Matatizo yaliyopo kwenye vyuo vya Tanzania

TanzaniaHuru

Member
Apr 2, 2016
13
7
Jamani hivi vyuo vya afya hapa Tanzania hasa ngazi ya Certificate na Diploma mbona vinaongozwa kilocal sana. Unakuta wakuu wa vyuo na Drs ambao wanafundisha wamekua mungu watu.

Mbaya zaidi wanaleta shida zao za binafsi na kuziingiza kwenye masomo ya wanafunzi.

Nimepokea malalamiko kadha wa kadha kwa miaka kadhaa juu ya malalamiko dhidi ya Drs wakileta maisha magumu kwa wanafunzi kwa namna mbalimbali.

1. Wakifelisha wanafunzi kwa uzembe wao.
2. Wakiferisha wanafunzi kwa personal conflicts zao.
3.Uongozi mbovu usio na ratiba za kueleweka.
4.Unyanyasaji wa kijinsia n.k

Maombi yangu serikali na wizara husika iangalie upya uendeshaji wa vyuo hivi,kuna ukatili na uonevu wa hali ya juu unaoendelea...

Nimekua nikisikia rumors sana kuhusu chuo Cha Madaktari Mtwara, naomba waandishi wa habari mtusaidie kwa hili,mkahojiane na wanafunzi huko Mtwara tuokoe taifa letu.

 
Mtwara hapo kuna dogo anamaliza mwaka huu alimkatalia teacher kimapenzi teacher kajenga bifu mpaka teacher kamtafutia kosa dogo akasimamishwa chuo mwaka mzima, afu dogo kwao maskini anaishi na mama yake tu dah thank God alirudishwa chuo
 
Back
Top Bottom