Matatizo ya Mzio (Allergies) Mbalimbali: Visababishi, Madhara, Kinga na Tiba

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,331
33,141

Mzio au aleji (allergy) ni matokeo ya mpambano uliopitiliza kati ya kinga ya mwili na kitu chochote (ambacho kwa ujumla huwa hakina madhara kwa mwili) inapotokea kimeingia ndani ya mwili au kimegusa sehemu fulani ya mwili.

Aleji husababishwa na nini?
Kuwa na mzio ni jambo la kawaida. Haishangazi basi kuona kuna baadhi ya watu wanakuwa na mafua karibu kila siku au wengine wanashindwa kuvaa baadhi ya vitu kama saa au cheni za dhahabu kwa vile tu huvimba mwili au kuwashwa pindi wanapofanya hivyo.Kwa kawaida kinga ya mwili huulinda mwili dhidi ya vitu mbalimbali hatari kwa afya kama vile vimelea vya bakteria na virusi, lakini wakati mwingine inaweza kupambana pia na vitu ambavyo havina madhara yeyote kwa mwili (ambavyo huitwa allergens). Watu wenye aleji/mzio huwa na hisia zisizo za kawaidaza mwili dhidi ya baadhi ya vitu.Mwili unapokumbana na vitu vinavyosababishia aleji (yaani allergens), mfumo wa kinga ya mwili huzalisha kemikali mbalimbali ikiwemo histamine ambayo hupambana na allergens hizo.

Mpambano huu ndo husababisha mtu kuwa na dalili za aleji/mzio.Matatizo ya kinasaba pamoja na hali tofauti tofauti za kimazingira zote zinahusika sana katika kusababisha mtu kuwa na mzio. Baadhi ya vitu vinavyosababisha mzio (allergens) ni pamoja na vumbi vumbi, baadhi ya dawa, baadhi ya vyakula, kung'atwa na wadudu kama vile nyuki, aina fulani ya uyoga, vumbi vumbi la maua (pollens) n.k.Wapo baadhi ya watu ambao hukumbana na mzio pindi wanapokuwa katika mazingira ya joto au baridi wakati wengine hupatwa na mzio pindi wanapopigwa na jua kali. Wakati mwingine, hata msuguano kidogo tu wa ngozi unaweza kuwasababishia baadhi ya watu dalili fulani fulani za mzio.Kama nina aleji mtoto wangu pia anaweza kupata aleji hiyo hiyo?

Kwa kawaida, mzio wa aina fulani huwa haurithishwi miongoni mwa wanafamilia. Kwa mfano kama mzazi ana aleji na baridi si lazima watoto wake pia wawe na aleji hiyo hiyo ya baridi ingawa wanaweza kuwa na aina nyingine ya aleji. Uwezekano wa mtoto kupata aleji huongezeka zaidi iwapo wazazi wote wawili wana aleji na vitu fulani fulani na huwa mkubwa zaidi iwapo mama ndiye mwenye aleji.Nini dalili za mtu mwenye aleji?

Dalili za aleji zipo nyingi kutegemeana na eneo gani la mwili linahusika, lakini kwa ujumla-Kama ni mfumo wa hewa ndiyo ulioguswa, mtu anaweza kuwa na matatizo katika kupumua (kikohozi au kubanwa na pumzi, makamasi na kuziba kwa pua, muwasho kwenye pua na koo, au kupumua kwa kutoa sauti kama mtu anayepiga filimbi)- Kama macho yataguswa, muhusika hujihisi hali ya kuchoma choma, kutiririkwa na machozi na muwasho kwenye macho, macho kuvimba na kuwa mekundu- Iwapo mtu atakula kitu ambacho ana aleji nacho anaweza kuwa na dalili kama vile kuharisha, kichefuchefu, kutapika, Kusokotwa au kuumwa na tumbo au hata hali mbaya ya kutishia maisha.- Allergens zinazogusa ngozi zinaweza kusababisha ngozi kuwa na mabaka mabaka, kubabuka, kuvimba, muwasho, kuota vipele na malengelenge, michubuko au ngozi kuwa nyekundu.- Aleji zinazohusisha mwili mzima zinaweza kuwa na mkusanyiko wa dalili zote za hapo juuWakati mwingine aleji inaweza kuzorotesha hali ya baadhi ya watu wenye magonjwa kama ugonjwa wa ngozi wa eczema au pumu kufanya iwe mbaya zaidi.

