itakuwa ni neema tu?.........there is a spritual dimension we have to concider here. sisi kama wanadamu, wanajamii kwa namna yoyote ile hatuwezi kushinda vita hii bila kumlilia yeye aliyetuweka hapa ulimwenguni.tamaa ya mali mamlaka, kupenda anasa,wizi, ujambazi,ufisadi, rushwa, mauaji, uongo, uzinzi, ufiraji,kutokufanya kazi, ulaghai,chuki, kujipenda na mengine mengi ndio yametufikisha hapa.

  mimi naona huzuni maana adui wetu mkubwa (shetani) hatumzungumzii kabisa, kafanikiwa kutugawa katika imani, dini, na hata tunashindwa kujua chanzo cha yote haya. ile roho ambayo wengine waniita ya ubinadamu imekwisha toweka ktk mioyo ya watu, (mi naiita roho wa mungu) tunatawaliwa na roho ya uharibifu ambayo ni ya shetani. Roho hiyo ya MUNGU hairudi kwa siasa, sheria au katiba hata siku moja? ni kwa sala za toba na maombi makali, juu ya rehema za mwenyezi mungu kutuvusha na kutuokoa ktk makucha ya adui tuliye nae.

  dunia tunayoishi ipo katika wakati mgumu wa kufunga historia yake, huu ni utungu umeanza na unaenea mahali pote, adui amekalia kanisa adui amekalia msikiti adui ana ajenda moja tu,anaua imani na mwili. mambo haya ndugu zangu yameandikwa sio kwangu tu kwa mataifa yote. sisi sote tunayajua maandiko hayo, tumesikia, tuna amini lakini hatutendi kama tunavyo agizwa, tumeasi tunatafuta njia zetu binafsi zisizo asili yetu tukidhani tunajisaidia kumbe tunazidi kwenda mbali na ukombozi.

  ndugu zangu, kumbukeni tumeumbwa kwa mfano na sura ya MUNGU, the most high GOD, yeye katufanya kuwa watoto wake kwa manabii na mitume wote katufunulia ukuu, uwezo na rehema zake, katuhakikishia tukiamini na kujinyenyekeza mbele zake, kufuata njia yake, malipo yake ni kupewa kutawala pamoja nae ,utawala usio na mwisho..........basi tunapo kuwa tunajadili matizo yetu kama wanadamu fahamu kwamba tumepewa uhuru wa kuchagua, na makundi ni mawili tu, umfute yeye au umfuate shetani ambaye tayari kesha hukumiwa na anasubiri adhabu ya kuangamizwa, lakini katika kipindi hicho kapewa nafasi ya kujifunua na kujidhihirisha namna ya serikali yake ilivyo na watu wake wanavyotakiwa kuwaje,. ndipo bwana MUNGU wa majeshi awatenge watu wake pia kutoka ktk makucha ya mwana wa kuasi.
  mambo haya yalitabiriwa zamani zile, kwamba mtakapo ona watu wanaanza kujipenda nafsi zao wasithamini wengine, ufiraji ukieenea kwa kasi kwa walio oa na walio nje ya ndoa, makanisani, misikitini, ufisadi, rushwa,uongo, dhuluma,ugaidi,serikali na dini zikiutukuza na kualalisha uchafu kwa kuwafurahisha watu wao, matetemeko, mvua kubwa(mafuriko) vita, na tetesi za vita, mauaji ya kutisha na aina zote
  za uovu na uchafu. basi WATU WANGU CHANGAMKENI MKAVIINUE VICHWA VYENU,maana saa ile imewadia. swali ni yapi kati ya haya hatujayasikia,ama kuyatenda, au kuyaona???????????
  ndio maana nasema sisi sote ni mashaidi tukubali kukiri, kutubu, na kuomba na kusamehe kama vile sisi tunavyo samehewa si kwa kuwa tuna stahili bali kwa rehema zake MUNGU zisizo chagua dhambi, tutakapomuita kwa sauti ya toba bwana anasikia bwana anasemehe na yeye huokoa.

  Ikiwa tukipuuza na kuona kwamba tunayaweza yote bila yeye hata hii katiba tunayolilia pakage yake itawekwa vitu ambavyo wewe mwenyewe hutaweza kuamini kama ni wanadamu wanaojiita wameendeleea na wasomi wanaweza kupanga mikakati na taratibu za taifa hivyo. NDUGU ZANGU, hakuna kitu shetani anatoa bure! hakuna! chochote anachokifanya atakachokupa ni kwa kubadilishana na roho yako, hiyo ndio gharama unayo mlipa. ndio tutapata katiba tena iliyo huru sana na inayowajibisha kiongozi ama viongozi hata rais, lakini ndani yake kawapa uhuru na ulinzi waovu na kupewa sheria ya kuwalinda ili waongeze(aongeze) jamii ya anasa na heshima kwa dhambi na uovu.
  msininukuu vibaya sipingi katiba mpya bali nachelea kusema sisi tu kwa uwezo wetu bila kumshirikisha MUNGU hatuwezi kufumbua fumbo za shetani. mfano mzuri angalieni mataifa yote yaliyo endelea marekani na ulaya, wanakatiba nzuri tu za kulinda maslahi na resources za nchi zao, hata kwa kuhujumu mataifa madogo, njoo katika jamii zao, ndoa za jinsia moja, ufiraji wa wake na watoto wao,uhuru wa mtoto kuishi atakavyo, matabaka kuongezeka kuporomoka kwa maadili ya jamii, hata wanyama wananafuu hawaishii hivyo, mapato ya serikali yanayotokana na uchafu,dhuluma, na kodi zinazo tokana na madanguro ndizo tunazo tumia kujengea shule, hospitali,barabara na huduma za maji. tunaishi katika ulimwengu ambao unaelekea ukingoni. tumuombeni mungu angali anapatikana atuvushe na dhoruba hizi kali.
   
Loading...