Matatizo ya Serkali kwa wananchi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Matatizo ya Serkali kwa wananchi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mtamanyali, Sep 6, 2012.

 1. mtamanyali

  mtamanyali JF-Expert Member

  #1
  Sep 6, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 1,127
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  katika hali isiyo ya kawaida mama mmoja anayejulikana kwa jina moja la songela amepinga na kudharau agizo la mkuu wa wilaya ya Iramba lililomtaka atoke kwenye nyumba katika kipindi kisichozidi siku thelathini. Nyumba hizi zinajulikana kama nyumba za wachina zilizopo katika kijiji cha kizaga kata ya ulemo wilayani Iramba. Kwa mujibu wa chanzo changu cha habari kinaanasema baada ya kumalizika kwa ujenzi wa barabara nyumba hizo zilikabidhiwa kwa shule ya sekondari kizaga ili itumike kama makazi ya walimu. Kinyume na maagizo hayo mama huyo kwa kushiriana na mkuu wa wilaya aliyemaliza muda wake walichukua nyumba hizo na kuzigeuza kama zao kwa muda mrefu sasa. Baada ya kuja kwa mkuu wa wilaya mpya alitoa agizo kwa mama huyo kwamba anatakiwa aondoke katika nyumba hizo kabla ya siku thelathini. Cha ajabu mama huyo hajaondoka na mpaka sasa hakuna chochote kinachoendelea. Kitendo cha mama huyo kukataa amri ya mkuu wa wilaya kimetafsiriwa na wananchi kama ni udhaifu mkubwa kwa serikali. Wananchi hao wanadai kwamba Mkuu wa wilaya ni mteule wa raisi na hivyo kupigwa kwa amri yake ni kumdhalilisha yeye na serikali yake kwa ujumla.
   
 2. kibogo

  kibogo JF-Expert Member

  #2
  Sep 6, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 9,477
  Likes Received: 784
  Trophy Points: 280
  Mh! umeamka na mning'inio wa ziada, mbona unaweka hoja za kitoto hivi
   
 3. mtamanyali

  mtamanyali JF-Expert Member

  #3
  Sep 6, 2012
  Joined: Dec 6, 2011
  Messages: 1,127
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  Ndugu katika utwala hakuna jambo la kitoto. Wewe unafikiri kama leo mtu anapinga agizo la mkuu wa wilaya na hakuna hatua zinazochukuliwa na wananchi wanaona unafikiri wananchi hao hao kesho wakipewa maagizo na huyohuyo watatii? na je wasipotii watakuwa wamefanya kosa? wanaojua kanuni za utawala wanafahamu kwamba hoja yangu ni nzito na madhara yake sio lazima uyaone leo.
   
 4. wijei

  wijei JF-Expert Member

  #4
  Sep 6, 2012
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 469
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  mkuu wa wilaya ndo kitu gani? Hicho cheo sikitambui kwenye kichwa changu,ndio maana kwenye katiba mpya tunataka kifutwe kabisa.hawa ni makada wa chama kwa hiyo magizo yao huwa ni yakisisiemCCM.
   
Loading...