Vipimo na uchunguzi Mgonjwa ataulizwa kuhusu historia ya tatizo lake, ni lini lilianza na vitu gani humfanya awe hivyo. Aidha tabibu pia atapenda kufahamu kuhusu dalili nyingine zinazoambatana na tatizo linamlomkabili mgonjwa.Baadaye vipimo vya aleji vinaweza kufanyika ili kufahamu hasa ni kitu gani mgonjwa ana aleji nacho na kama kweli dalili alizo nazo mgonjwa ni kweli zinatokana na aleji au zinatokana na sababu nyingine.

Hii ni kwa sababu kuna baadhi ya mambo yanaweza kumsababishia mtu kupatwa na dalili zinazofanana kabisa na mtu aliye na aleji ya kitu fulani. Kwa mfano matumizi ya aina fulani ya dawa zinaweza kumsababishia mtu kupata mikwaruzo au michubuko katika ngozi inayofanana na aleji nyingine, au mtu anaweza kuwa na mafua au kikohozi kwa sababu ya maambukizi ya bakteria au virusi na si kwa vile inatokana na aleji.

Kipimo maarufu kabisa cha kutambua aleji kwa mtu ni kipimo cha ngozi (skin testing) ambapo mgonjwa huwekewa baadhi ya vitu vinavyohisiwa kumletea aleji juu ya ngozi yake na kisha ngozi huchomwa kidogo kwa sindano ili hivyo vitu viweze kuingia ndani ya ngozi wakati huo daktari akichunguza kama kuna mabadiliko yeyote (kama vile uvimbe au ngozi kuwa nyekundu) katika eneo lilichomwa.

Kipimo cha namna hii hufaa zaidi kwa watoto wadogo kwa vile ni rahisi kufanyika kwao bila usumbufu mkubwa sana.Aina nyingine yay kipimo cha aleji cha ngozi hufanyika kwa kubandika vitu vinavyohisiwa kuleta aleji kwenye ngozi (patch testing) au kuchoma sindano zenye allergens sehemu ya juu ya ngozi
(intradermal injection) na kuchunguza uwepo wa mabadiliko yeyote katika ngozi.

Vipimo vingine ni pamoja na vipimo vya damu huonesha ongezeko la immunoglobulin E ambayo huashiria uwepo wa vitu vinavyosababisha aleji, na kipimo chaFull Blood Picture chenye kuonesha ongezeko la eosinophil (ambayo ni sehemu mojawapo ya chembe nyeupe za damu) iwapo kuna aleji.Lakini pia daktari anaweza kukushauri kuepuka baadhi ya vitu hasa dawa au aina fulani za vyakula ili kuona kama utapata nafuu yeyote au kukushauri kutumia baadhi ya vitu anavyohisi vinakuletea matatizo ili kuona kama utapata dalili zozote zile.

Ni kweli Aleji inatibika?
Njia bora kabisa ya kutibu na kupunguza uwezekano wa kupata aleji ni kutambua kitu au vitu vinavyokusababishia hali hiyo na kuviepuka. Kama ni chakula au dawa au kemikali, epuka kabisa matumizi yake, na kama ni vumbi jitahidi kukaa nalo mbali. Kadhalika shambuli kali la aleji laweza kusababisha muhusika kulazwa hospitali kwa vile lisipothibitiwa kifo kinaweza kutokea.

Zipo aina mbalimbali za dawa zitumikazo kutibu na kuzuia aleji, kulingana na jinsi daktari wako atakavyoona inafaa kutegemeana na ukali wa tatizo, dalili zake, umri wako pamoja na hali yako ya afya kwa ujumla. Dawa hizi ni pamoja na za jamii ya antihistamines, za jamii ya corticosteroids ambazo ni maalum kwa kutuliza mcharuko mwili ambazo huwa katika muundo mbalimbali kama vile cream, matone ya kuweka machoni au masikioni, za kuvuta au kupulizia, sindano au vidonge.

Kwa wale wenye mafua na kuziba kwa pua, hushauriwa kutumia dawa zinazosaidia kuzibua pua, hata hivyo dawa hizi hazina budi kutumiwa kwa uangalifu hasa kwa watu wenye magonjwa ya shinikizo la damu au moyo. Dawa nyingine ni zile zinazosaidia kuzuia vitu vinavyosababisha aleji.

Nini cha kutarajia kwa mtu mwenye aleji?
Aina nyingi za aleji hutibika kwa urahisi kwa kutumia dawa. Wapo baadhi ya watu hususani watoto wanaweza kujenga hali ya aleji dhidi ya aina fulani za vyakula, hali wanayoweza kuendelea nayo mpaka ukubwani. Kwa kawaida, kitu kikimletea mtu aleji tu mwanzoni huendelea kummuathiri daima.

Kuna madhara yeyote ya kuwa na aleji?
Madhara ya aleji ni pamoja na kupata shambulio kali la mcharuko mwili ambalo linaweza kusababisha kifo kama usipotibiwa haraka. Wapo baadhi ya watu, kwa mfano, wakila kumbi kumbi huvimba mwili na kushindwa kupumua mpaka kuhitaji kulazwa hospitali na kusaidiwa kupumua kwa mashine. Madhara mengine ni pamoja na shida ya kuvuta pumzi au kushuka kwa shinikizo la damu (kupata shock).

Nitajikingaje dhidi ya aleji?
Jambo la msingi la kufahamu ni kuwa, kuwa na aleji si uchawi. Pindi mtu anapopatwa na aina fulani ya aleji, kinga bora ni kukwepa mambo yote yanayoweza kuchochea kutokea kwa shambulizi la aleji. Kama ni chakula, jitahidi kukwepa aina hiyo ya chakula na kama ni dawa, acha matumizi yake na pia mueleze daktari wako au muuguzi kuhusu hali hiyo mapema kabla hajakupatia dawa hizo pindi unapokwenda hospitali kwa matibabu ya matatizo mengine.Wapo watoto wachanga ambao hupatwa na aleji mara tu wanaponyweshwa maziwa ya ng'ombe kwa mara ya kwanza. Hii hutokana na aina fulani ya protini iliyopo kwenye maziwa haya. Ili kuwakinga wasipatwe na aina hii ya aleji, mama hushauriwa kunyonyesha mtoto kwa angalau miezi minne ya mwanzo huku akiepuka kumpa maziwa ya ng'ombe katika umri huu.Baadhi ya kinamama hudhani kwamba kubadilisha aina ya chakula wakati wa kunyonyesha kunaweza kusaidia kumuepuesha mtoto asipatwe na aleji.

Hii si kweli kwa vile imeonekana kitendo hiki hakisaidii kumkinga mtoto dhidi ya aleji.Uchunguzi mwingine umewahi kuonesha kuwa watoto waliozaliwa katika mazingira ya vumbi vumbi na mifugo (yenye kiasi kikubwa cha manyonya ya wanyama na vumbi) wana uwezekano mdogo wa kupata aleji ya vitu vya aina hii pindi watakapokuwa wakubwa ikilinganishwa na wale waliozaliwa katika mazingira yasiyo na hali hizo. Hii ni kwa vile, mazingira ya vumbi huwajengea watoto hawa aina fulani ya 'kinga' dhidi ya aleji tofauti na wenzao. Hata hivyo, watoto waliohamia katika mazingira haya wakiwa na umri mkubwa wameonekana kuathirika kwa vile wamekosa ile kinga ya utotoni.


BAADHI YA MASWALI YA WADAU
Wakuu nikila nyama napata allergy, mwili unawasha najikuna hadi navimba,nina maanisha nyama ya wanyama wote waliwao hususan hapa Tz, ila nikila samaki hakuna shida.Sasa kwa waelewa wa hii kitu nitumie dawa gani nipone?


BAADHI YA MICHANGO YA WADAU

PIA, SOMA:

Unywaji maji, lishe yenye binzari zinavyotibu aleji

Pia, katika lugha nyingine nyepesi, aleji inaelezwa kuwa kitendo cha mwili kupungukiwa maji wakati kitu kinachoitwa ‘histamini’ kinapozalishwa kupita wastani, ili kuhimiza unywaji maji na ugawanyaji wa kiasi kidogo cha maji kipatikanacho katika mwili.

Histamini, kimsingi ni kihisio cha kwanza (primary sensor) cha ubongo kinachozalishwa ili kujishughulisha na ugawanyaji maji kwa viungo muhimu, wakati kunapokuwepo upungufu wa maji.

Inafanya kazi ya ugawanyaji kiasi kidogo cha maji kinachopatikana (maji ya mgawo kutokana na wewe kuendelea kusubiri kiu, ndipo unywe maji) wakati wa upungufu wa maji mwilini

Madhara ya aleji yanapompata mtu ni kama maradhi. Ili kujitibu aleji, kuna njia nyingi za kiafya zinazotumika. Hapa zipo njia kadhaa za asili. Inashauriwa kuwa, ni muhimu mtu akajitibu aleji kabla haijawa sugu.

Tiba ya Binzari
Je, unatafuta dawa ya asili nzuri na yenye uhakika ya kutibu aleji? Au umechoka kutumia dawa zenye kemikali inazokuacha na madhara mengine baada ya kuzitumia?

Manjano au binzari, inaelezwa kuwa mbadala bora wa kuendelea kutibu aleji.

Ni dawa yenye nguvu ya asili kutibu aleji, kwa sababu ina vitu vinavyodhibiti dalili mbalimbali za aleji.

Mtu anahitaji atumie kwa kipindi kirefu binzari mpaka anapoanza kuhisi anapona. Matumizi ya kila mara ya kiungo hicho hayana madhara na mtu anaweza kuitumia kwenye vyakula vingi kama kiungo cha kawaida.

Binzari ina namna nyingi inavyofanya kazi mwilini katika njia zifuatazo:

Manjano ina kitu kinachoitwa ‘curcumin’ ambacho ndicho kinahusika katika kudhibiti dalili mbalimbali za aleji

Kiungo hicho ‘manjano’ kinafanya kazi kama mdhibiti wa asili wa histamini (natural antihistamine). Hiyo inamaanisha kuwa binzari inao uwezo mahsusi wa kuzuia kutolewa histamini mwili wako na hivyo kuzuia dalili na ishara za aleji.

Ni mdhibiti mzuri dhidi ya maambukizi mbalimbali, dhidi ya bakteria, na hivi vyote kwa pamoja vinasaidia kuondoa dalili za aleji. Pia, inaongeza kinga ya mwili ambayo huwa inapotea kama matokeo ya dalili za aleji.

Binzari kwa asili inazuia kuongezeka aina fulani za aleji, kama vile pumu ya koo na matatizo mengine mengine ya mapafu.

Binzari inaweza kutumika kutibu aleji zote. Ile aleji sugu na hata ya kawaida.

Mtu anahitaji kuitumia kwa kipindi kirefu, mpaka anapoanza kuhisi anapona. Matumizi ya kila mara ya kiungo hicho, hayana madhara na mtu anaweza kuitumia kwenye vyakula vingi kama kiungo cha kawaida.

Namna ya kujitibu
Njia ya kwanza: mtu anahitaji binzari ya unga nusu kijiko kidogo cha chai, maziwa ya moto kikombe kimoja, asali na pilipili manga nyeusi ya unga.

Kisha, anachanganya vyote pamoja na kunywa mchanganyiko huo, katika dozi ya kutwa ama mara mbili au tatu kwa siku. Iwapo mtu atakunywa asubuhi, ni vyema akafanya hivyo tumbo likiwa tupu hajala chochote.

Njia ya pili: Ni kuchanganya nusu kijiko cha chai ya binzari cha unga na maji ya vuguvugu kikombe kimoja,

Hapo intakiwa kuongezwa asali kidogo katika kiungo hicho kupata ladha na kisha anayejitibu anywe mchanganyiko huo katika dozi ya kutwa mara mbili, kila siku, hadi hatua ya kupona.

Mtu anaweza kutumia binzari au manjano kama dawa ya nguvu mbadala kujitibu aina mbalimbali za aleji. Ni dawa salama na inayoweza kutumika kwa namna nyingi.

Hivyo, wakati mwingine mtu akipata aleji, si lazima kukimbilia katika duka la dawa. Badala yake andelee na matibabu hayo mbadala.

Tiba ya maji
Kuna uhusiano uliopo kati ya upungufu wa maji mwilini na aleji. Hiyo inatoa somo kwa watu kupanua mtazamo wao kuhusiana na uwepo wa aleji kwa afya ya watu.

Binafsi, kati ya mwaka 2006 hadi 2007, nilisumbuliwa sana na aleji ya vumbi. Wakati huo nilikuwa nikipita sana katika barabara ya vumbi.

Ilikuwa lazima nijifunike pua, maana kila gari ilipopita karibu na kunitimulia vumbi, basi ni lazima nikabiliwe na mwitikio wa kupiga chafya na hata kukohoa.

Baada ya kugundua kuwepo uhusiano huo, wa kuwepo aleji na upungufu wa maji mwilini, nikaaza kuwa mnywaji mzuri wa maji na kugundua kitu kigeni kinatokea katika mwili na afya yangu.

Ndani ya mwezi mmoja tu tangu nianze kufuatilia tiba kwa kutumia maji, basi aleji hiyo ya vumbi ilipotea kiasi kwamba hata gari ukitupa vumbi moja kwa moja kuja usoni kwangu, hakuna chochote kilichonitokea, iwe chafya au kikohozi kilichozoeleka.

Inajihusisha na kazi ya ugawanywaji wa kiasi kidogo kinachopatikana cha maji (maji ya mgawo kutokana na wewe kuendelea kusubiri kiu ndipo unywe maji) wakati wa upungufu wa maji mwilini (Unintentional chronic dehydration).

Chanzo: IPP Media
 
Asante sana mkubwa!

Msongo wa mawazo unaweza sababisha hili tatizo?kwani mimi ni mtumiaji wa vinywaji vyenye vileo ila toka dec2011 kila ninapokunywa bia natokwa na vipele vidogo vidogo vingi maeneo ya mapajani na kwenye ngozi za mikononi. Nikiacha kunywa bia kwa siku mbili vinapotea nateseka sana sijui nifanye nini?

Naomba msaada wako.
 
Si bora uache hiyo pombe mkuu, Kama ndio inayosababisha wewe kutokwa na hivyo vipele pombe bora uiache Kenya unesemaje?.
 
Msaada wa dawa ya asili ya allergy.

If you suffer from an allergic reaction, perhaps a challenge you often face when it comes to finding the most ideal solution is that treatment may cause further adverse reaction and instead, perpetuate the allergy. This wariness is

certainly not unfounded, as some studies have suggested. Allergies may be seasonal like hay fever which can be caused by the immune system's overreaction to an otherwise harmless substance like pollen. This form of

allergy is usually accompanied by sneezing, watery and itchy eyes, nasal discharge and perhaps breathing difficulty. Others like allergic asthma can come from more varied origins like genetic, infectious and nutritional

factors. This type of allergy continues to be on the rise despite modern pharmacological treatments for it. Still, other allergies may solely come from food sources and may cause skin irritation.Most allergic sufferers resort to

antihistamines as a remedy. The problem with these drugs however is that they are also carried to the brain, causing drowsiness and sleepiness. On the other hand, doctors have found that herbal remedies do not necessarily have this side-effect because the mechanisms involved are different from those of medications; herbs

have been shown to protect cells from histamines rather than block them as drugs do. Here are 10 such herbal remedies that have been reported to bring natural relief from allergy:-

10 Herbs For Allergies:

Stinging Nettle(Majani ya Upupu)
Leaves from this plant remain one of the top choices for alleviating the onset of allergic symptoms. They are rich in carotene, vitamin K and quercetin and can be taken in tea or capsule form. From a 2003 human trial, more than half of the

participants confirmed the efficacy of freeze-dried nettle formulations against their allergies while close to half stated this herb worked at par or even better than their usual medications.Licorice:In 2010, a study in Korea demonstrated the effects of licoachalcone, a constituent of licorice, as having antitumor, antimicrobial and anti-inflammatory effects. It inhibits cellular activities that promote allergic

reaction and has been found to have therapeutic potentials to decrease skin inflammation. [SUP][5][/SUP] Researchers have found that the reduced inflammation is due to licorice's ability to enhance cortisol levels or to enable this hormone to last longer without any adverse side effects.

Garlic: (Kitunguu Saumu)Perhaps one of the safest and most accessible methods to prevent or relieve allergy is by taking raw garlic. Like stinging nettle, it contains quercetin which research shows, has anti-inflammatory characteristics [SUP][1][/SUP] and serves as a mast cell stabilizer to keep cells away from histamine-causing inflammation.

Bromelain: (Nanasi) Well, this is not an herb in itself but could be considered a herbal remedy as it is a natural enzyme that is extracted from the stems of pineapples. Some studies show that bromelain can help reduce nasal swelling and mucus production to make breathing easier such as during sinus infections. Accordingly, a 2012 experiment on mice revealed bromelain's significant anti-inflammatory activities along the lungs, confirming its therapeutic value for allergic asthma sufferers.

Butterbur: Some medical experts hail butterbur as having the most promising results among all herbal supplements to prevent air passageway swelling because of its leukotrine inhibiting effects. Other findings show that extracts of this herb's roots are equally potent as prescriptive drugs like Zyrtec and Allegra but without causing drowsiness.

Sida cordifolia (aka. bala, country mallow, heart-leaf sida or flannel weed)... native to India, Sida cordifolia is reported to have anti-inflammatory and decongestant effects and has traditional use in asthma, bronchitis and nasal decongestion. It is contraindicated in individuals with a history of heart disease as it can raise blood pressure and heart rate.

Phleum pretense Extensive studies had been conducted to determine the effects of using pollen extract from phleum pretense in dealing with various allergy symptoms. Majority of the results showed that the extract has the ability to eliminate symptoms like eye irritation and fever in people suffering from allergies. When put under the tongue, phleum pretense is believed to be effective in relieving the symptoms of grass pollen allergies or hay fever. When injected into the skin, this herb can eliminate the symptoms of hay fever and some seasonal allergies. Some researches even believe that administration or using this herb for 3 years to children can significantly reduce their susceptibility to asthma.

Tinospora cordifolia Widely used in India as treatment for various health conditions, results of initial studies show that Tinospora cordifolio has the potential in the treatment and management of allergy symptoms. Results showed that intake of Tinospora cordifolio tablet can help in eliminating nasal discharge, itching and sneezing which are considered as one of the most common symptoms of allergy. One study involving 75 patients diagnosed with hay fever or allergenic rhinitis were given with tinospora cordifolia to test the claims on the healing capacity of tinospora cordifolia. Based on the results of the study, it was found out there has been a significant statistical reduction in the symptoms experienced by the patients.

Ginkgo biloba Best known for its cardiovascular benefits, intake of ginkgo biloba has also shown to be important in managing asthma and allergy. Aside from the fact that it contains highly potent anti-inflammatory chemicals, ginkgo biloba is also packed with seven antihistamines which make it an effective natural reliever to allergy symptoms. Also, ginkgo biloba contains ginkgolides which are scientifically proven to be effective in relieving asthma attacks, allergy and other lung problems. It actually relieves inflammation by eradicating free radicals. Furthermore, it allows better entry of oxygen into the lungs so sufferers are able to breathe easily and freely.

Reishi Mushroom Hailed as the medicine of kings or mushroom of immortality, reishi mushroom is a potent herb that offers astounding health benefits. For thousands of years, reishi has been used by ancient Japanese and Chinese cultures as medicine.Researchers have finally found out what makes reishi mushroom effective in eliminating allergy symptoms. Reishi contains high amounts of lanostan compounds which act as natural antihistamines. Lanostan in reishi helps in controlling the release of certain chemicals within the body thereby inhibiting the release of histamines also.

Note Some herbs are known to trigger allergies in some individuals. The most commonly allergenic herbs and spices include oregano, cinnamon, black and white pepper, mint, paprika and cumin.

 
Wadau,

Nina allergy ya mafua ambayo nimeipata ukubwani nilipofikisha miaka 30 hivi. Mpaka sasa nasumbuliwa na strong perfumes, harufu ya baadhi ya sabuni za kuogea, kufulia na harufu zingine kali.

Naomba kujua dawa nzuri itakayonitibu au hospitali nzuri wanayotibu allergy kwa hapa Dar.

Nawasilisha
 
Hiyo inaitwa type I hypersensitivity reaction

Pole sana. Hebu elezea zaidi unapatwa na dalili gani ukisikia hizo perfume. Mf. Kifua kubana, ugumu wa kupumua, n.k
 
Mkuu gasgas,

Pua huanza kufukuta then naanza kupiga chafya nyingi ambazo baada ya muda mfupi mafua huanza kuchuluzika. Pia kichwa huuma wakati mwingine. Nimekuwa natumia piriton ili kukausha lakini lazima nilale walau saa moja ili yakauke. Nisipolala hata nikimeza piriton kiasi gani hayakauki.
Kifua hakibani
 
Aisee ukipata ufumbuzi na mie nisaidie.Nikiwa form five nilipatwa na allergy.Kilichotokea macho yakawa yanavimba nikaambiwa ni mafuta ya pamba wanayopikia chakula nikaambiwa na vumbi na harufu kali asikwambie mtu niliteseka sana nikajaga kupasuliwa ule uvimbe wa macho so sikuwahi kuvimba tena ila nikisikia vumbi kidogo au harufu kali ya perfume kama mara nyingi napata shida kupumua na kupiga chafya sana nimemeza midawa weee lakini siponagi sijui kwanini tu
 
Mkuu gasgas,

Pua huanza kufukuta then naanza kupiga chafya nyingi ambazo baada ya muda mfupi mafua huanza kuchuluzika. Pia kichwa huuma wakati mwingine. Nimekuwa natumia piriton ili kukausha lakini lazima nilale walau saa moja ili yakauke. Nisipolala hata nikimeza piriton kiasi gani hayakauki. Kifua hakibani

Kuna bidhaa mbili nashughulika nazo hapa nadhani zinawez kukusaidia. Ya kwanza inaitwa splina chlorophyll drink ina hivi ndani yake

Chromium; Stimulates fatty acid and cholesterol synthesis and an activator of of several enzymes. Phosphorous; Assists in the contraction of muscles in functioning of kidneys, maintaining of regularity of heartbeat
Potassium; It is necessary for muscle building and normal body growth.
Zinc - helps in cell division and cell growth for faster wound healing.
Selenium - Provides protection from the toxic effects of heavy metals and other substances. It helps to boost the sperm count in men.
Vitamin E - Nourishes the skin and keeps the brain active.
Vitamin C - Promotes healthy teeth and gums. Increases alertness and possesses anti-cancer properties.
Vitamin A - Helps in the formation and maintenance of healthy teeth, skeletal and soft tissue, mucous membrane and skin. Promotes good vision. Strengthens the heart function.
Folic Acid: Acts as a co-enzyme with vitamin B12 and Vitamin C in the breakdown and synthesis of hormones and cholesterol.
Pantothenic Acid: Essential in the synthesis of hormones and cholesterol
Calcium: important for growth and reproduction of human body, maintains also healthy teeth and bones.
Magnesium: Helps in Muscle relaxation and contraction
Iron: Essential to the formation of hemoglobin which carries the oxygen in the blood and muscles.

Ya pili inaitwa Bubble C.

Mimi nimetumia splina na imenisaidia sana. Ilikuwa haipiti wiki sijapata mafua hasa nikisikia vumbi au perfume ngeni/kali
kwa sasa yamepungua sana na nadhani nikimaliza nitakuwa nimepona.
 
OLEWAO,

Kama ni kweli hayo mafua yanasababishwa na allergy basi dawa sahihi kwako ni avamy's nasal spray ambayo utaweza kuitumia hata kila siku asubuhi kabla ya kwenda kwenye shughuli zako.itakusaidia kukufanya uwe fresh siku nzima.

Nenda kwenye duka la dawa au kainunue kisha hakikisha unapata maelekezo vizuri namna ya kuitumia.bei ni kati ya buku 15 mpaka 20.kila la heri mkuu.
 
Mimi ni wakala, na pia mtumiaji. Kama ungependa kujua zaidi nicheki kwenye 0685661790 ntakupa maelekezo zaidi

Mie naomba kujua yanacost shilingi ngapi? Na matumizi yake yakoje kama hautojali ili wengine pia watakaokuwa wanahitaji.
 
Mimi natatizo la mafua kila mara, tena hasa wakati wa asubuhi nikiamka napiga chafya na kutoa kamasi nzito.
 
Allergy yangu ndio balaa kila nikiamka asubuhi chafya hata hamsini napiga harufu ya pray mie shida kukiwa na vimbi shida kipndi cha baridi napo na shida koo linaniwasha halijawahi kupona vipele majani na kwenye mikono karibu na mabega tena mikono yote kivaa nguo kata mikono siwezi.nimehangaika sana mahospitalini hakuna kitu natupa tu hela sina raha na mwili wangu kwa kweli. MziziMkavu naomba msaada kwa hilo.
 
Pole sana mkuu. Una tatizo kama la mke wangu, yaani ni shida kwa kweli. Ngoja tusubiri msaada hapa.
 
Hukisoma hapo unaambiwa epuka hizo mambo. Wa pombe acha wa mafua na kamasi. Pole sana.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…